Zitto aanika siri nyeti za Mbowe! Adai hatakufa kama Chacha Wangwe
haponi msaliti yoyote hapa. ni kukatwa tu nakusonga mbele kuanza upya siyo ujinga,Mungu yupo atawanyosha tu
 
....hata mimi nasema ni utoto tu,akikua/pakipoa ataacha...
 
Haijalishi Zitto amesema wakati gani, lakini je ni sahihi kwa hao viongozi kupita kila sehemu kuita wengine mafisadi huku wanapokea michango ya hao hao mafisadi?

Zitto anaweza kuwa na makosa yake kwa kuficha taarifa hii, lakini kwa sisi kama wananchi amefanya la maana kusema ukweli huu. better late than never. Na sasa tunajua kumbe Mbowe anachukua pesa kwa akina Rostam na Mkono.

Jamani mmeanza kusahau hii vita chanzo chake, chanjo ni Zito Kabwe kuonyesha nia ya kuwa mwenyekiti wa taifa wa chadema ndio vita inaendelea Je kama zito angesema siku nyingi Habari hizi za mbowe kupokea pesa kwa vigogo wa CCM ingekuaje kwa zito, kuweka nia ya uenyekiti yamemkuta haya!
 
Siyo vibaya kupewa pesa na Kikwete au CCM ~ Freeman Mbowe.

Kwi kwi kwi kwi!
 
Huyu Nimrod Mkono alikuwemo katika list ya mafisadi iliyowekwa hadharani na Dr Slaa pale mwembechai. Hivi huyu Mkono kama angekuwa ana ushahidi wa kuonyesha undumilakuwili dhidi ya Dr Slaa na Mbowe kweli angeshindwa kufanya hivyo miaka yote hii!? Kwanini hiki Kirus kama kulijua uchafu huu miaka yote hii kikae kimya hadi kilivyoadhirika ndio kianze kubwabwaja!? Mkono ni lawyer aliyebobea kama ana ushahidi wa kina kuthibitisha maneno ya mhaini kuhusu hizo milioni 40, milioni 200 za kutoka kwa Mkono na milioni 100 za kutoka kwa Rostam basi auweke hadharani.

Kwa maandishi yako ambayo huwa ninayasoma ninaamini kwamba wewe ni msomi na muelewa wa baadhi ya mambo.

Kikawaida ndoa ni mpaka ivunjike ndio watu wa nje tutajua ni mangapi wamevumiliana.

So unatakiwa usiwe na upande kwanza ili ufanye informed decision, fikiria kama ni kweli Mbowe kapokea hizo fedha kutoka kwa watu hao, Rostam na Mkono chama kiko salama?

Zitto hastahili kubaki, lakini ni lazima tuhakikishe kuwa tunaobaki ni wenye mlengo mmoja.
 
Funguka ZZK,funguka,ndio usaliti wako unapoonekana,mbona hayo yote hukuwahi kuyasema?Kwa hiyo mafisadi kama wako CDM unawafumbia macho,mnafiki mkubwa,yako wapi ulivyokuwa unajipambanua unapiga vita rushwa,kumbe umewafuga ndani ya chama;unasubiri wanamwaga mboga unamwaga ugali!!Unajidhalilisha tu Zito,its better u shut up!!Kumbe kweli --------- kwa kuwa wakubwa zako ----------,utateteaje tena mali za Umma Zito kama sio unafiki?!

Ok, labda ni kweli tunahitaji majibu yaliyonyooka juu ya hilo kutoka kwake...na wakati huohuo tuwageukie hao wengine wanaojiita wapambanaji ndani ya chadomo...tukianza na Tundu Lisu (mwanasheria)....ni wazi anayajua haya...je ameshachukua hatua gani mpaka sasa ? ...Mnyika, Mdee......nao watoke mbele watuambie kuwa wapo ndani ya chama kuchumia tumbo tu na hawana nia yoyote ya kuisaidia nchi.......SHAME ON YOU ALL.....
 
Well noted! Zitto tumemrushia tuhuma za kutosha na binafsi sina mjadala tena juu ya usaliti wa Zitto.

Lakini hizi za Mbowe nazo ni tuhuma.Zijibiwe tupime!

Sheria msumeno tunataka Wapinzani sio Wakinzani!!

Ndo maana napendaga quotes zako umenikuna kwa kutofumbia kufumbia macho upande wa pili wa shilingi
 
itajulikana tu acha wapelekane kwanza,African politics
 
Kuleta tuhuma mpya na kuhalalisha kuwa zako ni za kweli ni kukiri hufai kabisa na kwamba hutaki kuondolewa peke yako which is the fact, you must go! Pia umethibitisha Mbowe alipokea hela ikatumiwa na chama we umepokea kwa ajili ya kuisaliti CDM na watz na kuanza kujijenga kwa maslahi yako sasa kimenuka be wise otherwise unaendelea kujimaliza kaka!
 
Well noted! Zitto tumemrushia tuhuma za kutosha na binafsi sina mjadala tena juu ya usaliti wa Zitto.

Lakini hizi za Mbowe nazo ni tuhuma.Zijibiwe tupime!

Sheria msumeno tunataka Wapinzani sio Wakinzani!!
Zimejibiwa hivi


Majibu ya Mbowe

Akizungumza na mwandishi wetu Mbowe alisema ni utoto kukwepa kujibu hoja kwa kuanzisha tuhuma dhidi ya mtu mwingine ambazo si za kweli.

"Mimi nimekuwa nikisimamia ukweli, mtu anapotuhumiwa ni lazima ajibu tuhuma hizo. Ni utoto kuacha kujibu tuhuma na kuzusha tuhuma nyingine. Anapaswa kufanya utetezi wa tuhuma zinazoelekezwa kwake.

"Mimi ni mbunge, bungeni nimekuwa nikichangia watu mbalimbali mimi kama Freeman, si ajabu watu wengine kunichangia. Hapa jambo la msingi ni kwamba unapewa pesa kwa sababu gani, kwa nia ipi? Kupewa pesa na Kikwete au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa malengo gani?" alihoji Mbowe.

Mbowe alilaumu baadhi ya vyombo vya habari kushiriki kumchafua kwa taarifa za kutunga kutoka kwa watu anaodhani wamekuwa na uhusiano na Zitto.
 
Zitto hajachelewa kusema
ukweli ukizingatia CDM hawapendi kuambiwa ukweli wa udhaifu wao. Kaka
Zitto funguka zaidi kuhusu deal la Kinana na Sumaye maana umetuacha njia
panda. Pia usisahau lile la NHC na NSSF sisi tunataka kujua ili
tuchague pumba na mchele.

Kama unajua Chacha wangwe alichofanyiwa pls tenda Polis ukawape ukweli
wote haki ichukue mkondo wake.

Lete petrol mimina kwenye hizi kuni mpaka kieleweke. Waliambiwa watumie busara wakagoma.
 
Kama habari ya Lissu na hiyo ya Zitto kuhusu kutoa na kupokea rushwa ni za kweli hakuwezi kuwa na makosa ya kijinai (ukiacha ya kimaadili)? Wametajwa Mkono na Rostam (kama watoaji) na pia wametajwa kina Sumaye na Kinana (wametoa/wamepokea?)- wote hawa ni wa CCM! Wanatajwa pia wapokeaji: Mbowe na Zitto. Takukuru mpo? Kesi rahisi sana hii.

Wasiwasi wangu ni kuwa inaweza kuishia kama habari ya mabilioni ya uswisi - chini ya kiapo wanasema hawajui chochote, nje wanasema wana ushahidi!
 
Mbowe toa maelezo ya kutosha kuhusu haya mambo, mana Zitto mi nishamdelete so tuhuma dhidi yake hazina maana kwangu.
 
Zitto ametuhumiwa na chadema kama chama lakini yeye anamshambulia mbowe .why? Anazidi kuonyesha kuwa waraka wa mabadiliko 2013 waliuandaa
 
Nimeipenda hii quote:

Si vibaya kupewa pesa na CCM na Kikwete - Mbowe

Jamani pesa tamu sana.
 
mimi binafsi zito nilimtilia mashaka kitambo sana, na nilijua tu siku yake itafika sasa yametimia.
 
Back
Top Bottom