Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Ajibu wapi? Humu JF?
Zitto ana haki ya kujibu tuhuma kupitia njia zile zile maadui zake wanazotumia. Wanatumia JF, Facebook, na blogs mbalimbali bila ya kusubiri jibu rasmi kwenye kikao.
Wana behave kihuni na ana respond kihuni, binafsi sipendi aina hiyo ya malumbano maana yanakidhoofisha chama, lakini ni vigumu kunyamaza tu ukirushiwa kila aina ya matusi, kebehi, kennel I na uzushi!
Sasa ni wakati wa kuingia ndani, kuzungumza bila ya kumpa faida adui kwani maadui wa CHADEMA wanarukaruka kwa furaha kila wanapotuona tukivuana nguo hadharani!
Msimamo wangu mimi ni kwamba inawezekana ndugu hao walikosea, lakini chama kime over react katika suala hili ambalo lingeweza malizwa kistaarabu na bila ya kukijeruhi chama. Nauliza tena hivi ni nani huyu aliyeturoga hadi tunahangaikia issue ya watu watatu, wanne na kusahau mambo muhimu kabisa kwa nchi kama Katiba, madawa ya kulevya yaliyotamalaki na utoroshwaji wa kutisha wa nyara za taifa na manyang'au hawa CCM?
Watu hao hao watatu wanne wa uongozi wa juu wa CHADEMA wametuonesha kwamba zile hadithi zote za ufisadi and list of shame zilikuwa ni habari za danganya toto tu, na wao wanaabudu katika madhabahu hayo hayo.
Na kwa kutaka kumminya Zitto asipate haki yake ya kusikilizwa na Baraza Kuu, wametoa nafasi ya malumbano yao ya ndani kujulikana nje.
Kama ulifikiri CHADEMA kilikuwa chama kilichokuwa tayari kukomboa Watanzania fikiri tena.
Bila kuvaa miwani ya kioo chenye rangi ya "kipendacho roho hula nyama mbichi".
Unaposema "inawezekana ndugu hao walikosea" unaonesha cognizant dissonance ya hali ya juu.
Huku si kukosea tu, useme nilikuwa sijui mlango wa mbele uko wapi nimeingilia mlango wa uani kwa bahati mbaya. This seems to be a deliberate scam with some intricate planning to protect personal interests, how would you let them off the hook that easily if the allegations carry weight?
Especially if their entire careers are based on fighting graft?
