Zitto aanika siri nyeti za Mbowe! Adai hatakufa kama Chacha Wangwe
Ajibu wapi? Humu JF?
Zitto ana haki ya kujibu tuhuma kupitia njia zile zile maadui zake wanazotumia. Wanatumia JF, Facebook, na blogs mbalimbali bila ya kusubiri jibu rasmi kwenye kikao.
Wana behave kihuni na ana respond kihuni, binafsi sipendi aina hiyo ya malumbano maana yanakidhoofisha chama, lakini ni vigumu kunyamaza tu ukirushiwa kila aina ya matusi, kebehi, kennel I na uzushi!
Sasa ni wakati wa kuingia ndani, kuzungumza bila ya kumpa faida adui kwani maadui wa CHADEMA wanarukaruka kwa furaha kila wanapotuona tukivuana nguo hadharani!
Msimamo wangu mimi ni kwamba inawezekana ndugu hao walikosea, lakini chama kime over react katika suala hili ambalo lingeweza malizwa kistaarabu na bila ya kukijeruhi chama. Nauliza tena hivi ni nani huyu aliyeturoga hadi tunahangaikia issue ya watu watatu, wanne na kusahau mambo muhimu kabisa kwa nchi kama Katiba, madawa ya kulevya yaliyotamalaki na utoroshwaji wa kutisha wa nyara za taifa na manyang'au hawa CCM?

Watu hao hao watatu wanne wa uongozi wa juu wa CHADEMA wametuonesha kwamba zile hadithi zote za ufisadi and list of shame zilikuwa ni habari za danganya toto tu, na wao wanaabudu katika madhabahu hayo hayo.

Na kwa kutaka kumminya Zitto asipate haki yake ya kusikilizwa na Baraza Kuu, wametoa nafasi ya malumbano yao ya ndani kujulikana nje.

Kama ulifikiri CHADEMA kilikuwa chama kilichokuwa tayari kukomboa Watanzania fikiri tena.

Bila kuvaa miwani ya kioo chenye rangi ya "kipendacho roho hula nyama mbichi".

Unaposema "inawezekana ndugu hao walikosea" unaonesha cognizant dissonance ya hali ya juu.

Huku si kukosea tu, useme nilikuwa sijui mlango wa mbele uko wapi nimeingilia mlango wa uani kwa bahati mbaya. This seems to be a deliberate scam with some intricate planning to protect personal interests, how would you let them off the hook that easily if the allegations carry weight?

Especially if their entire careers are based on fighting graft?
 
Alikuwa akiwaheshimu Viongozi wenzie ndio maana alikuwa akiwafichia maovu yao ila kwakuwa watu wenyewe hawana wema sasa ndio ameanza kuyasema aliyopaswa kuyasema miaka mingi iliyopita.
uadilfu anavuka mipaka ya kuficha siri za watu unaowaheshimu.
 
Mtanzania mwenzangu Zitto Kabwe, umekuwa very reactive. Be cautious and control your emotions. Unaanza kuexpose your weakest side.

Unarejea matukio ya 2005 leo 2014, ulikuwa wapi? Unatuaminisha umenyamazia mangapi ktk taifa hili? On every action theres equal and opposite reaction. DID U?

WAMEMWAGA UGALI? Unamwaga mboga wakati wenzio weshashiba??!!

So kina mbowe lissu na slaa wanataja mambo yaliyotokea 2013 tu na ya 2014?? Hivi mkoje?! wakisema kina lissu mambo ya 2009 ni sawa, akisema zzk ni kosa. Hii kali ya mwaka.
 
Ajidhaniaye amesimama na aangalie asianguke! ZZK ni bora angekaa kimya akubari matokeo. kwa hicho alichokiandika,anazidi kujiharibia haiba yake kwa jamii.kama kwa muda wote wote mambo yalipokuwa shwari alinyamazia maovu ya ndani ya chama chake, kwa sasa hana tena ushawishi kwa jamii ya kutetea mali za umma. siasa za bongo bana!

Kwahiyo unataka kusema nn mkuu?
 
Pole mkuu, ndio nchi yetu hii, inakila kitu cha kufanya maisha yawe mepesi kwa wananchi wake, ila imekua kinyume chake. Nafikiri tuwe wavumilivu maana haya yana mwisho wake mkuu.

Poa mwana JF mwenzangu!Acha mm niende Tanesco-Kinondoni nikaongee nao maana asubuhi nilinunua LUKU ya 10,000 hata saa 8 haijafika imekwisha!

Maisha magumu sana kwangu na ongezeko hili la umeme
 
Kwani alikuwa anajua kwamba atatolewa mpaka awepo?

Aaaah! Rafiki yng naona wanchokoza taratibu!

Miaka ya 2000 Mwanzoni Mh Lipumba aliwahi kuandamana na akakumbana na nguvu ya dola akaumia mkono!

Mchungaji Mtikila nae pia amewahi kua na kesi kibao mahakamani!

Baadhi ya wabunge na viongozi na makada Wa Cdm wamewahi kumbana na nguvu ya dola na wengine wana makesi mahakamani!

ZZK Mbona sijawahi kusikia kukumbana na nguvu ya dola au kua na kesi mahakamani zaidi ya hiialiyoifungua mwenyewe?

Napia ata vurugu zilipotokea bungeni sizani Km alikuwepo. Kwanini asiwepo?

Ninachojua ZZK aliwahi kupata adhabu tu bungeni miaka ya nyuma! Tafakari sn ndugu!

Nafikiri nitakua nimekujibu swali lako!
 
tuhuma hizo ni za kijinga kwakuwa hata yeye aliendelea kukaa kimya ndani ya chama akiona yote yaliotendeka hata ilo analodai la chacha na hayo mengine, leo wanamfukuza anaanza kujitetea, huyu ni kama mgonjwa wa sijui nini anataka kuleta msemo wa tufe wote. hapati kitu hapa.kick ya ass kick ya ass.gif
 
Leo nikiwa makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Willibroad slaa amerusha kombora kwa Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa CHADEMA Mheshimiwa Zitto Kabwe.


Kwa mujibu wa Dk Slaa,Zitto kabwe ni mnafiki mkubwa kumuhusisha mwenyekiti wa CHADEMA taifa mheshimiwa Freeman Mbowe na ufisadi wa kupokea pesa kutoka kwa Mheshimiwa Nimrod Mkono.


Dk Slaa amesema,ZITTO alikuwa wapi kufichua ufisadi huo hadharani wakati wa vikao vya chama tangu mwaka 2005 aje atoe shutuma na malalamiko yasiyo na ukweli leo anaposhughulikiwa na chama???.


Dk Slaa amesema, lengo la ccm,Zitto na vibaraka wote wa ccm akiwepo Habibu Mchange ni kutaka Mbowe na Dk Slaa wakosane ili chama kiyumbe ili wapate pa kusemea. Dk Slaa amesema Ccm na vibaraka wake walifanikiwa kuiangamiza NCCR-Mageuzi, TLP na UDP lakini mbinu hiyo chafu inayotumiwa na Ccm kupitia kwa Zitto haitafanikiwa kuiua CHADEMA.

Mapambano yanaendelea.

Kwani chadema walikuwa wapi toka huko nyuma kusema wanayosema leo kuhusu zzt? Mbona nyinyi mnazungumza vitu ambavyo mlipaswa kisema long time ago, acheni unafiki au ndio mkuki kwa ngurue, Lisu ulikuwa wapi kusema hayo, alafu eti uko majakamani kudai haki mnafiki mkubwa
 
Watu hao hao watatu wanne wa uongozi wa juu wa CHADEMA wametuonesha kwamba zile hadithi zote za ufisadi and list of shame zilikuwa ni habari za danganya toto tu, na wao wanaabudu katika madhabahu hayo hayo.

Umesahau Mabere Marando ni wakili wa baadhi ya hao mafisadi....?
 
Ulikua unajinasibu kua wewe ni mfuatiliaji Wa Siasa za Tz na kimataifa! Lkn kwa Jibu lako hili wewe ni mshabiki Wa mtu binafsi! Kwasababu wapinzani wote bungeni walitoka nje kupinga kuburuzwa ktk kujadili swala la katiba mpya kwa uchache wao kasoro Mh Mlema!

Sasa hapo ukimsifu Huyo ZZK wakati hajaonesha kupigania ata swala la katiba mpya sikuelewi!

sema mazoba cdm ndo walitoka kwa kujidai wanajua kumbe wanautindio wa ubongo
 
Mtanzania mwenzangu Zitto Kabwe, umekuwa very reactive. Be cautious and control your emotions. Unaanza kuexpose your weakest side.

Unarejea matukio ya 2005 leo 2014, ulikuwa wapi? Unatuaminisha umenyamazia mangapi ktk taifa hili? On every action theres equal and opposite reaction. DID U?

WAMEMWAGA UGALI? Unamwaga mboga wakati wenzio weshashiba??!!
mbowe atabaki salama , zitto atabaki ana weweseka . hizo ni siasa za kina mwigulu na kibajaji, si zitto shtuka heshima yako itaondoka bila sababu wakati bado una hitajika , kwani kukataliwa chadema si mwisho wa siasa
 
Hatukutegemea uondoke hivihivi hii ni dalili kwamba mwisho umefika, lete tuma nyingine ........
 
sema mazoba cdm ndo walitoka kwa kujidai wanajua kumbe wanautindio wa ubongo

Hao mazoba ndio waliitwa ikilu kusikilizwa!

Pole sn! Mmegundulika njama zenu! Mlizoea Kunywa Damu za vyama vya Siasa ila kwa Cdm itawanywa nyie!
NCCR mmeinywa
Cuf mmeinywa
Sijui Udp sijui Tlp vyote mmevinywa!

Cdm hainyweki!
 
Chadema nawapenda sana wako kikazi zaidi wanapiga dili mpaka shetani hapendi, pesa za michango kukikopesha chama tena! Hii nimeipenda halafu chama kikilipa zinakwenda wapi? Sasa watahutubia kuku maana hata watoto watawakimbia.
 
Wakuu, inasemekana Zitto Kabwe ali-post facebook hii kitu halafu aka-edit later.

Original post:

Revised Post:


Kutoka Gazeti la Raia Tanzania
Kiongozi mzuri ni yule ambaye anajizuia kutoa matamshi wakati anahisi kvulugwa. Kitendo cha ZZK kukimbilia kutoa hoja dhidi ya Mbowe kimemfunua yeye kiongozi wa jazba tena asiye na uvumilivu.Nampenda sana rais wangu JK kwa jinsi ambavyo ni mvumilvu na si mwepesi wa kusema. Zito umepungukiwa na hekima tu
 
AMA KWELI FADHILI MBUZI UTAMLA NYAMA.............

Nampa pole sana Mh Freeman Mbowe, mwenyekiti wa Chadema Taifa kwa kutukanwa na kukosewa adabu na kijana mdogo, Msaliti Zitto Kabwe, ambaye leo mafanikio yake yametokana na yeye Mh Mbowe, lakini kasahau na kaamua kukutuna ati wewe ndo kamati kuu!

vile vile nimpe pole Mh Tundu Lissu Mbunge wa Singida mashariki na Mwanasheria wa chama, kwa kuitwa Kifaranga na huyu kijana ----- asiye na Adabu, we mpuuuze kwani leo amewadhihirishia watanzania kuwa hafai hata kuwa Balozi wa nyumba kumi......

Zitto Z Kabwe mpaka sasa hujakanusha tuhuma za kweli kabisa kwamba ulihongwa Magari mawili na Mh mkono iliusimsimamishe mgombea Msoma Vijijini, badala yake uliishia kujitoa ufahamu na kuwatukana Viongozi mtandaoni kuonyesha ulivyofilisika mawazo kama si kufilisika hoja!

Zitto Kabwe amejitoa ufahamu na kudai eti mtu asiyemuheshimu mke wake aliyewazalia watoto wake hawezi kumfundisha mtu maadili.......
Zitto, kabla ujanyoosha kidole kwa mwenzako embu jaribu kujitazama wewe mpaka leo una umri miaka 37 umeshindwa kuoa, na kinacho kusumbua ni uzinzi, embu kumbuka April tukio la aibu ulilolifanya pale Mount Meru Arusha, baada ya kunywa KONYAGI, mbona sisi hatusemi..........

Si jambo jema kujadili misha ya Binafsi ya Kiongozi, kwani hakuna aliye mkamilifu Chini ya Jua.......

SI VEMA MAAMUZI YA KAMATI KUU KUMBEBESHA MH MBOWE NA LISSU PEKE YAO..

..well noted!!
 
CHADEMA mabingwa Mh. Mkono kwa inategemea wakati gani, kuna wakati anaitwa fisadi alafu pia kuna wakati ni Mfadhili... haya yote yanatoka kwa vinywa na maandishi ya viongozi wa CDM; Hongereni kwa kuchezea umma wa waTanzania.
We zimpopopompo umeshamuuliza Mkono akakuhakikishia kuwa aliihonga CDM au unatoa mapovu kama omo. Mkono aihonge CDM kwa hofu ipi alokuwa nayo wakati jimboni kwake anakubalika.
 
Mwisho wa jina la Zito katika siasa za Tanzania. Rangi kamili ya Zito inaanza kuonekana.
Zitto hafai kuwa kiongoz, ameonesha ni mtu dhaifu sana ambaye hana uvumiliv na staha ya uongozi. Zito nenda hufai kabisa kuwa kiongoz
 
Back
Top Bottom