Zitto aanika siri nyeti za Mbowe! Adai hatakufa kama Chacha Wangwe
Watu hao hao watatu wanne wa uongozi wa juu wa CHADEMA wametuonesha kwamba zile hadithi zote za ufisadi and list of shame zilikuwa ni habari za danganya toto tu, na wao wanaabudu katika madhabahu hayo hayo.

Na kwa kutaka kumminya Zitto asipate haki yake ya kusikilizwa na Baraza Kuu, wametoa nafasi ya malumbano yao ya ndani kujulikana nje.

Kama ulifikiri CHADEMA kilikuwa chama kilichokuwa tayari kukomboa Watanzania fikiri tena.

Bila kuvaa miwani ya kioo chenye rangi ya "kipendacho roho hula nyama mbichi".

Unaposema "inawezekana ndugu hao walikosea" unaonesha cognizant dissonance ya hali ya juu.

Huku si kukosea tu, useme nilikuwa sijui mlango wa mbele uko wapi nimeingilia mlango wa uani kwa bahati mbaya. This seems to be a deliberate scam with some intricate planning to protect personal interests, how would you let them off the hook that easily if the allegations carry weight?

Especially if their entire careers are based on fighting graft?


....Chadema Chadema Chadema Pepoziiiiiiiiiiiiiiii power!!! X2

dadadek bahari nauchafu ni kama mbingu na dunia!!!


...
 
Kwa tuhuma hizi nzito alizozitoa mh. Zitto Kabwe dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema mh. Freeman Eikaeli Mbowe, Chadema inabidi ijibu coz its very serious na wakikaa kimya ina maana yanayosemwa na mh. Zitto dhidi ya mh. Mbowe ni ya kweli...basi Chadema haitakuwa na locus standi ya kunyooshea watu kwa tuhuma za ufisadi na michezo michafu...tunamtaka mh. Mbowe atoke kukanusha au tuziamini.

Akanushe ili iweje wakati kishakubali kuwa Baniani mbaya kiatu chake dawa..........!!!!!!

“Mimi ni mbunge, bungeni nimekuwa nikichangia watu mbalimbali mimi kama Freeman, si ajabu watu wengine kunichangia. Hapa jambo la msingi ni kwamba unapewa pesa kwa sababu gani, kwa nia ipi? Kupewa pesa na Kikwete au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi, kwa malengo gani?” alihoji Mbowe.
 
Kwa tuhuma hizi nzito alizozitoa mh. Zitto Kabwe dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema mh. Freeman Eikaeli Mbowe, Chadema inabidi ijibu coz its very serious na wakikaa kimya ina maana yanayosemwa na mh. Zitto dhidi ya mh. Mbowe ni ya kweli...basi Chadema haitakuwa na locus standi ya kunyooshea watu kwa tuhuma za ufisadi na michezo michafu...tunamtaka mh. Mbowe atoke kukanusha au tuziamini.


Ayapeleke mahakamani na waliotoa pesa watasema ukweli ikijulikana ndio useme haya unayoyasema. lakini kwa haya ya Zitto kuongea baada ya kutaka kuvuliwa kwenye chama hayana mashiko amechelewa haya alitakiwa hayatoe mwaka 2012 akiwa bado yuko kwenye chama. Hapa ni kilio cha samaki... yatapita ila yeye ndie anaelekea kule kwa Lyatonga
 
R.I.P Chacha Wangwe, waliokusaliti leo wanapigana, damu yako inawaandama.
 
Alikuwa wapi siku zote hizi? Mpaka kinuke ndio aseme? Huu ni uongo. Zito hafai
 
Malezi ya baba na mama yana nafasi kubwa sana ktk maisha... Malezi ya Mama pekee kwa mtoto wa kiume...nashindwa hata kupangilia hoja yangu! hope mmenielewa...
 
Bora ufukuzwe chadema zitto Damu za watu bado zinakulia zito huwez kuuwa kwa upanga nawe uwe na Aman unahaki ya kupata unachokifanyia chama toka 2008. Safi na bado nenda ccm utapewa cheo cha mwigulu au kama vp potea kama wengne tuu .
 
Kweli Tindu Lissu ni kifaranga tu...haya mambo ya Mkono,Mbowe na Zitto wanayajua hawa watatu vizuri sana,kuyaingilia asiyoyajua ni kujidharirisha kama hivi....

Mkono anasema hajawahi kuwa na issue yoyote ya kuongea na Lissu zaidi ya mijadala ya kibunge sembuse hayo ya kumpa fedha Zitto aliyodai ameyapata kwa Mkono.Ndio tatizo la kifaranga kuingilia ugomvi wa mama yake.

MAMBO MSETO 24: LISSU MATATANI, ZITTO, MKONO WAMPA VIDONGE VYA MAUMIVU MAKALI

Zito katekenywa tu, anaanza kuimba, je akifikishwa itakuwaje?
 
mbowe atabaki salama , zitto atabaki ana weweseka . hizo ni siasa za kina mwigulu na kibajaji, si zitto shtuka heshima yako itaondoka bila sababu wakati bado una hitajika , kwani kukataliwa chadema si mwisho wa siasa

Mbowe hatabaki salama, credibility yake kama kiongozi imeshuka mno, ameonesha upeo mdogo wa uongozi kwa kuiingiza cdm katika mgogoro usio wa lazima, Hana maadili, hamheshimu mkewe, Kumbe anachukua hela kutoka CCM.

Zitto ana future, ni mtaji wa kisiasa kwa chama chochote atakachoamua kujiunga nacho, isitoshe dynamics za vyama vya siasa na hali yaq kisiasa itabadirika sana ikija katiba mpya.

Kwa hiyo wa kulaumiwa ni Mbowe, kwa kuharibu kazi ya mikono yake mwenyewe!. MBOWE HAWEZI KUQUALIFY KUCHUKUA UONGOZI WA JUU WA NCHI HII, AT THE END OF THE DAY ATABAKI CHINI YA MTU, LABDA ANG'ANG'ANIE UENYEKITI TU!
 
Hao mazoba ndio waliitwa ikilu kusikilizwa!

Pole sn! Mmegundulika njama zenu! Mlizoea Kunywa Damu za vyama vya Siasa ila kwa Cdm itawanywa nyie!
NCCR mmeinywa
Cuf mmeinywa
Sijui Udp sijui Tlp vyote mmevinywa!

Cdm hainyweki!

mkuu nakusoma taratibu lakini siasa ni mchezo mchafu Zitto kachukua magari mawili kutoka Mkono kosa,lakini hajajumlishwa kwenye yale makosa 11.
Mbowe kapewa pesa na Mkono hii haionekani analalamika kupewa hela na CCM haina shida inategemea umepewa za nini,halafu hao wanaokupa ndio mafisadi wakubwa.
Dah! yaani watu wanamuona Mbowe na Slaa kama malaika inasikitisha sana kwa kizazi hichi kuaminishwa hivi.
 
Zito anza mbele;kufa kiume...a cha kutapatapa..,sikio halizid kichwa.!
 
mkuu nakusoma taratibu lakini siasa ni mchezo mchafu Zitto kachukua magari mawili kutoka Mkono kosa,lakini hajajumlishwa kwenye yale makosa 11.
Mbowe kapewa pesa na Mkono hii haionekani analalamika kupewa hela na CCM haina shida inategemea umepewa za nini,halafu hao wanaokupa ndio mafisadi wakubwa.
Dah! yaani watu wanamuona Mbowe na Slaa kama malaika inasikitisha sana kwa kizazi hichi kuaminishwa hivi.

Ukifatilia maelezo ya Mkono na ya ZZK yanapishana sn! Kiasi huwezi kujua nani ni mkweli ZZK au Mkono?
Na kutokana na kupishana Kwao huko tuhuma dhidi ya Mbowe zinakua hazina nguvu! Na majibu ya Mbowe aliyotoa juu tuhuma za ZZK yanakua na nguvu!
 
do!kuna watu bado wana mahaba na mbowe pamoja na uchafu huo wa waziwaz!!!!!!!!!!!
 
Kiranga
I love this piece of writing that you depicted as per quote below; Going with this regard, now you could easily see what is all about the phenomenon "nidhamu".

"Huku si kukosea tu, useme nilikuwa sijui mlango wa mbele uko wapi nimeingilia mlango wa uani kwa bahati mbaya. This seems to be a deliberate scam with some intricate planning to protect personal interests, how would you let them off the hook that easily if the allegations carry weight?"
 
Umesahau Mabere Marando ni wakili wa baadhi ya hao mafisadi....?

Mabere Nyaucho Marando tunamjua siku nyingi yeye mzee wa danadana, tena kashajionea zogo CHADEMA karudisha kadi asije kuibuliwa madili yake naye bureee.
 
Back
Top Bottom