Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Kuna Bandari MTWARA ina kina kirefu ambacho kipo kiasili,hatuwezi kutumia nguvu nyingi kuendeleza!
Naona bandari zingine muhimu zinapotezewa bila kutengenezewa mkakati
Ile siyo bandari kama ya mtwara ilikuwa iwe bandari tofauti na nyingine zote na inhekuwa kubwa ya 3 duniani. Sema shida ni kwamba huo mkataba zaidi ya ikulu hata wabunge hawajui kilichomo hawakuwahi kuuona.
 
Mkataba uwe wazi na unajari sovereignty ya Taifa letu
Ndicho anachotaa uwekwe wazi tuone kaa ulikuwa na manufaa ama haukuwa na manufaa kwa taifa watu wauchambue waujadili hilo hata yeye ndilo anataka
 
Ile siyo bandari kama ya mtwara ilikuwa iwe bandari tofauti na nyingine zote na inhekuwa kubwa ya 3 duniani. Sema shida ni kwamba huo mkataba zaidi ya ikulu hata wabunge hawajui kilichomo hawakuwahi kuuona.
Yaani Bandari ya Dar ilikua inaingia Mara 25 kwa ukubwa kwenye hiyo Bandari ya Bagamoyo
 
Hii tabia ya kushambulia watu bila kusikiliza hoja zao inashangaza. Hebu jaribu kuweka hisia zako pembeni kamsikilize halafu rudi uchangie.
Katoa maelezo mazuri sana.
1. Katwambia walichoona wao na wabunge wengine ni presentation ya hiyo bandari.
2. Ile haikuwa bandari ya kawaida kama iliyokuwepo bali ililenga kupokea meli kubwa sana zishushe mizigo halafu meli hizi tulizozoea ziichukue na kuisambaza afrika na kwingineko.
3. Ingemaliza ingekuwa bandari ya 3 kwa ukunwa duniani
4. Hata bunge halikuwahi kuona mkataba wake ni ikulu tu waliyouona hivyo hata wao hawajui kilichomo zaidi ya kusikia kutoka kwa mwendazake, hivyo ingekuwa bora ungewekwa wazi ili watu wauchambua tujue yaliyomo.
5. Bandari ilikuwa ijengwe kwa ushirikiano wa Tanzania, China na Oman
6. Raisi Mwinyi ashawawahi waomna watajenga bandari zanzibar, hivyo anaona hakuna tena umuhimu wa kujenga bandari ya bagamoyo unless iwepo plan ya hiz bandari kushirikiana maana sisi ni nchi moja.
Sasa wapi alipokosea?
Why now?mbona inapigiwa upatu sana?ina maana hakuna miradi mingine muhimu zaidi ya huo?
Watu washakula % na uwakala lazima waupiganie.
Usiamini mwanasiasa-by zito mwenyewe
 
Yaani Bandari ya Dar ilikua inaingia Mara 25 kwa ukubwa kwenye hiyo Bandari ya Bagamoyo
Masharti aliyosema JPM ambayo wachina walitupa mbona hawayasemi , kukubali ama kukanusha. Kama ni yale masharti JPM ni shujaa tu. Mameli makubwa bila tuna yana faida gani. Watueleze ni wapi machina alijenga mradi ukalikomboa taifa
. Mbona nchi nyingi zinasurrenddr bandari kurudisha madeni ya machina . Mikataba ya sultnai Mangungo MUNGUapishe mbali.
 
Kwakuwa aliyekuwepo hakutaka mawazo tofauti akikusikia kitakachokupata wanakijua kilichowapata. Hivi shida iko wapi kuweka mkataba wazi maana hata yeye hajasema utekelezwe bila huo mkataba kuwekwa wazi.
Ni now kwasababu ndiyi watu wanajisikia huru walau kuzungumza mawazo yao. Mbona wakati wa JK watu walikuwa wanazungumza tu akitaka atayachukua akigoma basi sasa hiyo chance waliikosa sasa wameipata.
 
😂😂😂😂wakati wa jk?muswada unaletwa asubuhi bungeni kwa mara ya kwanza,jioni ushapitishwa.
 
Masharti aliyosema JPM ambayo wachina walitupa mbona hawayasemi , kukubali ama kukanusha. Kama ni yale masharti JPM ni shujaa tu. Mameli makubwa bila tuna yana faida gani. Watueleze ni wapi machina alijenga mradi ukalikomboa taifa
. Mbona nchi nyingi zinasurrenddr bandari kurudisha madeni ya machina . Mikataba ya sultnai Mangungo MUNGUapishe mbali.
Aliyasema yeye ambaye alikwambia ATCL ilikuwa inatengeneza faida hadi kutoa gawio.
Zitto yeye hajayasema kwakuwa kakiri mkataba ikulu haijawahi kuuweka wazi hata wabunge hawajawahi kuuona hivyo kaomba uwekwe wazi ili kila mtu aone na wataalam wauchambue.
Hayo uliyoambiwa umeambiwa tu mkataba wenyewe haujawahi kuwa wazi
 
Tatizo lenu hamtaki kusikiliza!

Mngekuwa mnasikiliza hoja na kizipima badala ya kupinga tu kwa kuwa mtoa hoja humpendi.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo,ulikuwa ujengwe kwa makubaliano ya uwekezaji wa pande tatu,Tanzania,Oman na China. Wawekezaji wangejenga miundo mbinu ya bandari na industrial parks kwa ajili ya viwanda zaidi ya 800 na kuchukua port charges kwa kipindi cha miaka 50. Serikali haikuyakiwa kutoa hata sumuni! Katika kipindi hicho serikali itachukua kodi zingine mbalimbali kama ushauri wa forodha kama kawaida. Baada ya miaka hiyo, bandari inakuwa mali ya serikali 100%

Utaratibu huu ndio unaotumika hata sasa kwenye bandari ya Dar. Wapo TICTS wanaendesha bandari hiyo.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo unamanufaa makubwa katika uchumi wa Tanzania. Pamoja na kuifanya Tanzania kuwa lango juu la bidhaa kwa zaidi ya nchi 8 za Afrika,unaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vya kisasa ambavyo vitahudumia soko la ndani na nchi nyingine za Afrika.

Mradi huu utazalisha ajira nyingi mno katika sekta mbalimbali kama mahoteli, usafirishaji nk.
Watu wanakuwa na jazba sana yani hat sielewi.
Kwani kama ukienda karume kununua viatu jamaa sianza haya na kama 70,000. Ukiwa jinga basi utatoa hiyo hiyo . Lakini kama mjanja basi unaongea nae unaishia kununua kwa 15,000.

Katika hiyo picha hapo juu mchina ndo yule muuza mitumba wa karume na sisi ndo wanunua viatu.

Tukae, tuzungumze, kutafute dili la ushindi kuingia nao mkataba.

Kiukweli hapo bandarini hakuna nafasi tena. Hivi gati la 25 kwa mfano tutajenga wapi? ?

Kama tunataka uchumi wetu upae basi hii bandari ijengwe. Ila kwa matakwa yetu. Sio ya mchina wala mwarabu.
 
😂😂😂😂wakati wa jk?muswada unaletwa asubuhi bungeni kwa mara ya kwanza,jioni ushapitishwa.
Kwani kulikuwa na tofauti gani na wakati wa JPM hata waliokuwa wanataka budget ifanyiwe marekebisho basi wakaitwa wasaliti. By the way umeuliza why now, nimekujibu kwakuwa now ndipo wana uhuru wa kuzungumza.
Kwani shida iko wapi kwa huo mkataba kuwekwa wazi?
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania

Kisha hizi meli tunazoziona zikileta mizigo Dar port ndio zitakuwa zinabeba miizigo kutoka Bagamoyo na kusambaza sehemu mbalimbali duniani amesisitiza Zitto

Tusiiache fursa hii jamani na siyo kweli kwamba kila mradi ulioanzishwa awamu ya Kikwete ulikuwa mbaya kwani hata reli ya SGR mradi uliasisiwa vizuri na serikali ya JK lakini serikali ya awamu ya tano imekuja kuutekeleza kwa namna tofauti, amemalizia Zitto.

Chanzo: Clouds 360
Yuda katika ubora wake....ni mtu mpumbavu tu ndie atakayemtilia maanani.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16].
Kabla sijafa nataka niione bandari yangu ya bagamoyo.
Hatuwezi kutegemea bandari ya dar miaka yote.
 
Huu mradi wa bagamoyo inaonekana kuna watu walishakula hela za wachina, ndani ya mwezi baada Magu kutangulia bwana speaker kalirudisha upyaaa...tuanze naye
 
Inawezekana kweli uongozi uliopita waliamua kuuchafua huo mkataba kwa maslahi yako,msome huyu jamaa hapo [emoji116][emoji116]

Tatizo lenu hamtaki kusikiliza!

Mngekuwa mnasikiliza hoja na kizipima badala ya kupinga tu kwa kuwa mtoa hoja humpendi.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo,ulikuwa ujengwe kwa makubaliano ya uwekezaji wa pande tatu,Tanzania,Oman na China. Wawekezaji wangejenga miundo mbinu ya bandari na industrial parks kwa ajili ya viwanda zaidi ya 800 na kuchukua port charges kwa kipindi cha miaka 50. Serikali haikuyakiwa kutoa hata sumuni! Katika kipindi hicho serikali itachukua kodi zingine mbalimbali kama ushauri wa forodha kama kawaida. Baada ya miaka hiyo, bandari inakuwa mali ya serikali 100%

Utaratibu huu ndio unaotumika hata sasa kwenye bandari ya Dar. Wapo TICTS wanaendesha bandari hiyo.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo unamanufaa makubwa katika uchumi wa Tanzania. Pamoja na kuifanya Tanzania kuwa lango juu la bidhaa kwa zaidi ya nchi 8 za Afrika,unaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vya kisasa ambavyo vitahudumia soko la ndani na nchi nyingine za Afrika.

Mradi huu utazalisha ajira nyingi mno katika sekta mbalimbali kama mahoteli, usafirishaji nk.

It makes sense ,hauwezi kula bila kuliwa ,hatutoi hata senti tano ,tunajengewa miundombinu ya kutosha ,viwanda zaidi ya 800 (Ajira kwa wanyonge) - Mnyororo wa thamani ,lango la nchi 8 za africa(Uchumi kukua) ,Kodi za forodha....Faida kubwa sana hii...Serikali ifanye tathmini kwenye miaka wapunguze iwe hata 30 na wao wabadilishe terms.
 
Naona wanasiasa wameanza kutafuta umaarufu juu ya hiyo bandari...ili mradi tu wawe kinyume na mitazamo ya mwendazake
 
Back
Top Bottom