Nadhani wewe ndio unachanganya mambo hapa, mimi naelewa vizuri. Hawa waliingia katika matatizo kwa ajili ya kukopa pesa nyingi China haikuwa uwekezaji wa kibiashara. Sisi issue ya Port ni uwekezaji wa makubaliano ya kibiashara. nikupe mfano miwili sisi na hao Srilanka. chukuwa wewe una kiwanja Kariakoo anakuja mfanya biashara anakwambia nipe kiwanja nijenge gorofa ikiisha nakupa maduka 4 mimi nachukuwa 10 baada ya miaka 20 nikiwa nimerudisha pesa zangu nitakupa wewe 10 na mimi 4 baadaya muda nyumba yote yako, huu uwekezaji wa kibishara na makubaliano ndio yetu Bagamoyo. Hao wengine ni kuwa walikuwa na kiwanja wakaenda Bank kukopa pesa nyingi biashara imekataa kurudisha hawawezi Bank inachukuwa nyumba. msichange mikopo na investment kama kukopa tumekopa kipande cha mwisho cha SGR toka Mwanza huo ni mkopo na lazima urudishwe, tulikopa Gas line toka Mtwara ndio mikopo. Ukisoma zote ulizonitumia ni kuwa walichukuwa mikopo
Sasa hapo hapo kwenye mfano wako nani ana control cost za investment , pili nani ana control rent, na kwa ujumla revenue wakati wewe huhusishwi ktk hiyo biashara, halafu risk nyingine ikiwa biashara isiende vizuri hivyo wasirudishe hela yao ktk kipindi walicho sema inakuwaje.
Mwisho kuna kitu kinaitwa substance over form.
Kimsingi mtu anapoweka sharti la kurudisha pesa yake na faida ni mkopo. Usidanganyike na haya maneno mengine ya uwekezaji wa kibiashara.
Another
example is the situation where a company short of cash sells its machinery to the bank and then leases the same property from the bank. ... Under the
substance-
over-
form principle, the sale and subsequent leaseback are considered
one transaction.
Hapa zimechukuliwa kwamba umekopa na sio umeuza hiyo machinery , na hela ya ku lease zimechukuliwa kama ni ya kulipa mkopo interest na principal
Ndio maana kwenye mambo kama haya tunatakiwa kuwatumia wataalamu na sio wanasiasa,
Hapa mwana siasa atakwambia huyu anatujengea sio anatukopesha na masharti yake ni nafuu kulinganisha na nini hakwambi,
Ndio tukaishia kujenga jengo la umoja wa vijana, uwt n.k n.k