Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

mbna yeye, siku ya ufunguzi wa bunge, alibaki ndani huku CDM wakitoka nje, hakuona ajabu, au akili zake hazikuwepo kipindi hicho?
Ndio maana alionekana mtu waajabu na mjinga, lakini wale waliotoka nao wanafanya yale ambayo tulikuwa tunayaona yakijinga, kwa nini nao tusiwaone hawana tofauti na Zitto ya ukasuku tu?.

Labda niulize tu Chadema wanaomba maridhiano ya nini?.

Waruhusiwe na Magufuli kufanya mikutano ya siasa?.

Wawaruhusu Wananchi kutambua viongozi wa serikali za mitaa?.

Maridhiano hayaombwi.
 
Haya tumekusikia kuhusu zitto! Turudi kwa Mhe Jiwe unaijua asili yake? Ukipata muda njoo kakonko uulizie mama biga , ! Mshkaji kachunga mbuzi saaana hapo kakonko!
 
Ni kweli kabisa lakini ujumbe ule wa kiinjili mbele watanzani wengi unaweza kumbadili mtu kuliko pambano la kivita. Pia hauzuii kuleta pambano ikiwa sikio la kufa halikusia dawa. Namuunga mkono Mbowe.
Kaika hali ile wanaopinga wangetaka Mbowe asemeje?
Wastaafu wakuu wote wanasifia mtawala na wananchi wanapokea. Kati ya na Mbowe wastaafu nani mkweli zaidi.
Na je, mbona hatusemi lolote kuhusu wao kuitakia nchi yote mema. Ina maana wanafurahia wapinzani kuonewa?
Mbowe yuko sahihi kuliko wote waliopewa nafasi ya kusema na ujumbe wake umefika japo wenye kiburi watakomaa
hawa watu hawajielewi, wanajidai kutaka jino kwa jino sijui kama wanajua maana ya huo msemo... wakiambiwa waingie barabarani tu shida!. hiyo jino kwa jino waitakayo sijui ya aina gani!
 
Hoja nyepesi sana. Kwamba yupo hivyo kisa baba ni mkongo na mama ni mrundi?
Sio nyepesi kihivyo kwa Zitto mwenyewe. Kama tuhuma hizi ni kweli na ikathibitika hakuzaliwa Tanzania, ndoto yake ya kugombea Urais wa Tanzania inaweza isifanikiwe.
 
mkuu bora ufanye effort kuyatafuta kuliko kusema waendeleze jino kwa jino, hivi wakiendeleza jino kwa jino unadhani ni nani atakaeumia, Mbowe au Magufuli!, watakaoumia ni wananchi wa kawaida, hili walilofanya CDM ni hekima iliyopitiliza. Tuliona Lowassa akiwaambia CDM 2015 wakubali matokeo, ile nayo ni hekima, Lowassa angesema wasikubali unadhani kingetokea nini na angeumia nani, ni mimi na wewe huku mtaani, tusijidanganye na jino kwa jino, hakuna anaependa vita aje kuona ndugu, jamaa, na marafiki zake wakiumia, haya mambo ni kuzungumza tu, hata akigoma kwa uamuzi mapenzi yake binafsi poa, hamna tatizo.
Penye kutafutwa maridhiano basi ujue kunawatu wameumia au kufa kabisa, pale ambapo watu wachini hasa walalahoi hawaumizwi moja kwa moja nawatawala basi utambue hakuna haja ya maridhiano.
 
Zitto hajawahi kupita majaribu wanayopitia CHADEMA, hajawahi kuwa na kesi kama wenzie! Jiulizeni anaongea mangapi na kwanini yeye hachukuliwi hatua! Zitto sio mtu kwa kuaminika kabisa la na shetani peke yake!
Mbowe hakujikomba alimpa raisi ukweli mtupu, na uliwaingia wote waliosikiliza! kwendaaaaaaaaaaaaaaa!
 
Back
Top Bottom