KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Mkuu 'Kiranga', leo nimekusoma tofauti sana na ninavyokusoma siku zote hapa JF.Ndiyo maana mimi nashauri kuungana kufanyike kwa sababu zenye mizizi mirefu, si sababu shallow za kutaka kuitoa CCM Ikulu tu.
Hivi kuna sababu gani kubwa zaidi kuliko ya kuiondoa CCM madarakani wakati huu?
CCM ambayo imeng'ang'ania kabisa, haitaki kuondoka madarakani kwa kutumia njia zote, hata za kukandamiza wanaotafuta njia za kuwaondoa kwa taratibu zilizopo!
Binafsi siyo muumini wa vyama vya upinzani kuungana, kwa sababu najuwa hilo haliwezekani kwa sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuungana huko kutumiwa kuwadhoofisha zaidi. Lakini, kama wangeweza kuungana kwa nia tu ya kuiondoa CCM madarakani, hilo lingekuwa lengo muhimu zaidi kuliko hizo sera na mambo mengine ya kuendesha serikali baada ya kuondoka kwa CCM.
In my view, that's how bad our political situation has become.