Mbona hili ni rahisi sana.
Lowasa kuhamia CHADEMA, ajenda yake ilikuwa ni moja tu - Kutafuta urais, hapakuwa na sababu nyingine yoyote iliyomfanya ahamie CHADEMA; kwa hiyo baada ya kuukosa urais, hapakuwa na sababu ya kumfanya aendelee kubaki CHADEMA.
Alipopewa misukosuko toka huko alikokukimbia akaona heri ajisalimishe.
Hapo jambo gumu lipo wapi hadi watu kuumiza vichwa vyao juu yake?
CHADEMA, na wao walikuwa na ajenda yao, matamanio ya kushika madaraka.
Walidhani mwonekano aliokuwa nao Lowassa baada ya kukatwa ungeweza kukidhi matamanio yao hayo.
Ndani ya chama chao kwa wakati huo hawakuwa na tegemeo lolote la mtu ambaye angepambana kuwaletea ushindi.
Chama chochote cha siasa lengo ni kupata ushindi.
Ushindi ulipokosekana, wakaendelea kuwa na matumaini kuwa mgeni wao atawaletea mbinu na uzoefu aliokuwa ameujenga kwa muda mrefu akiwa CCM. Lowassa hakuonyesha dalili zozote za kuwa na uongozi wa aina hiyo. Kwa hiyo akabaki kuwa mzigo tu.
Uchaguzi wa 2015, ulikuwa uwe ushindi wa Lowassa. Yule Lowassa, Waziri Mkuu wa Kikwete angekuwepo kwenye kampeni za uchaguzi wa 2015, Magufuli asingepiga kona.
Kwa bahati mbaya, Lowassa wa enzi za Kikwete hakuwepo kuchukua ushindi ule.
Lowassa alishindwa kwa mwonekano wake aliouonyesha kwenye kampeni