Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kwanza kabisa Samia kaenda kama rais, na kaalikwa na Mbowe. Katumia hela za umma kwenye shughuli ambayo ni ya kidini. Ile michango waumini walipewa fomu za kualika wachangiaji.Rais ni mtanzani kwa utanzania wake aliona ni vyema kushiriki kuchangia kanisa kwasababu hao ndio hutumika kutangaza amani, hivyo ni sehemu yake ku promote peace. Kumbuka rais hakualikwa, ilikuwa ni harambee/fund raising yeyote mwenye utashi alichangia, live cash au kwa bahasha, au ahadi.
Chanzo cha pesa siwezi kukielezea kwasababu sifahamu. Ila kwa kanisa wao wanataka pesa, sasa kuanza kuchunguza kila aka mchukuwa Silinde, wakampa ubunge na unaibu waziri wakamsingizia Mbowe mbinafsi.
Ccm wamemshindwa Mbowe na hata hili watashindwa, subiri muda ufike utaelewa naongea nini?.
Kiongozi wa secular state anapofanya siasa kutumia dini analeta matatizo zaidi ya anayotatua. Tayari kuna watu misikitini Zanzibar wiki hii wanamsema vibaya kwa kuwaopendelea Wakristo.
Kama hujui chanzo cha pesa, hilo ni tatizo kubwa. Walipa kodi wengine hatutaki pesa za kodi zitumike kwenye mambo ya dini. Dini si kazi ya serikali.
Mbowe na Samia wote wana lawama, wamevunja misingi muhimu ya Separation of Religion and State. Mbowe kwa kumualika Samia na Samia kwa kukubali. Wanaingiza siasa makanisani.
Mbowe mwenyewe anajijengea mazingira ya kuonekana kapewa rushwa. Kama kanisa kuchangiwa na Samia ni controversial, kwa nini ajiingize kwenye hiyo controversy kwa kumualika Samia? Yani hata ile favor tu kusema Tanzania kuna makanisa maelfu yanahitaji michango, Samia kaenda la Mbowe, ni scandal tayari. Political favoritism.
Kwa nini hatuoni hili?
Hebu msikilize JFK alivyokuwa anagombea urais Marekani akizungumzia suala la Swparationnif Rwligion and State halafu uangakie sisi tunavyochukulia poa mambo haya.
View: https://youtu.be/LAvHHTt2czU?si=9XltUA-Gw8NgutUI