Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Inawezekana pia ushindi kuwatenganisha watu.Nimemsikiliza Zitto na sababu yake/ zake kwanini suala la Membe kuhamia kwenye chama chake halitokuwa kama ilivyokuwa kwa CHADEMA na Lowassa na Sumaye na wengineo.
Sababu zake kuu ni kwamba hao waliohamia CHADEMA kipindi kile hawakujiona au hawakuonekana kuwa ni sehemu ya ‘movement’.
Pia, eti hawakujiona au kuonekana kuwa walikuwa ni sehemu ya ‘familia’ ya CHADEMA.
Muda utazungumza tu. Ila Zitto inabidi awe mwangalifu na uchaguzi wa maneno yake.
Kwenye hili nadhani Bw. Zitto anaathiriwa na kuwa ‘prisoner of the moment’.
Natumaini yeye na ACT yake watakuwa na mipango baada ya uchaguzi ujao baada ya kushindwa.
Maana ushindi huwaunganisha watu na ushindwaji hugawanyisha.
Kwa mfano, nasikia sana habari za wapinzani kutaka kuungana wawe na mgombea mmoja ili kuitoa CCM Ikulu.
Fine.
Lakini, wakiungana kwa lengo la kuitoa CCM Ikulu tu, bila ya kuwa na muungano wa zaidi kiitikadi, sera, mipango etc, ushindi ukipatukana, wataangaliana na kusema, ndiyo tumeshinda, tumemaliza kitu kilichotuunganisha. Zaidi ya hapa sisi si wamoja. Watapigana. Watatengana.
Kwa hivyo, hata ushindi unaweza kuwatenganisha watu.
Ndiyo maana mimi nashauri kuungana kufanyike kwa sababu zenye mizizi mirefu, si sababu shallow za kutaka kuitoa CCM Ikulu tu.