Zitto hafai kuaminika kwenye struggle za nchi hii, yule ni compromised Politician

Mbowe aliombewa msamaha kwa kosa gani dogo?! nani alimtuma Zitto?

Hebu punguza hizi kelele zako, yule DPP wenu sio mjinga kwa kile alichofanya.
 
Mbowe aliombewa msamaha kwa kosa gani dogo?! nani alimtuma Zitto?

Hebu punguza hizi kelele zako, yule DPP wenu sio mjinga kwa kile alichofanya.
Kuna sehemu nimekwambia Mbowe aliomba msamaha, nilichokwambia Zitto alikuwa anataka Mbowe aachiwe kama mtanzania yoyote dogo.
DPP wa nani? Yes, hakuna anayekataa kuwa ile kesi ilikuwa ya mchongo. We unajua Mbowe alipoenda ikulu alizungumza nini na raisi, hujiulizi kwanini brake ya kwanza iwe ikulu.
Ingelikuwa ni Zitto ndiye kafanya hivyo basi mngemwita msaliti.
 
Ngoja ni wa ku unfollow hata kule twita. Mnaweza kufika 1m akawauza kwa dalali wa magari
 
Siasa za upinzani ziko kwa mabeberu bhanaa, achana na hawa wanasiasa njaa kama akina zitto.........
 
🤔🤔🤔
 

Ninadhani Buthelezi kulinganisha na wetu wa zama hizi yeye alikuwa funga kazi.

Kama Mandela pamoja na yote bado hakumtupa ni maoni yangu kuwa huyu wetu ni cha mtoto.

Kwamba kabadilika au la - ndiyo msingi wa phrase hii "panapo uwezekano."

Sijamaanisha kuwa katiba mpya haipatikana bila yeye. Bali nimekuwa wazi: "umoja ni nguvu."

Pamoja naye hii ilikuwa yapatikana mwaka huu huu tu na tena bila maumivu. Maana ilikuwa kumwachia Mukandara na tume yake tu.

Kumbuka Lipumba - mwingine asiyeaminika ni huyu hapa:

Prof. Lipumba aikataa Kamati ya Prof Mukandala. Asema hakuna mjumbe hata aliyesema mchakato wa Katiba usubiri hadi mwaka 2025

Binafsi ninaipenda statement hii:

"Hakuna rafiki wala adui wa kudumu bali agenda."

I can't wait to see it applicable kwenye kupigania struggle.
 
Mkuu hata waliochukua sample ya maji ya mto Mara walichukua chupa moja tu ya maji sio mto mzima.
Hata wenye katiba mpya bado maisha yao magumu, ufisadi, Rushwa vimetamalaki na malalamiko ya wizi wa kura kama kawa mf.Kenya na SA
 
Zitto kasingiziwa kipi? vile vikao alivyokuwa anafanya enzi za JK kwa siri usiku halafu akiulizwa anadai JK ni sawa na baba yake then anakuja kutaka uenyekiti wa Chadema nani mwenye akili timamu atamuamini?
ACT tengenezeni Chama
 
Kila mwanasiasa anasaka maslahi yake
 
Umeandika ramli tupu, unaendelea kujitutumua tu.

Kwani wewe unajua Mbowe alivyoenda ikulu aliongea nini?
 
All the best.
 
Umeongea kweli.

Laiti ingekuwa ni Zitto aktoka selo directly ikulu yani ungesikia mengi.

Akifanya zitto nongwa, wanasema sijui ushirikiano na serikali zanzibar, why iwe nongwa wakat wao walishirikiana na Lowassa ili wavune mtaji wa wafuasi wake.
Tukumbushe tujue Ni lini huyu Zitto aliwahi ingia hata mahabusu achilia mbali kuhukumiwa,

maana japo kuwekwa mahabusu siyo sifa ya kisiasa tumeshuhudia hapa kwetu mpinzani halisi anaye tikisa maslahi ya ccm lazima ama aambiwe si raia, apokonywe hati ya kusafiria,au afunguliwe mashitaka tena yasiyo na dhamana.

Hapa kunaweza kuwa na "ka ukweli fulani" kwamba huenda huyu Zitto ni "mwenzao" aliyejivika joho la "mwenzetu".
 
Kipimo cha upinzani sio kuingia mahabusu, Mbowe mbona huko nyima hakuwahi kuingia walikuwa wanaingiaga wenzake tu na hamkuhoji?
Mbowe kaanza ingia akina Lissu na Slaa na Lema walipokosekana.
Lakini wenzake toka enzi za jakaya wanaingia tu.
Hivyo, narudia sio lazoma Zitto aingie mahabusu na haimaanishi hawezi kuingia ni muda ndio utaamua
 
Umeandika ramli tupu, unaendelea kujitutumua tu.

Kwani wewe unajua Mbowe alivyoenda ikulu aliongea nini?
Sasa kwanini hilo swali la kujua uwa hamlotumii linapokuja swala la zitto? Yani mnamhukumu kwa hisia na hearsay, ila likija kwa mtu wenu mtataka ushahidi.
Acheni double standards na kujiona nyinyi ndio bora
 
Kwani uongo?
 
Una hoja.

Angalia pia: Mwaka 1992, 80% ya wahojiwa wa Tume ya Jaji Nyalali walitaka tuendelee na demokrasia ya chama kimoja. Tukawapuuza na kuamua kuegemea kwenye maoni ya 20% ya wahojiwa waliotaka tuwe na mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini. Haikuwa sawa.

Basi ni vyema zaidi turekebishe uamuzi huo kwa kuchukua maoni ya 80%. Naamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetatua tatizo la msingi. Hatutakuwa tena na haja ya katiba mpya wala tume huru ya uchaguzi. Tume ya Warioba na CHADEMA watakuwa irrelevant. Problem solved.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…