Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Kuna mvutano Kati ya makundi ya Kanda ya ziwa na pwani.

Lakini Bandari ya Bagamoyo ni Macro Economic Project..
Kuna ulazima wa kupitia Mikataba vizuri, na Tender ishindandishwe kulingana na Public Procurement act
 
Hahahaaaa...... !

Mchina akitimba Bagamoyo wazaramo wote watasukumiziwa Msata na Pangani.
Kuna watu wanasubiria wauze maeneo yao
Sana sana wakipata hela wataongeza wake tu na wamama watatafuta viben10 tu
Kwishneyyy

Ova
 
Khaa . . management fees ? Pumbavu kabisa

hapo kuna mishahara yao utakuta ni 20,000.00 USD PM and above hapo kuna DG, kuna DF, kuna Mtu wa Operations, kuna ndege hapo ya kupiga misele, kuna kumwita fundi wa cranes au computer system
kuna mishahara yao utakuta ni 20,000.00 USD kwa mwezi and above kwa DG, DF, Mtu wa Operations, kuna ndege hapo ya kupiga misele, kuna kumwita fundi wa cranes au computer
 
Tatizo lenu hamtaki kusikiliza!

Mngekuwa mnasikiliza hoja na kizipima badala ya kupinga tu kwa kuwa mtoa hoja humpendi.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo,ulikuwa ujengwe kwa makubaliano ya uwekezaji wa pande tatu,Tanzania,Oman na China. Wawekezaji wangejenga miundo mbinu ya bandari na industrial parks kwa ajili ya viwanda zaidi ya 800 na kuchukua port charges kwa kipindi cha miaka 50. Serikali haikuyakiwa kutoa hata sumuni! Katika kipindi hicho serikali itachukua kodi zingine mbalimbali kama ushauri wa forodha kama kawaida. Baada ya miaka hiyo, bandari inakuwa mali ya serikali 100%

Utaratibu huu ndio unaotumika hata sasa kwenye bandari ya Dar. Wapo TICTS wanaendesha bandari hiyo.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo unamanufaa makubwa katika uchumi wa Tanzania. Pamoja na kuifanya Tanzania kuwa lango juu la bidhaa kwa zaidi ya nchi 8 za Afrika,unaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vya kisasa ambavyo vitahudumia soko la ndani na nchi nyingine za Afrika.

Mradi huu utazalisha ajira nyingi mno katika sekta mbalimbali kama mahoteli, usafirishaji nk.
Ajira nyingi za watoto wa wenye madaraka sio
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] waafrika bana. Mnapenda sana symbolism. Ati utakua ni mradi mkubwa afrika nzima. Ukiwa mkubwa afrika nzima bila kukunufaisha ni sawa lakini ukiwa mdogo afrika nzima na ukakunufaisha hutaki. Mpaka uwe mkubwa haijalishi utakunufaisha au la
 
Tunajua jinsi rais yule anavyojaribu kurudisha mradi huu kwa nguvu zote kupitia waganga njaa.
 
Wazungu wanasema "The Devil is in the details"
Habari ndiyo hiyo....
Huu mkataba upo na Sri Lanka alishaingizwa chaka......

1618521283098.png

KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania

Kisha hizi meli tunazoziona zikileta mizigo Dar port ndio zitakuwa zinabeba miizigo kutoka Bagamoyo na kusambaza sehemu mbalimbali duniani amesisitiza Zitto

Tusiiache fursa hii jamani na siyo kweli kwamba kila mradi ulioanzishwa awamu ya Kikwete ulikuwa mbaya kwani hata reli ya SGR mradi uliasisiwa vizuri na serikali ya JK lakini serikali ya awamu ya tano imekuja kuutekeleza kwa namna tofauti, amemalizia Zitto.

Chanzo: Clouds 360
Bila data kuhusu economic feasibility study, environmental impact study na project financial resources hizi ni ndoto tu.
 
Kwa gharama ipi , ya kuuza hiyo Bandari kwa wawekezaji.
Kwani mkataba upoje jamani mbona mnatuchanganya!!CAG mstafu aliuomba akanyimwa!!mimi siku zote sikuwahi na sitawahi kumuamini meko.
 
Hii nchi kwa sasa inashuhudia siasa za Karne ya '21...this is called 'Lobbying',bought and paid for...nchi za wenzetu mara nyingi unakutana na wanasiasa wnye mirengo miwili tofauti wanafananaga mawazo mara moja moja ,kumbe wameshachangiwa kwenye mifuko ya kampeni,au they have exchanged favors with their corporate buddies... I don't think our minds can quite comprehend these type of politics,tutasema wanatuchanganya and leave it as it is, kumbe ndo aim yao hio,kutupotezea interest huku wao wakifaidika
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania

Kisha hizi meli tunazoziona zikileta mizigo Dar port ndio zitakuwa zinabeba miizigo kutoka Bagamoyo na kusambaza sehemu mbalimbali duniani amesisitiza Zitto

Tusiiache fursa hii jamani na siyo kweli kwamba kila mradi ulioanzishwa awamu ya Kikwete ulikuwa mbaya kwani hata reli ya SGR mradi uliasisiwa vizuri na serikali ya JK lakini serikali ya awamu ya tano imekuja kuutekeleza kwa namna tofauti, amemalizia Zitto.

Chanzo: Clouds 360
Zitto yupo very smart katika kupita na kiki, I will never trust him. Sikatai ni msomi mzuri japo siasa inaharibu talent yake.
 
Katika hili hatupo pamoja! Je bandari zetu zilizopo hamna kitu cha kufanya kukidhi haja? Mameli makubwa yalete nini kilichoshindwa kuletwa na meli za kawaida? Hivi mna mkataba na 'locked countries' kwamba lazima watumie bandari zetu? Msituongezee deni la taifa kwa kugharamia vitu visivyo na tija, wakati wastaafu awapati mafao, ajira hakuna, mishahara madaraja/hayapandi.
 
Basi tuwakubali kwenye mkataba waongeze kakipengele ka kuandaa sehemu ambayo wananchi watakuwa wanaenda kufaidika kuyaona mameli makubwa, tutakuwa tunatembea kifua mbele kwakuwa wa kwanza kupokea mameli makubwa
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania

Kisha hizi meli tunazoziona zikileta mizigo Dar port ndio zitakuwa zinabeba miizigo kutoka Bagamoyo na kusambaza sehemu mbalimbali duniani amesisitiza Zitto

Tusiiache fursa hii jamani na siyo kweli kwamba kila mradi ulioanzishwa awamu ya Kikwete ulikuwa mbaya kwani hata reli ya SGR mradi uliasisiwa vizuri na serikali ya JK lakini serikali ya awamu ya tano imekuja kuutekeleza kwa namna tofauti, amemalizia Zitto.

Chanzo: Clouds 360
Ingawa umeandika analyitically lakini unaupigia debe mradi wa bandari ya Bagamoyo utekelezwe kinyume na maamuzi ya JPM kuwa usitekelezwe. Nami naona nikujibu kiuchambuzi kwa nini usijengwe. Katika uchambuzi huu nitatumia pia hoja za wengine wenye mawazo kama yako.

Kwanza, Ndugai mwanzoni kabisa alisema kuwa Magufuli alishauriwa vibaya. Wote tunamfahamu Magufuli kama mtu makini sana katika kusoma document hata iwe kubwa kiasi gani si rahisi kumchomekea kitu asikione, pili kati ya Ndugai na JPM ambaye anaweza asiwe na access ya document ni Ndugai lakini sio JPM kwa kuzingatia nafasi yake hivyo hoja ya Ndugai kuwa Magufuli alishauriwa vibaya haina mantiki kabisa ila Ndugai aliitumia kama gia ya kutaka kujenga uhalali wa kureverse maamuzi ya Magufuli kuhusu kukataa kujengwa kwa bandari hiyo.

Mnaoupigia debe mradi huo mnadai kuwa bandari ya Bagamoyo ina kina kirefu maji hayajai na kupwa hivyo ndio sehemu inayofaa kujengwa bandari ya kupokea meli hizo kubwa na kuwa bandari ya DSM haiwezi kupanuliwa kuchukua meli kubwa za mita mia tatu au mia nne. Sasa kwa nini mkataba ukataze kujenga bandari ya DSM au nyingine yeyote kuanzia Tanga hadi Mtwara? Hao wawekezaji na nyinyi mnaogopa nini hiyo bandari ya Bagamoyo kushindana na bandari zingine za Tanzania? kwa nini mnaikingia kifua dhidi ya bandari zingine? Busara ya kawaida hapa ni kuwa wao kama wangewekeza (japo mimi napinga) basi wangekuwa tayari kwa ushindani na sio kutaka upendeleo wa kipekee.

Mnadai meli kubwa ndizo zitakuwa zinatia nanga bandari ya Bagamoyo sasa kwanini hamtaki hizo meli mnazoziita ndogo ziendelee kutia nanga katika bandari ya Dsm, Tanga na Mtwara? Kwa nini mnataka kuziua bandari zingine ikiwa lengo ni bandari ya Bagamoyo kuhudumia meli kubwa za mita mia tatu au mia nne?

Pia mnadai kuwa meli kubwa zitaleta mizigo Bagamoyo kisha baada ya kupakuliwa mizigo hiyo itabebwa na meli ndogo kupelekwa sehemu zingine! Uongo ulioje! Hizo sehemu ni zipi? Jiografia ya Tanzania ni kuwa sisi tumezungukwa na nchi sita zisizo na bandari ambazo ni Malawi, Zambia, Congo Mashariki (ingawa atlantic ocean wanayo), Rwanda, Burundi na Uganda. Nchi tatu za mwisho huwa tunashindana na Kenya katika kugombania mizigo yao hivyo wanaotutegemea kabisa ni nchi tatu za mwanzo. Pia hata kwa Zambia huwa tunashindana na bandari ya Durban. Mizigo inapoletwa katika bandari zilizopo hubebwa kwa reli na malori kupelekwa huko katika nchi hizo hivyo suala la meli ndogo ndogo kuichukua mizigo na kuisambaza haina mantiki kabisa, Pia jiografia ya Africa, mizigo inayokwenda Africa kaskazini au Magharibi kutoka Asia ni rahisi kupita Suez canal, mediteranian kisha kwenda huko hivyo haiwezekani mizigo yao ije huku East Africa kisha irudi huku North au west Africa. Hali kadhalika kwa mizigo inayotoka bara la America haiwezi kuletwa huku kwetu kisha ipakiwe tena kwenda West Africa au hata South Africa. Pia mizigo ya Africa Kusini inayotoka Asia haiwezi kuletwa Bagamoyo kisha ipakiwe tena kwenda Africa Kusini. Ni wazi mizigo ya Africa Kusini kutoka Asia moja kwa moja inapelekwa bandari ya Durban ambayo ni bandari kubwa. Hivyo hoja kuwa sisi tutakuwa tunahudumia mizigo ya nchi zenye bahari kama sisi ni hoja mufilisi isiyo na mashiko. Sisi urefu wa Kamba yetu utaendelea kuwa nchi zisizo na bandari zinazotuzunguka tu na ambazo zinahudumiwa vyema na bandari za DSM, Tanga na Mtwara vizuri na kwa ufanisi.

Reli ya kutoka bandari ya Mtwara hadi Mbababay ikikamilika, tutakuwa na uhakika wa kuihudumia Malawi kwa ufanisi zaidi kuliko bandari ya Bagamoyo. Hali kadhalika bandari ya Tanga imepanuliwa na SGR ikikamilika mizigo ya Congo Mashariki, Rwanda, Burundi, Uganda itahudumiwa kwa ufanisi zaidi.

MAPATO

Serikali kupitia mamlaka ya bandari inapata pesa za handling na storage ya mizigo pamoja na kodi/tozo mbali mbali za forodha zinazokusanywa na TRA kutokana na meli zinazotia nanga katika bandari ya DSM, Tanga na Mtwara; lakini bandari ya Bagamoyo ikijengwa mamlaka hizo hazitakusanya mapato huko na wakati huo huo bandari hizo zitakuwa zimeminywa meli zisitie nanga huko, badala yake mapato hayo na mengine ambayo projections zinaonyesha yataendelea kukua yatakuwa yanachukuliwa na wawekezaji hao toka China na Oman kutokana na meli kutia nanga bandari ya Bagamoyo, ujinga ulioje. Tuwe wakweli hata bandari hiyo ya Bagamoyo ikijengwa asilimia kubwa ya meli zitakazokuwa zinatia nanga ni hizi hizi zinazoitwa meli ndogo ambazo kwa sasa zinatia nanga bandari za Dsm, Tanga na Mtwara. Wakina Ndugai wanapigia debe hata haya mapato tunayoyapata sasa kupitia bandari zetu tuyakose badala yake yakusanywe na kuchukuliwa na wachina kwa kisingizio mradi una manufaa. Mbona hawatauambii quantifiable revenue amount ambayo tutakuwa tunapata bandari ya Bagamoyo ikifanya kazi badala yake wamekalia kusema mradi una manufaa sana lakini hawatupi figure?

UJENZI WA VIWANDA

Hoja nyngine ambayo inapigiwa debe na kufungamanishwa na ujenzi wa bandari ni ujenzi wa viwanda katika ukanda huo wa Bagamoyo. Swali rahisi hivi ni lazima mtu akitaka kujenga viwanda lazima ajenge na bandari? Kama hao wawekezaji wana nia ya kujenga hvyo viwanda hawajakatazwa kwani eneo la Bagamoyo ni moja ya meneo yaliyoainishwa kama EPZ, Hivyo wanaweza kuja kupitia TIC na kupewa ruhusa ya kujenga viwanda. Jambo la msingi wajenge viwanda kwa terms zilizo sawa na wawekezaji wengine katika EPZs zingine na wasipewe upendeleo wa kipekee kuliko wawekezaji wengine wanaojenga viwanda. Ukipita barabara ya Kilwa kuelekea Mkuranga, njia ya Chalinze na Tanga, utaona kuna viwanda vya wachina vimejengwa/vinaendelea kujengwa; mbona hao hawakufungamanisha ujenzi wa hivyo viwanda na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo?

Ujenzi wa viwanda na ujenzi wa bandari ni vitu viwili tofauti ambavyo mwekezaji hana uhalali wa kulazimisha kuwa lazima afanye vyote. Amekataliwa bandari ajenge hivyo viwanda. Kama atahitaji bandari za kuimport raw materials au export ya bidhaa zake atatumia bandari zilizopo. Hoja kuwa bandari ya Bagamoyo ikijengwa na viwanda 700 vitajengwa haina mashiko kwa sababu hayo mambo mawili siyo lazima yafanyike pamoja.

Hoja yako kuwa China inaitambua Bagamoyo katikampango wake wa Belt and Road sisi haituhusu kwani hiyo ni mikakati yao ya kuitawala na kuinyonya dunia. Kwani hata kama tungeamua kujenga bandari ya Bagamoyo ni lazima wajenge wachina? Hatuwezi kujenga kwa nguvu zetu?

Watu wanapopata nafasi za uongozi wajifunze kuiga uzalendo kama ambavyo viongozi wa mataifa ya Uchina na mengine yaliyoendelea wanavyoweka maslahi ya nchi zao mbele hata kama ni kwa kunyonya nchi zingine.

Bandari ya Baagamoyo ikifanikiwa kujengwa basi itakuwa ni ufisadi kama ufisadi mwingine uliokuwa unafanyika huko nyuma hususan awamu ya nne.
 
Back
Top Bottom