Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Nashangaaga sana CHADEMA kumuita Zitto mnafiki!!
 
kibokomchapaji,
mzee kwanza wacha bangi pili ni sherehe za UHURU wa nchi gani? maana kila siku munatwambia Tanganyika haipo. Tatu ivi wewe na akili zako za bangi wazungu watake kufanya fujo hapa Tz watakwenda kumtafuta zito. tano kwa taarifa yako wazungu wako poa kabisa na serikali hii ya kikatoliki kwasababu wana wacontrol waislam kwahivyo wewe usiwe na khofu ila kama unataka tu kufurahisha vijiwe vyenu vya gongo ni sawa.
 
Zitto yuko sahihi.

Wapinzani kwa sasa hawalijui lipi walitakalo.


Wasitarajie maradhiano kwa serikali hii inayoongozwa na jiwe.
Je ungekuwa ni wewe Mbowe unguwasilisha ujumbe vipi? ukianzia hapo ili tuone kama usingeingia mtego alionaswa nao Mbowe
 
Zitto buana.......,..kuna watu wanamuona shujaa kwa hizi mbwembwe ila soon atawaacha midomo wazi maana ni zaidi ya kinyonga
 
RUSTEM PASHA,
Mkuu mie kwa hili naona Mbowe yuko sahihi, ni miaka 4 imepita ambayo siasa za upinzani zimepitia shida kubwa na kwa uchaguzi ulivyokuwa ni proof kuwa mwakani hakuna hopes za mpinzani yeyote kurudi.

Sasa kwa muda uliobaki (miezi 10) suluhu ya kisiasa inatakiwa ili uchaguzi huru na haki uhakikishwe so maridhiano ni jambo jema kama upinzani watatala CCM isikilize maoni yao ila siasa za mapambano kwa mtu kama Rais wetu haziwezi saidia sababu ana ego so yuko tayari hata kuua waandamanaji wote kuprove nguvu yake na hyo itakuwa na faida gani kwa upinzani?

Hata wakiandamana wataundiwa kesi nyingine kama ya Akwilina na mwaka unao wote wataishia selo tu. So kama Violent option sio viable ni heri njia zote za kidiplomasia zitumike ili zikifeli basi watakuwa hawana la kupoteza wakianza siasa za kibabe kama ODM kenya.
 
Mimi Nipo na Zitto kwa mambo waliyofanyiwa CHADEMA na serikali hii ya awamu ya 5 ni kweli kitendo cha Mbowe kupanda jukwaani na kuomba maridhiano ni kujidhalilisha
 
Rais Mstaafu Kikwete ambaye sote tunajua yupo Marekani kwa majukumu muhimu ya kimataifa.
Kikwete hawezi kuhudhuria maana angepigwa za uso na magu,kuna jukumu kubwa la kitaifa zaidi ya kuhudhuria
 
MsemajiUkweli,

Natofautiana kidogo na wewe kumwona Zitto Kabwe kwa jicho hili....

Kwa maoni yangu wote wanataka kitu kimoja lakini kwa approach tofauti....

Zitto kwa mtazamo wake, anadhani njia hiyo anayoifikiria yeye, ndiyo the best approach kutatua mgogoro uliopo.....

Wenzake wa upande mwingine wanadhani meza ya mazungumzo ndiyo the best approach...

Wakati mwingine, approach zote mbili zinaweza kutumika...

Ya Zitto Kabwe Mara nyingi huwa ya mwisho baada ya meza ya mazungumzo (ndiyo hiki kinachoitwa maridhiano) kushindikana....

Ni jukumu letu wote kuamua tuzimalize kwa njia gani tofauti zetu za mitazamo ya kisiasa kwa sababu siasa ndiyo inayoamua maisha yetu ktk nyanja zote....

Tatizo ninaloliona mimi ni wenye madaraka na mamlaka ya kiserikali kuamini kuwa hicho kinachoitwa mgogoro wa kisiasa hakipo!!

Na kwamba kinachotafutwa na wanaoomba sisi kama jamaa kukaa meza moja "kuridhiana" si kuridhiana for real bali ni huu upande unaotaka hiyo kitu kutumia fursa hiyo kutaka kuharibu mikakati ya maendeleo ya wanaoongoza serikali na hivyo kufungua mlango wa kushindwa kwao kisiasa!!

Hapo ndipo lilipo tatizo yaani hakuna kuaminiana
 
For the first time Pascal nakuita ndumilakuwili.
Hivi huwezi kuona njia waliyotumia Chadema ni best calculation ever? Hawajaomba poo, bali wamemkumbusha Rais mbele ya Watanzania wote katika siku yao ya Uhuru, mbele ya mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa juu ya kufuata demokrasia na maridhiano tena kwa kauli ya kistarabu sana "unayo nafasi kubwa ya kuweka maridhiano ya kitaifa na historia ikakukumbuka".

Maneno mazito kabisa.

Hapo yasipo tekelezeka na nchi ikachafuka waweza kweli kutupa lawama kwa upinzani? Ushahidi mpaka kwa mabalozi utakuwa walionya na kutoa tahadhari, huko sio kuomba poo.

Siasa za kihuni anazoleta Zitto sio za nyakati hizi ukizingatia ubovu wa katiba na madaraka makubwa inayo mpa Rais. Eitha kutumia njia hiyo ya Mbowe au total battle ndio utaweza kuondoa utawala wa aina hii katika katiba hii.
Pascal Mayalla hivi kesho au kesho kutwa ukisikia " huko ulimwenguni" wamemtangaza Mbowe kuwa mshindi wa NOBEL utashangaa na kuwahoji kwa nini?
 
Zitto inawezekana kweli akawa mnafiki,lakini kwa haya aliyosema hayana unafiki. Wapinzani wote hasa hawa wakubwa kwa sasa wanafikiria nafasi zao za ubunge,maana kwa hali ilivyo Kuna uwezekano mwakani tukarudi kwenye mfumo wa chama kimoja.

Viongozi wa vijiji,mitaa na vitongoji walitii maelekezo ya hawa hawa waliojipendekeza jana,km wanaomba maridhiano leo wataomba pia uchaguzi wa serikali za mitaa urudiwe ili kutoa fursa kwa vyama vyote kushiriki!??
 
Egnecious, Zitto hana chochote, yeye siku zote ni mpingaji wa kila kitu. . .uzuri ni kwamba kila siku tunazidi kuelewa hizi harakati zake za kipumbavu. Na akika vibaya anguko lake litakuwa baya sana kisiasa
 
Ni Zitto huyu huyu wakati Lissu akiomba jumuiya za kimataifa ziingilie kati yeye alisema ni umazwazwa, nafikiri kipindi hicho alidhani Magufuli labda atakuwa 'mtamu' kwake japo kidogo.
 
Halafu mtoa mada unasema uhuru wa tanzania,kwanza rudi shule
 
Jino kwa jino ukiwa nyuma ya keyboard/keypad!

Tanzania kuna vituko!
Leo nakuunga mkono. Utafanyaje siasa ya jino kwa jino na serikali? Ambayo ina vyombo vyote vya dola na mamlaka? Hatua hiyo huwa ni ya mwisho kabisa baada ya kukaa mezani kukubaliana kutokubaliana huku mkiangalia Taifa lenu na sio vyama vyenu kwanza.

Maana yawezekana mie nikawa mpenzi kindaki ndaki wa Chadema, lakini nikurudi kijijini namkuta mama yangu humuambii kitu kuhusu ccm na ni mjumbe wa serikali ya kijiji kupitia ccm, jee nitamchukia? Au yeye atanikana kuwa sikutaki mwanangu mbona umenisaliti kwa kuwa Chadema? La hasha haiwezekani.

Nimesema jino kwa jino kuwa huwa ni hatua ya mwisho maana sisi Tanzania hatujafikia huko na Chadema imeona hali hii ya kususiana uchaguzi na sasa fujo za kuwakataa wenyeviti walio penyezwa ndio inatupeleka huko basi maridhiano yafanyike maana sio kuwa ccm ndiyo pekee inayokosea bali hata upinzani (Chadema) nao wanakosea, wazungumze, wafanye siasa na kukubaliana bila kuumizana.

Mazungumzo yana sababisha sumu kupungua mwilini, hiyo Zitto hakuna anayemzuia na hilo jino lake pengine ndivyo alivyofundishwa na mshauri wake mpya.
IMG_20191209_200625.jpeg
 
Back
Top Bottom