Zitto Kabwe atoa hoja nzito juu ya uwekezaji wa DP World Tanzania

Nasikia mwenye jina hili ni wa kiume sio wa kike kama unavyojiita Gertrude Mollel...

Swali langu je, kama tu umeamua kujiita jina kike, kuna uhalali gani wa kuamini ulichoandika?
 
Kongole kwake kamarada ZZK[emoji7]

Usimfananishe Zitto na kile chama cha akina Mdude Nyagali [emoji1787][emoji1787]

Chama cha kitapeli kileee....

Umeona wapi duniani wanachama wa chama cha mrengo wa kulia kidogo....wanavaa MAGWANDA NA BERETI NYEKUNDU ??!![emoji1787][emoji1787]

Utapeli mtupu [emoji1787]
 
Mara EDA ,HGA DP ,Chama cha kijani ,MP Sasa mtanzania maskini ,mkulima anaelewa Nini? si muendelee kuiuza nchi kimya kimya😅😅
 
Eti tunaliwa au tunakula. Kuliwa lazima Hamna uwezo wa kumzidi akili mwekezaji na tulishaona mikata mingi tu.
 
Tena uyo ndio mtetezi mkubwa wao
 
Memorandum of Understanding kati ya serikali ya Tanzania na taasisi nyingine yoyote ile huwa haijadiliwi bungeni! MOU siyo binding. Iweje MOU ambayo siyo binding ipelekwe kujadiliwa bungeni halafu mikataba ambayo ni binding haijadiliwi bungeni? Angalau hata kwa kupitia executive session.
 
Mwanangu una hoja sema hujui kuiwasilisha, kuifafanua, kuitetea na kushawishi.
 
Kwa elewa wangu

1. Mkataba umeandikwa na Mwekezaji peke yake.

2. Anataka apewe Bandari zote.

3. Anataka azimiliki milele

4. Anataka alikosea ashtakiwe Afrika Kusini tu

5. Anataka akikosea zitumike sheria za Uingereza.

6. Anataka hata asipotimiza malengo yake na kuharibu kwa jambo lolote mali zake zisitaifishwe.

Swali.
1.Tumemwamini vipi kuwa Mwekezaji hata fanya hujuma ?

2. Akifanya hujuma tutamdhibiti vipi wakati kutupa masharti ya kutoshtakiwa kwetu na kwa sheria zetu ?

3. Tunamwamini vipi Mwekezaji asiyethamini sheria na taratibu zetu ?

4. Kwanini tusimpe Bandari moja kwa majaribio cha kipindi hata cha miaka kadhaa ili akifanya vizuri tumpe na nyingine, akifanya vibaya iwe nafuu kwetu ?

NB
Hili jambo lina maslahi ya Kitaifa kwanini tupate mda wa kusikiliza mawazo ya Watanzania wote wakijumishwa vyama vyote na taasisi zote ili kujiridhisha?

Kwa nini jambo kubwa la Kitaifa kama hilo lilazimishwe kuamuliwa na watu wachache tu na kwa muda mchache ?

Kama Mwekezaji kajipambanua kuwa ana uwezo mkubwa basi zingatieni swali langu la (4) hapo juu ili kwanza kujiridhisha naye.

Hata huko Wingereza vyanzo vinasema kapewa mamlaka ya kuiendesha Bandari Mbili (2) tu. Tumpe moja kwa kipindi maalum tujiridhishe kwanza. Tumpe Bandari ya Tanga tuone.

Hata ndoa ambazo watu wanafunga kwa mapenzi ya hali ya juu, nyingi zinaishia na migogoro na kuachana. Vipi kumwamini asilimia 100 mtu baki ?

Kwako Mis
getrude,
 
Punguza ujinga, MoU haijadiliwi bungeni maana MoU haina nguvu kisheria. Yenye nguvu kisheria ni mkataba. Na mkataba walisha sign kitambo , bunge linaenda kubariki ujinga huo.
Hivi mkataba ulishasainiwa? Ulihusisha watu gani?

Wanasheria wanaodeal na Masuala ya uwekezaji walihusishwa?

Mkataba unatangulia kusainiwa kabla ya Bunge kujadili? Kisheria na kiutaratibu ni sahihi?
 
Yaani kisomo cha Zitto kinamtofautisha saana na wale wengine wanaotumia siasa za maji taka kupotosha kama Mzee Mbowe na wachagga wenzake
 
Jamani inatoshaaa.....hatutaki DP World kwa sasa tujipange upya ....Kwa miaka 5 mingine .....hatutakiiii
 
Umendika kwa hoja kali Kati ukachafua Hali ya hewa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…