Dini ni imani ya mtu binafsi haiingiliwi na ili mradi haivunji katiba. Gwajima anatumia haki yake kikatiba. Chanjo ni Hiyari. AnAyechanjwa anajitangaza amechanjwa na asiyechanjwa anajitangaza hajachanjwa sasa kwa nini mwingine alazimishe watu kuchwanjwa? Au kutochanjwa? Jibuni maswali ya Gwajjma. Acheni blah blah.... Jibuni ili ionekane amepotoka wapi... Msianike upumbavu wenu mkitaka watu wakausage wapikie uji.
Hii nchi haina dini kikatiba.
Masuala ya serikali hayajibiwi kwenye nyumba za ibada Kwa kuweka msimamo wa kidini.
Maswali ya Gwajima yameshajibiwa kitaalam na wa taalam wengi ndani na nje ya nchi.
Suala la chanjo lipo dunia nzima na hakuna atakayekwepa ni suala la muda tu na kujifariji.
Sayansi siku zote inapoletwa duniani watu wa dini wamekua wakiipinga lakini baadae wao ndio wanakua mstari wa mbele kunufaika nayo.
Oooh wazungu wanataka kutumaliza waafrika wakati kila kitu cha kisayansi kinatoka kwao. Sio kila mzungu ni mbaya.
Wenzetu hawalali ili waondoe matatizo yao yanapojitokeza. Gwajama anapinga chanjo kama nani?
Kama anachanjo yake ailete ili apinge iliyopo sio kupinga dawa kwa maneno ya mitandaoni.
Sayansi inapingwa kisayansi kwa kuingia kwenye maabara sio kama mabishano ya kisheria kahakamani.
Ndio maana hata mahakamani ushahidi wa kitaalam unatolewa na wataalam sio vinginevyo.
Gwajima anataka ajibiwi na wataalam kama nani? Rais alishakaa na wataalam akaunda mpaka tume ikampa majibu ya kitaalam sasa Gwajima anataka aunde tume yake au anataka tu kumsumbua kwa sababu Rais aliyepo hatumii mkono wa Chuma au kwa sababu Rais sio wa kabila lake au dini yake??
Acheni kuyumbisha maamuzi ya serikali.
Gajima ahubiri watu waache ulevi,uzinzi, rushwa, ufisadi,wizi wa kura,dhuluma ,uonevu ,kubambikia watu Kesi za uongo ,ulawiti,ushoga, uasherati, ushirikina ,uchawi ,kupenda pesa kupita kiasi.kuua n.k.
Hayo ndiyo Mwenyezi Mungu anayotaka yaachwe ili dunia iwe sehemu salama ya kuishi.
Watu wasipoacha dhambi bado pataibuka gonjwa lingune tena baya zaidi mana dunia inaangamia kwa sababu ya uovu na sio chanjo.
Yaani unatangazia waovu kuwa watakua salama bila kuacha uovu wao.
Haiwezekani.
Sayansi inakimbia kasi sana yale mambo ya kufanya tafiti miaka kumi yamepitwa sana na wakati.
Sasa hivi tafiti zinafanywa kwa kasi kubwa lakini pia ikimbukwe kuwa korona na magonjwa yanayofanana nayo yapo kwa kipindi kirefu hivyo tafiti zilishaanza muda mrefu kwa ajili ya magonjwa yanayoshabihiana nayo.