Zitto anasema Magufuli aliharibu uchumi kwa miaka 5, msikilize hapa akiwa na Magufuli akimsifia hadharani

Hiyo ni kweli jamaa aliiharibu nchi
 
Dini yake inamruhusu!
 
Kwa kimombo cha kwetu ukichekeshwa sana mpaka ukagalagala chini huwa tunasema "..iseko isi nunu..."
 
Na hii imekaaje?
 
Nadhani ndio tatizo la kushindwa kutofautisha kati ya kukosoa na chuki, watu wengi wamejijaza chuki na mwenye ni nadra kuona anakusifia hata ukifanya jambo zuri yeye hutaka kila siku akueleze kwa ubaya tu maana anakuchukia.
 
Mkitaka kuwafuatilia Wanasiasa watawatesa sana....wao wenyewe wanajua sifa kuu ya kuwa Mwanasiasa ni kuwa muongo.
 
Alete na Ile ya.... Mbowe wewe ni WA kipekee ...Mbowe Safi,Mbowe Oyee
 
Nafasi za ubunge wa kuteuliwa zimekwisha . Atafute mengine
 
Mwanasiasa yoyote bila unafki mambo yao hayaendi

Ova
 
Katika uhalisia maraisi wa Africa
wana nguvu kutokana na katiba na utamaduni wa kuwafanya miungu watu sio rahisi kumkosoa Raisi alie madarakani
utarisk maisha yako au utatengenezewa matatizo majubwa sana na wapambe wake na vyombe vya dola na ndio maana ukosoaji unajitokea wakati wakitoka madarakani Zitto yuko sahihi na wakosoaji wengine wanaojitokeza sasa
 
Wew ni mpuuzi na zito wako hujui chochote

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Zitto Zuttu Zuzzu.
 

 
Zito ni mnafiki tu kama wanafiki wengine nakumbuka ziara ya Magufuli kigoma alimsifia sana
 
EeenHeee, mkuu 'Hakimu Mfawidhi', wewe unatumia tukio hilo la kumsifia Magufuli kumhukumu Zitto? Hapana.

Pamoja na kukubaliana na wewe moja kwa moja juu ya tabia za Zitto, lakini hilo tukio huwezi kulifanya ndilo liwe kipimo cha kuaminika kwa Zitto. Kwenye hadhara kama hiyo ni kawaida sana kufunika yale yasiyosemwa mbele za mhusika na badala yake kunakshia yale mazuri.

Ninakubaliana nawe pia kwamba tabia ya mtu ni ile 'consistency' anayokuwa nayo katika misimamo yake. Hapa ndipo sehemu nzuri zaidi ya kum'categorize' Zitto. Ukirudi nyuma katika historia yake ya kufanya siasa, kuna matukio mengi sana yanayombainisha kuwa siyo mtu wa kutegemewa sana katika uaminifu.
Sifa kuu aliyonayo Zitto ni uwezo wa kueleza na kufafanua mambo, hasa yanayohusiana na eneo lake la elimu. Laiti kama angekuwa na tahadhari ya kuchunga uaminifu wake, sifa hii ingemfikisha mbali zaidi kwenye nyanja ya siasa za Tanzania.

Lakini sasa imeanza kuonekana pia kwamba ni mtu mwenye tamaa ya kuzoa kwa manufaa yake au kundi analohusika nalo zaidi kuliko manufaa ya wananchi wa Tanzania kwa ujumla. Hapo awali alijitambulisha kuwa karibu zaidi na filosokia ya Mwalimu, lakini siku hizi anaonekana kuwa kwenye kambi ya wapigaji walioko kwenye kambi ya Kikwete!

Sasa Zitto tumuweke wapi? Maslahi ya taifa hili, au maslahi ya makundi yanayofaidika na ulanguzi wa mali za taifa hili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…