Zitto Kabwe atoa hoja nzito juu ya uwekezaji wa DP World Tanzania

Zitto umelogwa na nani unategemea kwenye majadiliano kati TPA na DP tutatoka salama? Kwa TPA gani tuliyonayo nayo?
Haya mambo yamejificha kwenye msingi wa katiba. Hii TPA ya kuteuliwa kweli kweli kabisa ikapingane na chief Hangaya? Ngoja tuone mwishowe
 
Unadhani kauli za Mbowe Juu ya Rais Samia Suluhu na Mh Makame Mbarawa zilikuwa kauli nzuri na zakiungwana?

..sio sahihi Mzanzibari kuongoza wizara isio ya muungano.

..Kauli ya Mbowe kuhusu Prof.Mbarawa ni marudio ya malalamiko ya muda mrefu ya Watanganyika kuhusu kupokwa haki zao na Wazanzibari.
 
Mbona nishakutana na mmoja tayari, namjibu hapa. Focus kwenye mjadala, kwani JF ya Baba ako? Focus kwenye hoja ya msingi, na nashukuru unanijua, sikujui.
We nae mara mara moja moja vua koti njaa alafu ulivae tena
 
Hatutaki chochote kile kuhusu bandari na Mali zingine za tanganyika kuchezewa mkitaka vita na vifo endeleeni
 
Nimesikiliza kwa makini sana alichozungumza Zitto Kabwe juu ya hili suala la DP World.

Kwanza ningependa kumpongeza Zitto Kabwe kwa kazi nzuri sana anayoendelea kufanya, kwenye hili ametenda haki na ameonesha ukomavu wa hali juu kama kiongozi wa Chama cha Upinzani (ACT Wazalendo).

Ameweza kuondoa ukakasi kwa maneno machache sana na rahisi mno ambayo kila mtu anaweza kuelewa.

ZK anasema, kwenye jambo hili ni vyema tukatofautisha kati ya hisia na facts, ingawa hawapingi wazungumzao kwa kutumia tu hisia, kwani hisia nazo ni muhimu bali tunapaswa tuwe makini zaidi ili tuepuke upotoshaji ambao kama umejitokeza siku kadhaa nyuma.

Kwenye suala hili, ZK anasema kwamba kulikuwa na sababu za makusudi za upotoshaji, ambazo lengo lake ni kuleta hataruki (confusion) kwa jamii kwa maslahi ya kisiasa.

ZK anasema kwamba kupitia chama chake cha ACT Wazalendo, wametoa tamko linalowaeleza wananchi ni kitu gani kinakwenda kujadiliwa Bungeni. Nipongeze hatua hii kwani kwani vyama vingine mfano CHADEMA, kwenye hili kimekuwa mstari wa mbele kupotosha umma kuliko kuelimisha umma, Hongera ZK kwa hili.

ZK anaendelea, Kinachokwenda kujadiliwa Bungeni ni MoU ambayo imetoka hadharani, MoU ile, ni makubaliano kati ya serikali mbili (Dubai na Tanzania) ambapo makubaliano hayo sasa, yanatoa ruhusa ya serikali yetu kwenda kujadiliana hayo mambo yanayohusu uwekezaji wa DP World, na huko kwenye hayo majadiliano, ndipo tunapaswa tuwe makini kwa sababu ndio tutakapokuwa na masharti yote ya mkataba wa utekelezaji.

ZK kwa umakini wa hali ya juu anasema kwamba, hiki ambacho kinakwenda kujadiliwa Bungeni, "is simply the framework agreement" ambayo ina muda mahususi. ZK anasema, amesoma Kamati ya Bunge inayohusika moja kwa moja na jambo hili, na ripoti ya azimio la ambalo linakwenda kujadiliwa Bungeni inasema kwamba, "Serikali ya Tanzania itahakikisha kuwa, mamlaka ya bandari haitapokea maombi mengine kwenye maeneo ya ushirikiano yaliyoanishwa katika kiambatanisho namba 1 awamu ya kwanza mkapa hapo mazungumzo katika ya TPA na DP World yatakakuwa yamesitishwa au baada ya kupita kipindi cha miezi 12 baada ya kusainiwa kwa MoU".

Sasa basi, ili tuweze kupata mkataba wa utekezaji, ni hadi Bunge lijadili MoU na kutoa ridhaa kwa TPA kuanza majadiliano na DP World ili kuandaa mkataba wa utekelezaji (HGA), sasa kama itatokea TPA na DP World wameshindwana kwenye majadiliano ndani ya kipindi tajwa, serikali inaweza kutafuta kampuni nyingine ya kuwekeza kwenye bandari zetu.

ZK anaendelea kusema kwamba, mjadala wa Bunge juu ya MoU hii ndio muhimu zaidi, yaani ndio msingi mkuu wa HGA, kupitia hapa ndio tunaweza kujua kwamba tunaliwa au tunakula, kwahiyo ni muhimu sana Wananchi kwamba kinachokwenda kuamuliwa na Bunge, sio kuwapa DP World uendeshaji wa bandari zetu, bali kinachokwenda kuazimiwa, ni kuipa ruhusa serikali kuanza majadiliano na DP World, na kama majadiliano hayo yakishindikana, azimio lote halipo tena. Nguvu zetu,tuwekeze kwenye majadiliano ambayo yanakwenda kutupa mkataba wa utekelezaji.

Kwa ufafanuzi huu wa @zittokabwe ,kama mtu hatoelewa basi, na unaua kabisa hoja muflisi za mkataba usiokua na kikomo na mkataba wa miaka 100.
Yaani kumbe na wewe ama kwa upungufu wa akili au kulipwa mahali fulani. Tayari kinachojadiliwa kimetiwa saini na rais wa JMT na kama bunge litabatilisha kilichotiwa saini hao jamaa wa Dubai kuishtaki JMT kwa kuwaondolea legitimate expectation ya fortune waliyokuwa nayo. Fuatilia kesi za hao waDubai mahakama mbalimbali duniani
 
kubwa ni mashaka ya serikali uwa inaingi mikataba ya ajabu mno huku taifa likipata maslahi kidogo.
Mkuu mimi siongelei huo mkataba sababu siujui ila most of Time humu nawaongelea DP, Jamaa ni real deal na wanaweza kukuza Uchumi kwa Muda mfupi mno.

Case study angalia hapo Djibouti na Senegal. Ndani ya mda mchache DP wame triple uwezo wa Bandari ya Dakar, na juzi hapa wameanza ujenzi wa Bandari itakayogharimu trilioni 3 yenye uwezo wa kuhudumia Meli hadi zenye ukubwa wa mita 400.

Congo wamesaini Juzi na DP bandari yao ya Banana, soon kutajengwa madude hapo hatutawaona wacongo hapa, dunia inaenda kasi, sasa hivi taja Any random company kubwa kubwa Apple, Facebook, Hawa DP, Gazprom ukiangalia mapato yao ni Makubwa kuliko nchi nzima ya Tanzania. Sisi ni Masikini wa kutupwa na huwezi ukawa unatumia njia zile zile ambazo zinafeli kila siku ukatoboa.

Waangalie hio mikataba yao jamaa waje, utaona pale makontena siku moja ama 2 limeshatoka.
 
Nimesikiliza kwa makini sana alichozungumza Zitto Kabwe juu ya hili suala la DP World.

Kwanza ningependa kumpongeza Zitto Kabwe kwa kazi nzuri sana anayoendelea kufanya, kwenye hili ametenda haki na ameonesha ukomavu wa hali juu kama kiongozi wa Chama cha Upinzani (ACT Wazalendo).

Ameweza kuondoa ukakasi kwa maneno machache sana na rahisi mno ambayo kila mtu anaweza kuelewa.

ZK anasema, kwenye jambo hili ni vyema tukatofautisha kati ya hisia na facts, ingawa hawapingi wazungumzao kwa kutumia tu hisia, kwani hisia nazo ni muhimu bali tunapaswa tuwe makini zaidi ili tuepuke upotoshaji ambao kama umejitokeza siku kadhaa nyuma.

Kwenye suala hili, ZK anasema kwamba kulikuwa na sababu za makusudi za upotoshaji, ambazo lengo lake ni kuleta hataruki (confusion) kwa jamii kwa maslahi ya kisiasa.

ZK anasema kwamba kupitia chama chake cha ACT Wazalendo, wametoa tamko linalowaeleza wananchi ni kitu gani kinakwenda kujadiliwa Bungeni. Nipongeze hatua hii kwani kwani vyama vingine mfano CHADEMA, kwenye hili kimekuwa mstari wa mbele kupotosha umma kuliko kuelimisha umma, Hongera ZK kwa hili.

ZK anaendelea, Kinachokwenda kujadiliwa Bungeni ni MoU ambayo imetoka hadharani, MoU ile, ni makubaliano kati ya serikali mbili (Dubai na Tanzania) ambapo makubaliano hayo sasa, yanatoa ruhusa ya serikali yetu kwenda kujadiliana hayo mambo yanayohusu uwekezaji wa DP World, na huko kwenye hayo majadiliano, ndipo tunapaswa tuwe makini kwa sababu ndio tutakapokuwa na masharti yote ya mkataba wa utekelezaji.

ZK kwa umakini wa hali ya juu anasema kwamba, hiki ambacho kinakwenda kujadiliwa Bungeni, "is simply the framework agreement" ambayo ina muda mahususi. ZK anasema, amesoma Kamati ya Bunge inayohusika moja kwa moja na jambo hili, na ripoti ya azimio la ambalo linakwenda kujadiliwa Bungeni inasema kwamba, "Serikali ya Tanzania itahakikisha kuwa, mamlaka ya bandari haitapokea maombi mengine kwenye maeneo ya ushirikiano yaliyoanishwa katika kiambatanisho namba 1 awamu ya kwanza mkapa hapo mazungumzo katika ya TPA na DP World yatakakuwa yamesitishwa au baada ya kupita kipindi cha miezi 12 baada ya kusainiwa kwa MoU".

Sasa basi, ili tuweze kupata mkataba wa utekezaji, ni hadi Bunge lijadili MoU na kutoa ridhaa kwa TPA kuanza majadiliano na DP World ili kuandaa mkataba wa utekelezaji (HGA), sasa kama itatokea TPA na DP World wameshindwana kwenye majadiliano ndani ya kipindi tajwa, serikali inaweza kutafuta kampuni nyingine ya kuwekeza kwenye bandari zetu.

ZK anaendelea kusema kwamba, mjadala wa Bunge juu ya MoU hii ndio muhimu zaidi, yaani ndio msingi mkuu wa HGA, kupitia hapa ndio tunaweza kujua kwamba tunaliwa au tunakula, kwahiyo ni muhimu sana Wananchi kwamba kinachokwenda kuamuliwa na Bunge, sio kuwapa DP World uendeshaji wa bandari zetu, bali kinachokwenda kuazimiwa, ni kuipa ruhusa serikali kuanza majadiliano na DP World, na kama majadiliano hayo yakishindikana, azimio lote halipo tena. Nguvu zetu,tuwekeze kwenye majadiliano ambayo yanakwenda kutupa mkataba wa utekelezaji.

Kwa ufafanuzi huu wa @zittokabwe ,kama mtu hatoelewa basi, na unaua kabisa hoja muflisi za mkataba usiokua na kikomo na mkataba wa miaka 100.
Punguza ujinga, MoU haijadiliwi bungeni maana MoU haina nguvu kisheria. Yenye nguvu kisheria ni mkataba. Na mkataba walisha sign kitambo , bunge linaenda kubariki ujinga huo.
 
Back
Top Bottom