Zitto Kabwe amdhihaki Tundu Lissu kwa kumuita CHIBA. Aomba radhi baada ya kulalamikiwa

Zitto Kabwe amdhihaki Tundu Lissu kwa kumuita CHIBA. Aomba radhi baada ya kulalamikiwa

Suzy Elias

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2021
Posts
1,067
Reaction score
6,200
Zitto sasa amevuka mpaka na shime ndugu Tundu usimchekee tena hasa kwa hatua hiyo ya kukudhalilisha kwa kilema chako.

Hii ndiyo Tweet aliyoandika Twitter wakati akijibu hoja ya mdau

zitto.jpg

Baada ya kulalamikiwa na wadau, Zitto Kabwe aliomba msamaha na kudai kuwa hakuwa anajua maana ya neno ''CHIBA'' kama linamaanisha mlemavu, bali alijua ni maneno ya vijana tu

Nukuu
Kwa kweli sikufahamu kama jina Chiba linahusiana na ulemavu. Nilidhani ni majina ya Vijana ya kutaniana. Mama yangu mzazi alikuwa mlemavu kamwe siwezi kutweza ulemavu wa Mtu. Naomba radhi sana Kwa hili. Hakika Sio Sawa. Uzee umeingia tunapitwa na majina ya mtaani. Mniwie radhi

msamaha.JPG
 
Kiburi Cha ndugu yetu Zitto Kabwe kimekuwa kikubwa Sana
Juzi alituita tunaotaka katiba mpya hatuna ubongo na Leo kamuita Tundu Lissu Chiba akiwa na maana ya mlemavu. Yaani inaonekana Zitto alifurahia saana Lissu aliposhambuliwa kwa risasi
IMG_20220316_123045.jpg
 
Ameomba radhi! Seems alijua ni jina la utani lakini hakujua linahusishwa na ulemavu. Itakuwa ajabu hili tukitaka kulifanya topic.

Nashauri likomee hapo, kulizungumza zaidi halitamuumiza tu Zitto bali hata ndugu yetu. Mengine tuache yapite.
 
Anatakiwa ajiuzulu mara moja uongozi wa Jukwaa la Wanasiasa.

Huyu Zitto Kabwe ana dini kweli?
 
Back
Top Bottom