Nimesikiliza kwa makini sana alichozungumza Zitto Kabwe juu ya hili suala la DP World.
Kwanza ningependa kumpongeza Zitto Kabwe kwa kazi nzuri sana anayoendelea kufanya, kwenye hili ametenda haki na ameonesha ukomavu wa hali juu kama kiongozi wa Chama cha Upinzani (ACT Wazalendo).
Ameweza kuondoa ukakasi kwa maneno machache sana na rahisi mno ambayo kila mtu anaweza kuelewa.
ZK anasema, kwenye jambo hili ni vyema tukatofautisha kati ya hisia na facts, ingawa hawapingi wazungumzao kwa kutumia tu hisia, kwani hisia nazo ni muhimu bali tunapaswa tuwe makini zaidi ili tuepuke upotoshaji ambao kama umejitokeza siku kadhaa nyuma.
Kwenye suala hili, ZK anasema kwamba kulikuwa na sababu za makusudi za upotoshaji, ambazo lengo lake ni kuleta hataruki (confusion) kwa jamii kwa maslahi ya kisiasa.
ZK anasema kwamba kupitia chama chake cha ACT Wazalendo, wametoa tamko linalowaeleza wananchi ni kitu gani kinakwenda kujadiliwa Bungeni. Nipongeze hatua hii kwani kwani vyama vingine mfano CHADEMA, kwenye hili kimekuwa mstari wa mbele kupotosha umma kuliko kuelimisha umma, Hongera ZK kwa hili.
ZK anaendelea, Kinachokwenda kujadiliwa Bungeni ni MoU ambayo imetoka hadharani, MoU ile, ni makubaliano kati ya serikali mbili (Dubai na Tanzania) ambapo makubaliano hayo sasa, yanatoa ruhusa ya serikali yetu kwenda kujadiliana hayo mambo yanayohusu uwekezaji wa DP World, na huko kwenye hayo majadiliano, ndipo tunapaswa tuwe makini kwa sababu ndio tutakapokuwa na masharti yote ya mkataba wa utekelezaji.
ZK kwa umakini wa hali ya juu anasema kwamba, hiki ambacho kinakwenda kujadiliwa Bungeni, "is simply the framework agreement" ambayo ina muda mahususi. ZK anasema, amesoma Kamati ya Bunge inayohusika moja kwa moja na jambo hili, na ripoti ya azimio la ambalo linakwenda kujadiliwa Bungeni inasema kwamba, "Serikali ya Tanzania itahakikisha kuwa, mamlaka ya bandari haitapokea maombi mengine kwenye maeneo ya ushirikiano yaliyoanishwa katika kiambatanisho namba 1 awamu ya kwanza mkapa hapo mazungumzo katika ya TPA na DP World yatakakuwa yamesitishwa au baada ya kupita kipindi cha miezi 12 baada ya kusainiwa kwa MoU".
Sasa basi, ili tuweze kupata mkataba wa utekezaji, ni hadi Bunge lijadili MoU na kutoa ridhaa kwa TPA kuanza majadiliano na DP World ili kuandaa mkataba wa utekelezaji (HGA), sasa kama itatokea TPA na DP World wameshindwana kwenye majadiliano ndani ya kipindi tajwa, serikali inaweza kutafuta kampuni nyingine ya kuwekeza kwenye bandari zetu.
ZK anaendelea kusema kwamba, mjadala wa Bunge juu ya MoU hii ndio muhimu zaidi, yaani ndio msingi mkuu wa HGA, kupitia hapa ndio tunaweza kujua kwamba tunaliwa au tunakula, kwahiyo ni muhimu sana Wananchi kwamba kinachokwenda kuamuliwa na Bunge, sio kuwapa DP World uendeshaji wa bandari zetu, bali kinachokwenda kuazimiwa, ni kuipa ruhusa serikali kuanza majadiliano na DP World, na kama majadiliano hayo yakishindikana, azimio lote halipo tena. Nguvu zetu,tuwekeze kwenye majadiliano ambayo yanakwenda kutupa mkataba wa utekelezaji.
Kwa ufafanuzi huu wa @zittokabwe ,kama mtu hatoelewa basi, na unaua kabisa hoja muflisi za mkataba usiokua na kikomo na mkataba wa miaka 100.
Hivi unaongelea habari ya MOU wakati vipengere vya mkataba vimeshajitanaibisha? Au unabebwa na upepo wa Zitto?
Skia mkuu na uache upotoshaji wewe na Zitto wako.
MAMBO YASIYOFAA KABISA MKATABA WA BANDARI.
1. TANZANIA HAIRUHUSIWI KUJITOA KWENYE MKATABA
Ibara ya 23(4) ya mkataba huo inakataza wahusika wa mkataba ambao ni serikali ya Tanzania na Kampuni mwekezaji DPW kujitoa(Denounce) katika mkataba, Kuvunja, Kuahirisha(suspend), au Kusitisha(terminate).
Na ni masikitiko sana kuwa ibara hii imesisitiza kuwa haturuhusiwi kujitoa kwenye mkataba huu hata kama kuna ukiukwaji mkubwa wa masharti(Material Breach), hata kama kuna mabadiliko makubwa ya kimazingira katika utekelezaji wa mkataba(fundamental change of circumstances), hata kama kuna mgogoro mkubwa wa kidiplomasia(severe diplomatic/condular dispute), au sababu zo,ote zile zinazotambulika na sheria za kimataifa.
Maneno haya yameandikwa hivihivi kwenye huo mkataba. Si mlisema ule Fei toto, sasa upo huu mbele yenu.
2. MKATABA HAUNA MUDA
Ibara ya 23 ya mkataba inasema kuwa ukomo wa mkataba huu ni mpaka shughuli za mradi zitakapokuwa zimekamilika. Maneno haya yameandikwa hivihivi.
Serikali inawajibika kutoa maelezo kuhusu hili. Katika sheria hakuna mkataba usio na muda isipokuwa mkataba wa kuuza au kununua tu.
Ukimuuzia mtu kitu haumwambii tumia mpaka muda fulani, ni moja kwa moja. Je na huu mkataba ni hivyo ??.
3. MIGOGORO KUHUSU MRADI KUTATULIWA AFRIKA KUSINI.
Ibara ya 20 ya mkataba inasema migogoro kuhusu mkataba wa mradi utatatuliwa Johannesburg Afrika Kusini na Sheria itakayotumika ni sheria za umoja wa mataifa UNICITRAL Arbitration Rules.
Kumbuka mwaka 2017 tulitunga sheria yetu kwa ajili ya kulinda rasimali zetu.
Katika sheria hii The Natural Wealth and Resources , Parmanent Sovereignty Act 2017, tuliweka wazi katika kifungu cha 11 kuwa Migogoro yoye inayohusu Rasilimali za Taifa hili itatatuliwa na vyombo vya hapa nchini kwa sheria zetu.
Na hiii ilikuja baada ya kuonekana hawa wanaojiita wawekezaji wanatunyonya kisha tukilalamika wanatuburuza kwenye vyombo vyao tena kwa sheria zao.
Unamshitaki mtu kwenye mahakama yake mwenyewe kwa kutumia sheria alizotunga yeye mwenyewe, halafu unategemea upate haki.
Tulitunga sheria hii kujikomboa na huu ukoloni. Mkataba huu sasa unataka kuturudisha huko.
4. TANZANIA HAINA MAMLAKA YA KUTAIFISHA MALI ZA MWEKEZAJI.
Ibara ya 14 ya mkataba inakataa kabisa Serikali ya Tanzania kutaifisha mali yoyote ya mwekezaji.
Yaani hakuna sababu yoyote iwe ya kimadai au kijinai itakayoifanya serikali itaifishe mali ya mwekezaji.
Mnajua kuwa suala la kutaifisha lipo kisheria hasa inapothibitika jinai. Lakini hii si kwa mwekezaji wa Bandari.
Ibara hii inasisitiza kuwa endapo itatokea mali zao kutaifishwa na serikali basi fidia na stahiki ya kuridhisha italipwa na serikali. Neno STAHIKI YA KURIDHISHA limetumika hivyohivyo kwenye mkataba.
Hatujui hiyo ya kuridhisha itakuwa ni kiasi gani lakini limeandikwa hivyohivyo.
5. KUTUNGA SHERIA MPYA.
Ibara ya 27 inasema baada ya mkataba kusainiwa Tanzania haitakuwa na mamlaka ya kutunga sheria, kanuni mpya ambayo itapingana na mkataba.
Tafsiri yake, kama mna marekebisho yenu ya kikodi, sera pengine kutokana namabadiliko na mda kupita hamtaruhusiwa.
Uchambuzi utaendelea.