Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Hivi Yericko unamtafuta nini Zitto yaani umemshindwa Twiter umekimbilia uku kuja kumshambulia sasa naanza kuamini kwamba wewe Yericko ni mtu ambaye hujitambui
 
Zitto akipewa uenyekiti wa Pac atawaacha wenzake solemba ahah

Watulie
 
Walichofanya cdm jana, nawaza angekifanya Zitto ingekuwaje?.

Walichofanya Cdm jana ndio alikuwa anakifanya Zitto nyakati za Kikwete akaitwa mnafiki, leo nisahihi kabisa Zitto kuwaita wanafiki Chadema maana waliyokuwa wanamtuhumu nayo, ndio wameanza kuyafanya.

Kamwe mwenye nguvu haombwi maridhiano, bali mwenye nguvu ndio huomba maridhiano pindi anapoona nguvu zake zinataka kupunguzwa na wafuasi wavyama vingine.

Chadema jana mmejidhalilisha na naamini JPM hatawapa nafasi ya maridhiano bali atawananga kwenye mikutano yake ijayo.

Inawezekana mlikuwa na lengo zuri, lkn sikwawakati huu baada yakususia uchanguzi wa vitongoji na vijiji.

Labda niulize tu Chadema wanaomba maridhiano ya nini?.

Waruhusiwe na Magufuli kufanya mikutano ya siasa?.

Wawaruhusu Wananchi kutambua viongozi wa serikali za mitaa?.

Mtu mnamtuhumu kawaua ndugu zenu kina Mawazo,Ben Saanane,kawapiga risasi ndugu zenu,kawafunga viongozi wenu,na anawambia mjaribu hata kumwaga mkojo muone chamtema kuni.

Mnamtuhumu ananunua viongozi wenu,mliomba viongozi wa dini wawaombee maridhiano lakin aliwapuuza leo mnaenda hadharani kuomba maridhiano.

Kipindi nyie mnataka kuacha siasa za kiharakati mrudi kwenye siasa za Zitto kabwe, mnaemuomba msamaha yeye anafanya siasa za kiharakati bila kujali nyie mtamuonaje.

Maridhiano hayaombwi bali yataletwa na mawazo Kama ya ukuta ukuta.


Yetu waungwana macho, tunasubir tuone itakuwaje, muda huwa mwalimu mzuri.
 
Yaan kwakwel baada ya wachekeshaji WA Tanzania kuadimika nikajua sitakuwa najipatia raha tena ila mambo ya siasa za Tanzania yamenifanya nipate sehem ya kurefresh mwili wangu. Nachukulia siasa hizi Kama sehem ya starehe. Utamkuta mnafiki huyu kamsema mnafiki mwenzie kwa kufanya unafiki na kujipendekeza kwa mnafiki ambae anawafanyia unafiki. Yaani rahaa. Hahahahahaaa
 
RUSTEM PASHA, suala la Magufuli kuja kuwasema CHADEMA mbele ya safari ni kusubiri na kuona, but muhimu CDM wameonesha motive ya kutafuta maridhiano, kama yeye anavyopenda kujinasibu anamjua Mungu sasa ndio aoneshe kwa vitendo, vinginevyo akipuuzia halafu aendelee kumtaja Mungu kwenye shughuli zake, sijui atakuwa anamtaja mungu wa wapi!, na wastaarabu wote watakuwa wamejionea aina ya mtu alivyo.
 
Zito anaakili nyingi sanaa. Nakumbuka wakati Rais anahutubia bunge kwa mara ya kwanza wafuasi wa ukawa wote walitoka bungeni wakimuimba seif..seif..seif.. Kuwa amenyang'anywa urais Zanzibar. Zito alibaki ndani ya bunge na alisifiwa kuwa mwanasiasa mkomavu.

Wanaukawa walimuita msaliti na mnafiki kwa kuwa kinyume na wenzie. Leo seif aliyekuwa akipiganiwa na ukawa yupo kwa Zito na ACT imeenea Zanzibar. Sasa zito sio mnafiki tena na CDM wamegeuka kuwa wanafiki mbele ya zito na ACT yake.
 
Zitto ni mtu mbaya sana kwa ustawi wa Amani ya Tanzania

Huyu yupo tayari kuisaliti Nchi kwa ajili ya tumbo lake
 
Jicho la mbali,
Kinachowasumbua Chadema ni kesi ,
Wakijifanya wanapambana na jiwe jino kwa jino
Watakwenda kweli segedensa
Kuna mtu mkubwa kawashauri wajitafakari na kisha waungane na jiwe, katika kujenga nchi
Na jiwe atawaonea huruma na
kesi yao itafutwa kimya kimya..
Mtoto wa mjini ukiona maji mazito unatafuta chocholo..
 
Jicho la mbali,
Kinachowasumbua Chadema ni kesi ,
Wakijifanya wanapambana na jiwe jino kwa jino
Watakwenda kweli segedensa
Kuna mtu mkubwa kawashauri wajitafakari na kisha waungane na jiwe, katika kujenga nchi
Na jiwe atawaonea huruma na
kesi yao itafutwa kimya kimya..
Mtoto wa mjini ukiona maji mazito unatafuta chocholo..
Una pweinti!
 
Back
Top Bottom