Zitto akiwa mwenyekiti; naahidi kuipa CHADEMA kura zangu zote!

Zitto akiwa mwenyekiti; naahidi kuipa CHADEMA kura zangu zote!

Jason Bourne akitiririka......!

"......................Kwakushirikiana na mashirika ya kijasusi ya CIA-USA, M1-6-UK, RAW-India, DGSE-Ufaransa, FSB Urusi, ISI Pakistan, na MSS-China, ambayo yamekuwa yakifuatilia nyendo za fedha haramu hasa za kighaidi dunia, tumefanikiwa kutambua Watanzania, Wakenya, Waafrika kusini, Waganda na Wakongo wengi matajiri walioficha fedha uswisi.
Hapa nitawaorodhesha Watanzania tu;
Orodha ni ndefu ila hapa ni wale walioficha zaidi ya USD $3.5 mmilion kila moja. Wamo wanasiasa pamoja na wafanyabiashara kadhaa maarufu. Imebainikwa kwamba fedha nyingi za wanasiasa zimewekwa na makampuni ya nje yenye shughuli Tanzania. Wamo hata Makatibu Wakuu Wizarani na wakurugenzi ila hawajafikia USD3.5million ndio maana majina yao hayamo.
Orodha kamili ni:
Jakaya M. Kikwete, January Makamba, Abdalla Kighoda, Nimrod Mkono, Nazir Karamagi, Andrew Chenge, Yusuf Makamba, Edward Lowassa, Rostam Aziz, Yusuf Manji, Ridhiwani Kikwete, Mohamed Dewji, Bernard Membe, Paul Chagonja , Zitto Kabwe, William B. Mkapa, Said Mwema, Abdulrahman Shimbo, Edward Hosea, Daudi T.S Balali, Basil Mramba,Mustapha Mkullo, Grey Mgonja, Patrick Rutabanzibwa,Tanil Somaiya, Jeetu Patel, Onoko Okesukwu mwenye asili ya Kinigeria, Awadh Mohamed (mwenye uraia wa msomalia) na Subhash Patel"

Mkuu, hili sikulijua hili (hasa hapo ulipo Bold na herufi kubwa) kumbe ndio maana alikataa kutaja majina? Aise! halafu eti kuna mtu anataka huyu ndio awe mwenyekiti wa CHADEMA, kifo cha hicho chama kitakua hapo. Kuna comment 1 kwenye uzi 1 humu ulionesha kua, gari la Zitto liliwahi kupata hitilafu maeneo ya Igunga, Igunga pale kuna diwani wa CHADEMA, CHEDEMA wanao mafundi wao wa magari (rejea kilicho mtokea Sugu, aliwapigia simu mafundi wa CDM na walikuja ku-attend gari lake) kitu cha ajabu sana, Zitto alifanya mawasiliano na Rostam Aziz, hivi hili halishangazi kweli?
 
You are a total disappointment HAMY-D; kura yako moja kama ni ngumu namna hivyo ibakize huko huko ccm hata ushindi wa chama kingine usifikirie ya kuwa hawatakuwa watakaopuigia ccm ukiwepo; it is just baki huko
 
Jamani, huyu mleta mada siyo muislaam, ni mkristu alafu siyo mfia dini I mean siyo mdini hata kidogo. Ila kwa wale ambao hamumfahamu...huyu jamaa ni mfuasi wa mzee Lowassa. Na wanakundi lao ambalo ndani yake kuna wanasiasa, waandishi wa habari kama yeye na baadhi ya wafanyabiashara. So anachokifanya hapa ni kutaka kuwagombanisha viongozi na wanachama wa Chadema kwa maslahi ya mzee Lowassa.

Huyu mtu yuko hapa kikazi kwa maslahi ya mzee Lowassa. Hutaki Unaacha.

Ahaaa, kumbe huyu ni mwandishi wa habari? nimeanza kumuhisi, huyu sio yule aliyekua akiandikaga makala za Mchokonozi huyu? Kijana toka mkoa wa Mwanza, aliwahi kufanyia kazi gazeti la Tanzania Daima na sasa yupo kwenye ile kampuni ambayo low watch anahisa? O. K! I think so!
 
Kama kura yako Hamy-D inaweza kutukosesha ushindi basi na iwe hivyo lakini hata siku moja ccm haiwezi kutuchagulia kiongozi wa Chadema. Na hata mara moja hujawahi kuwa na nia njema na Chadema na hata hiki unachokifanya hapa unakijua kuwa unatafuta kupandikiza chokochoko miongoni mwa wanchadema kwakuwa unatambua nguvu ya Chadema kwa sasahivi, kwahiyo mawazo kama haya u najaribu kuyaleta ili kama itafanikiwa kuleta migawanyiko kwa wanachadema basi nyie ccm mpate kupumua.

Ukweli ni kwamba kiongozi wa Chadema atakayechaguliwa na wanachama wenyewe ndiye atakuwa chaguo lao na wala hakuna cha vikundi wala kikundi cha kuweza kuamua kuwa nani awe kiongozi na nani asiwe.

Mwita Maranya,

Precisely my point.Typical case ya jaribio la shetani ! ! !
 
Last edited by a moderator:
Zitto kupewa uenyekiti labla akubali kubatitwa kwanza.
Kweli kabisa, lazima abatizwe kama mtatiro alivyosilimishwa kwanza kisha akapewa unaibu katibu mkuu. Na mkuu wa magamba alipobatizwa na kuambiwa yeye CHAGUO MUNGU.
 
Ahaaa, kumbe huyu ni mwandishi wa habari? nimeanza kumuhisi, huyu sio yule aliyekua akiandikaga makala za Mchokonozi huyu? Kijana toka mkoa wa Mwanza, aliwahi kufanyia kazi gazeti la Tanzania Daima na sasa yupo kwenye ile kampuni ambayo low watch anahisa? O. K! I think so!
Ni timu ya watu wengi. Fuatilia posti zao hata masalia wamo. Id moja watu kibao. Wanapokezana. Iko hewani almost masaa 24. Ukiikosa ID hii hewani masaa ma3 nenda katambike.
 
Ahaaa, kumbe huyu ni mwandishi wa habari? nimeanza kumuhisi, huyu sio yule aliyekua akiandikaga makala za Mchokonozi huyu? Kijana toka mkoa wa Mwanza, aliwahi kufanyia kazi gazeti la Tanzania Daima na sasa yupo kwenye ile kampuni ambayo low watch anahisa? O. K! I think so!

Huyo tunamjua mkuu na wanaomtumia ndiyo watakaomtoa roho kwa sababu ya siasa
 
Endelea kumsoma between the line kwenye kila thread zake utamjua tu na utatambua why jamaa habanduki hapa jukwaani. Chezea pesa za mamvi wewe
 
wanajf!

Binafsi nina amini katika 'uongozi' na sio hali ya taasisi, hii ni kwa kumaanisha kuwa endapo akipatikana kiongozi bora, basi hata taasisi iwe hoi namna gani itanyooka tu na kuwa yenye tija na yenye manufaa makubwa kwa umma.

Nina yasema haya kwa kutambua kuwa hivi karibuni una tarajiwa kufanyika uchaguzi wa ndani ya chadema ambao umekuwa ukifanyika kwa kila baada ya miaka mitano, hivyo mimi kama mwananchi mpenda amani, haki na usawa, nimeona nitoe yaliyo moyoni kuhusu uchaguzi huo.

zitto ni kijana ambae amehusika kwa kiasi kikubwa katika haya mabadiliko tunayo yaona hivi sasa kwa chadema na taifa kwa ujumla wake, ni kijana ambae amejitoa kuhakikisha haki ina tolewa, usawa una kuwepo na sheria zinafuatwa, na hayo amekuwa akihakikisha yanafanywa na kuonekana kufanyika.

zitto ndiye amekuwa tanuru la vuguvugu lenye kutoa hamasa na ujasili kwa vijana kuamka na kuhoji juu ya mambo mbalimbali yanayogusa mstakabali wa taifa letu, kwani itakumbukwa vijana wengi walijiunga na chadema kwa kuvutiwa na ushawishi wa zitto, uwezo wa kujenga hoja na uzalendo wake.

Aidha, itakumbukwa kuwa zitto ndiye aliye ifyeka njia na kuwaandalia mazingira ya kuaminiwa na wananchi hawa wabunge wapya wa chadema, kwani ni zitto ndiye aliyekuwa akiibua mambo mbalimbali ya kifisadi serikalini, hii ilijenga imani kuwa ya wananchi kwa kijana huyu na kupelekea chadema kujulikana nchini.

Chadema (nikiwa na maana ya wanachama) kama itajivika ujasiri na kukataa hali ya kuendeshwa na kikundi cha watu wachache na ikathubutu kumpa ridhaa ndugu zitto nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, binafsi nitatoa kura zangu kuanzia ya urais, ubunge mpaka udiwani kwa chadema bila kujali ni nani aliye simamishwa kugombea nafasi hizo (soma aya ya kwanza).

Angalizo: Ushabiki wa itikadi za kisiasa ni kikwazo kwa maendeleo ya nchi.

''bahati haimfanyi mwendawazimu kuwa na busara''
 
mbona ulisema baada ya mgombea binafsi kupitishwa hakutakua na kitu kinachoitwa CHADEMA. wewe ndugu vipi mbona hauleleweki mara hii umeshasahau ulichoongea mda si mrefu kweli ukiwa muongo uwe na kumbukumbu dada.

Hivi unajua maana ya kifo cha CHADEMA?, au uelewa wako haustaili kuwepo humu?, hadi hilo nalo unataka ufafanuzi?
 
Usimpe tu kura pekee kwani haitoshi. Mpe "MNDUKU" kabisa ili tuamini kuwa Unamuadmaya!!
 
Hammy-D anajitahidi sana kuwachokonoa CHADEMA wakati ilikuwa muhimu kutoa ushari mzuri kwa chama chake ambacho kuna kila ushahidi kuwa maji yapo shingoni as we approach to 2015

CCM haikuwahi kuwa kwenye hiyo hali mkuu, wenda ingekuwa kama vijana hawa aina ya Zitto wangesimama kupambana kwenye nafasi ya urais, ila kwa watu wachovu kama Dr Slaa CCM inajipatia usingizi mwanana.
 
Duh!
ndivyo manvyopiga kura huko MACCM, wenyewe mnaita MAFIGA MATATU hata kama mbunge ni wakusinzia kama LUKUVI basi nyie mnapiga tu.

Mwenyekiti akiwa "jembe" basi taasisi hata ikiwa hoi vipi itanyooka tu. Watu wakionyesha dalili ya uzembe wa aina yoyote mbele ya mwenyekiti mwenye sifa tajwa, basi atawajibishwa ipasavyo.
 
Hammy-D nakushauri uelekeze nguvu zako kumshawishi bwana Zuberi Zitto ahamie CCM ili mumchague kuwa m/kiti huko ili ikinyooshe chama chenu kipenzi. Achana na CDM wajifanyie mambo yao wenyewe.

Demokrasia haitulei hivyo mkuu, mimi kama mwananchi mpenda amani, haki na usawa nina haki ya kutoa maoni yangu kwa chama chochote regarless mimi ni mwananchama au sio, ila nisivunje sheria tu katika kuyatoa maoni hayo. Hivyo haya ndio maoni yangu kwa CDM.
 
Zito kunasiku atawaumbua watanzania wanamjua kazi yake kunasiku ataibukia kokote kule na watu watamfuata.

Mkuu, eti hilo nalo linahitaji tuwe na DVR ili kuligundua?, mbona liko wazi sana na kwa sasa Mbowe na Dr Slaa wamelihalalisha kwa wanachama wengine kumtenga Zitto na kutompa ushirikiano, ila kwa vijana walio wengi CHADEMA hilo hawako tayari kulifanya.

Mkuu,Ngoja mgombea binafsi ipitishwe halafu uone kama kutakuwa na kitu kinaitwa CHADEMA baada ya hapo.

Back
Top Bottom