Zitto akiwa mwenyekiti; naahidi kuipa CHADEMA kura zangu zote!

Hammy-D anajitahidi sana kuwachokonoa CHADEMA wakati ilikuwa muhimu kutoa ushari mzuri kwa chama chake ambacho kuna kila ushahidi kuwa maji yapo shingoni as we approach to 2015
 
Mkishashiba ubwabwa wa kwenye vikao basi mnatafuta pakupunguzia shibe, unakura ngapi?
 
CHADEMA (nikiwa na maana ya wanachama) kama itajivika ujasiri na kukataa hali ya kuendeshwa na kikundi cha watu wachache na ikathubutu kumpa ridhaa ndugu Zitto nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, binafsi nitatoa kura zangu kuanzia ya urais, ubunge mpaka udiwani kwa CHADEMA bila kujali ni nani aliye simamishwa kugombea nafasi hizo (soma aya ya kwanza).

ANGALIZO: USHABIKI WA ITIKADI ZA KISIASA NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA NCHI.

Duh!
ndivyo manvyopiga kura huko MACCM, wenyewe mnaita MAFIGA MATATU hata kama mbunge ni wakusinzia kama LUKUVI basi nyie mnapiga tu.
 
Hammy-D nakushauri uelekeze nguvu zako kumshawishi bwana Zuberi Zitto ahamie CCM ili mumchague kuwa m/kiti huko ili ikinyooshe chama chenu kipenzi. Achana na CDM wajifanyie mambo yao wenyewe.
 
ha ha ha ha ha.. mkuu HAMMY-D umenichekesha mno... yaani wewe.. uache buk7 uipe kura CHADEMA? By tha way naona umeamua kujitekenya.....!
 
Huna issue wewe ni yule yule tunakumbana naye humu ndani. Huwazi kitu kingine zaidi ya Chadema na viongozi wake. Huyo Zito mchukue kwako kampongeze. Halafu huo mkataba wa kulipwa buku mbili au tatu hujabadilisha tu. Ungepata mkataba wenye pesa nzuri ungeacha kuwa kituko humu jf.
 
Hivi ilikuwaje mpaka Zitto akawekewa kizuizi ili asigombee uenyekiti, nikumbushe ni kikao gani kilifanyika kumkataa Zitto asiwe mwenyekiti wa CHADEMA!

Hakuwekewa pingamizi, pole sana na habari za vijiweni. Zitto alishauriwa kutogombea nafasi hiyo kwa kipindi kile. Na ndio maana umeona mafanikio yaliyofikiwa ndani ya chadema tangu iasisiwe. We ulitaka awe mwenyekiti alafu akawafanyie kampeni wabunge wa NCCR kule kigoma??

Pale unapotega CDM wameshapita mda mrefu. Ni sawasawa na Yanga kuwapa ushauri Simba kabla ya mechi kati ya Yanga Vs Simba.
 
HAMY-D ni janga la karne; wewe ndo unachagua Mwenyekiti wa CDM??? wakati unafanyakazi na kulishwa na CCM??? kweli unadhani wewe ni mjanja kuliko vichwa vya CDM? fikiri kwanza maana tisa ni karibu na kumi sio kumi yenyewe.
 
Ndugu Hammy-D nimekusoma lakini labda ningependa kuwaambia washabiki wa Zitto Kabwe nikiwemo mimi binafsi.Ni kweli Zitto ni Kijana mwenye uwezo wa kujenga hoja na si yeye tu wapo vijana wengi tu wenye uwezo wa kujenga hoja CDM,mfano Mnyika,Mdee,Msigwa n.k.Lakini kwa mazingira ya siasa ya nchi yetu ilivyo chini ya CCM ni vigumu saana kubadilisha mfumo wa utawala nchini bila ya kuwa na kiongozi mwenye uelewa mpana wa namna CCM kinaendesha siasa tangu nchi yetu ipate uhuru mpaka sasa.Tunahitaji mtu atakaye bomoa system ya utawala wa CCM uliopo na kwa ufahamu wangu mimi ni kwamba huwezi kubomoa system ambayo huifahamu kwa kina jinsi inavyofanya kazi,wa mukitadha huu basi tunahitaji stuational leader ambaye ataweza kuiondoa nchi hapa ilipo,nionavyo mimi Dr.Slaa anauelewa vizuri mfumo wa uongozi wa CCM kiinchi kwa sababu moja tu ya msingi kwamba alikuwemo ndani ya CCM na amekuzwa kisiasa ndani ya CCM.Je,Zitto Kabwe amewahi kushiriki siasa za ndani ya CCM?.Najua jibu ni hapana,kama hapana ataweza vipi kubomoa mfumo wa utawala wa CCM na kuweka mfumo mpya kama hajui undani wa mfumo wa CCM unavyofanya kazi?Je,si kwamba tutakuwa tumebadilisha Rais lakini haelewi namna ya kubomoa mfumo kandamizi wa CCM uliopo?Kwa iyo mimi namshauri kaka yangu Zitto kama ana ndoto za kugombea urais ampishe Dr.Slaa ili aje kubadili mfumo kwa sababu anaelewa deeply kuliko Zitto ambaye amekulia CDM,sina maana ya kwamba hana uwezo wa kuongoza laasha.Naomba tu washabiki wa Zitto tujiulize kwanini Dr.Slaa anaogopwa sana na CCM kuliko mtu yoyote CDM?we angalia tu ata post za wanaCCM ndani ndani ya JF wanamtaja sana Dr.Slaa,kwanini,ni kwa sababu he is a threat to CCM.Ndugu wanaCDM msifanye makosa katika hili la urais.
 
Mkuu, nina ushawishi kwenye jamii, hivyo sio tu mimi ambae nitapigania CHADEMA ishinde (endapo Zitto akiwa mwenyekiti), bali hata vijana na wazee watajumuika na mimi kuhakikisha hilo linafanikiwa.

Au wewe ndiyo mwanamziki mwenyewe, unamtetea afisa habari wenu shusha mistari basi humu uanze kutushawishi
 
WanaJF!

Binafsi nina amini katika 'uongozi' na sio hali ya taasisi, hii ni kwa kumaanisha kuwa endapo akipatikana kiongozi bora, basi hata taasisi iwe hoi namna gani itanyooka tu na kuwa yenye tija na yenye manufaa makubwa kwa umma.

Nina yasema haya kwa kutambua kuwa hivi karibuni una tarajiwa kufanyika uchaguzi wa ndani ya CHADEMA ambao umekuwa ukifanyika kwa kila baada ya miaka mitano, hivyo mimi kama mwananchi mpenda amani, haki na usawa, nimeona nitoe yaliyo moyoni kuhusu uchaguzi huo.

Zitto ni kijana ambae amehusika kwa kiasi kikubwa katika haya mabadiliko tunayo yaona hivi sasa kwa CHADEMA na taifa kwa ujumla wake, ni kijana ambae amejitoa kuhakikisha haki ina tolewa, usawa una kuwepo na sheria zinafuatwa, na hayo amekuwa akihakikisha yanafanywa na kuonekana kufanyika.

Zitto ndiye amekuwa tanuru la vuguvugu lenye kutoa hamasa na ujasili kwa vijana kuamka na kuhoji juu ya mambo mbalimbali yanayogusa mstakabali wa taifa letu, kwani itakumbukwa vijana wengi walijiunga na CHADEMA kwa kuvutiwa na ushawishi wa Zitto, uwezo wa kujenga hoja na uzalendo wake.

Aidha, itakumbukwa kuwa Zitto ndiye aliye ifyeka njia na kuwaandalia mazingira ya kuaminiwa na wananchi hawa wabunge wapya wa CHADEMA, kwani ni Zitto ndiye aliyekuwa akiibua mambo mbalimbali ya kifisadi serikalini, hii ilijenga imani kuwa ya wananchi kwa kijana huyu na kupelekea CHADEMA kujulikana nchini.

CHADEMA (nikiwa na maana ya wanachama) kama itajivika ujasiri na kukataa hali ya kuendeshwa na kikundi cha watu wachache na ikathubutu kumpa ridhaa ndugu Zitto nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, binafsi nitatoa kura zangu kuanzia ya urais, ubunge mpaka udiwani kwa CHADEMA bila kujali ni nani aliye simamishwa kugombea nafasi hizo (soma aya ya kwanza).

ANGALIZO: USHABIKI WA ITIKADI ZA KISIASA NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA NCHI.

Naanza kwa kumnukuu Mwalimu JK Nyerere; "Wapo watu ambao wakishindwa kujipambanua kwa hoja zenye mashiko mbele ya wananchi,watu hao watatafuta uhalali kwa kwa hoja za UDINI,UKABILA au UCHAMA".

Mwaka 1995 to 2005 Mgombea uraisi alikua Mh. mkapa (christian),kipindi hicho haswa mwaka 2000 CUF ndiyo ilikua mpinzani mkuu. Campaign team ya CCM ilijitoa kwenye sera zake amabazo nyingi zilishindwa term ya kwanza,ikaona njia pekee ni kuanza campaign za UDINI. Ndipo ukaanza kuenezwa kuwa CUF ni cha waislamu wenye mlengo wa msimamo mkali na ni magaidi. Jamii ikameza propaganda hiyo na hata IGP Mahita akatunga uongo wa kukamata "mapanga" kuwa yameingizwa na CUF (sijui kesi ilifia wapi). Cuf ikapoteza umaarufu,ikaibuka CHADEMA amabayo ikasimamisha Christian Vs Muslim, Campaign team ya CCM ikageuka na sera ya "chama cha wakatoriki". Ikatumika BAKWATA kufanya propaganda,wakaja watabiri wa nyota ( Shekh Yahaya) kuwa atakae mpinga JK atakufa. CCM ikashinda kwa mbinu zile zile za enzi za Mkapa.

Akili ya udini ikamea hadi kwa mashabiki na wapenzi wa CCM,matokeo yake ndiyo tunao watu aina ya akina HAMY-D katika jukwaa muhimu kama hili. Uenyekiti ni nafasi ambayo ina vigezo vyake kwa mujibu wa sheria na kanuni za chama husika. Kwa jinsi post ilivyo,tatizo kwa HAMY-D siyo Mbowe kuwa Mwenyekiti ila "MKRISTO" kuwa mwenyekiti. Aliyofikisha CHADEMA hapa ilipo siyo ZITTO,ila ni "KANSA YA UONGOZI" ndani ya CCM na SERIKALI yake ndiyo vimeifanya CHADEMA kuwa hapa kilipo. Watu wakiyakosa maendeleo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Wananchi wamepoteza matumaini kwa chama na serikali,hawana chaguo lingine zaidi ya kugeukia kule ambako wanaona matumaini yapo. CCM imekosa viongozi "wawazi na shupavu". Mwalimu wakati akihutubia pale DODOMA katika mkutano wa NEC taifa alisema hivi ; "Mtupatie mgombea uraisi ambaye anajua kwamba anaenda kuwaongoza watanzani masikini ambao matumaini yao yapo kwake,anaenda kuwaongoza wananchi ambao hawana taifa lingine lolote isipokuwa tanzania yao tu". Ila leo pesa ndiyo inachagua mtu ndani ya CCM.

Sipingi uwezo wa Zitto,ila sipingi pia taratibu za CHADEMA za kumpata mwenyekiti. Zitto ana fursa ya kuchagua,kubaki kupambana ndani ya chama, au kwenda amabako fursa ya kuwa mwenyekiti iko wazi. Hiyo ndiyo demokrasia ya kiuamuzi.
 
No.... no... no.... tena NO!!!! kifo cha CDM kitaanza kwa kumpa Zitto Kiti kikuu!!!
 
Hammy d umekosea ila ni sawa kwa mtazamo wako! Unaposea zitto akiwa mwenyekit utatoa kura yako kwa cdm kuanzia rais hadi diwan bila kujali nani kasimamishwa,hapo umenishangaza yan hata kama ni vilaza kisa zito kawa mwenyekit kura zitakuja cdm,pole sana, halafu zito akiwa mwenyekiti ina maana unachokiamin kuhusu ccm kitakuwa hakina maana kwako? Lazima kuwe na kiulizo hapo! Binafsi ni mwanachadema ila si kila mgombea namuunga mkono,lazima tuwe wakwel,kuhusu uchaguz wa cdm katiba ya chama na wanachama ndio watakaoamua!
 
WanaJF!

Binafsi nina amini katika 'uongozi' na sio hali ya taasisi, hii ni kwa kumaanisha kuwa endapo akipatikana kiongozi bora, basi hata taasisi iwe hoi namna gani itanyooka tu na kuwa yenye tija na yenye manufaa makubwa kwa umma.

Nina yasema haya kwa kutambua kuwa hivi karibuni una tarajiwa kufanyika uchaguzi wa ndani ya CHADEMA ambao umekuwa ukifanyika kwa kila baada ya miaka mitano, hivyo mimi kama mwananchi mpenda amani, haki na usawa, nimeona nitoe yaliyo moyoni kuhusu uchaguzi huo.

Zitto ni kijana ambae amehusika kwa kiasi kikubwa katika haya mabadiliko tunayo yaona hivi sasa kwa CHADEMA na taifa kwa ujumla wake, ni kijana ambae amejitoa kuhakikisha haki ina tolewa, usawa una kuwepo na sheria zinafuatwa, na hayo amekuwa akihakikisha yanafanywa na kuonekana kufanyika.

Zitto ndiye amekuwa tanuru la vuguvugu lenye kutoa hamasa na ujasili kwa vijana kuamka na kuhoji juu ya mambo mbalimbali yanayogusa mstakabali wa taifa letu, kwani itakumbukwa vijana wengi walijiunga na CHADEMA kwa kuvutiwa na ushawishi wa Zitto, uwezo wa kujenga hoja na uzalendo wake.

Aidha, itakumbukwa kuwa Zitto ndiye aliye ifyeka njia na kuwaandalia mazingira ya kuaminiwa na wananchi hawa wabunge wapya wa CHADEMA, kwani ni Zitto ndiye aliyekuwa akiibua mambo mbalimbali ya kifisadi serikalini, hii ilijenga imani kuwa ya wananchi kwa kijana huyu na kupelekea CHADEMA kujulikana nchini.

CHADEMA (nikiwa na maana ya wanachama) kama itajivika ujasiri na kukataa hali ya kuendeshwa na kikundi cha watu wachache na ikathubutu kumpa ridhaa ndugu Zitto nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, binafsi nitatoa kura zangu kuanzia ya urais, ubunge mpaka udiwani kwa CHADEMA bila kujali ni nani aliye simamishwa kugombea nafasi hizo (soma aya ya kwanza).

ANGALIZO: USHABIKI WA ITIKADI ZA KISIASA NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA NCHI.

Tumefika hapa kwa sababu ya watu kama ninyi.Watu ambao kazi yenu ni kuchagua WATU badala ya SERA.Nilitegemea ungesema mtu yoyote atakayetoka CDM anachagulika kwa sababu ya SERA nzuri.Lakini kwa kuwa wewe ni gamba basi kazi yako ni kuonyesha unampinga mtu mmoja tu,Dr Slaa a.k.a.kiboko yenu!
 
Last edited by a moderator:
Hivi ilikuwaje mpaka Zitto akawekewa kizuizi ili asigombee uenyekiti, nikumbushe ni kikao gani kilifanyika kumkataa Zitto asiwe mwenyekiti wa CHADEMA!
psc unahangaika sana ok uenyekiti na kura wapi na wapi?
 
WanaJF!

Binafsi nina amini katika 'uongozi' na sio hali ya taasisi, hii ni kwa kumaanisha kuwa endapo akipatikana kiongozi bora, basi hata taasisi iwe hoi namna gani itanyooka tu na kuwa yenye tija na yenye manufaa makubwa kwa umma.

Nina yasema haya kwa kutambua kuwa hivi karibuni una tarajiwa kufanyika uchaguzi wa ndani ya CHADEMA ambao umekuwa ukifanyika kwa kila baada ya miaka mitano, hivyo mimi kama mwananchi mpenda amani, haki na usawa, nimeona nitoe yaliyo moyoni kuhusu uchaguzi huo.

Zitto ni kijana ambae amehusika kwa kiasi kikubwa katika haya mabadiliko tunayo yaona hivi sasa kwa CHADEMA na taifa kwa ujumla wake, ni kijana ambae amejitoa kuhakikisha haki ina tolewa, usawa una kuwepo na sheria zinafuatwa, na hayo amekuwa akihakikisha yanafanywa na kuonekana kufanyika.

Zitto ndiye amekuwa tanuru la vuguvugu lenye kutoa hamasa na ujasili kwa vijana kuamka na kuhoji juu ya mambo mbalimbali yanayogusa mstakabali wa taifa letu, kwani itakumbukwa vijana wengi walijiunga na CHADEMA kwa kuvutiwa na ushawishi wa Zitto, uwezo wa kujenga hoja na uzalendo wake.

Aidha, itakumbukwa kuwa Zitto ndiye aliye ifyeka njia na kuwaandalia mazingira ya kuaminiwa na wananchi hawa wabunge wapya wa CHADEMA, kwani ni Zitto ndiye aliyekuwa akiibua mambo mbalimbali ya kifisadi serikalini, hii ilijenga imani kuwa ya wananchi kwa kijana huyu na kupelekea CHADEMA kujulikana nchini.

CHADEMA (nikiwa na maana ya wanachama) kama itajivika ujasiri na kukataa hali ya kuendeshwa na kikundi cha watu wachache na ikathubutu kumpa ridhaa ndugu Zitto nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, binafsi nitatoa kura zangu kuanzia ya urais, ubunge mpaka udiwani kwa CHADEMA bila kujali ni nani aliye simamishwa kugombea nafasi hizo (soma aya ya kwanza).

ANGALIZO: USHABIKI WA ITIKADI ZA KISIASA NI KIKWAZO KWA MAENDELEO YA NCHI.
Hata angekuwa kiongozi mzuri namna gani, akishapendekezwa na kushabikiwa na wapinzani wako, fikiri mara mbili zaidi! Mtu kama HAMMY-D kupendekeza kiongozi chadema! Duu!
 
:bored::bored:Hoja imekaa kinafiki, kwanini Zitto? kura yako ni moja na pengine usipige kabisa hivyo hatutaki kujadili mambo ya kibinafsi. Bwana mdogo Tanzania kwanza Zitto baadaye.
 
Back
Top Bottom