Walichofanya cdm jana, nawaza angekifanya Zitto ingekuwaje?.
Walichofanya Cdm jana ndio alikuwa anakifanya Zitto nyakati za Kikwete akaitwa mnafiki, leo nisahihi kabisa Zitto kuwaita wanafiki Chadema maana waliyokuwa wanamtuhumu nayo, ndio wameanza kuyafanya.
Kamwe mwenye nguvu haombwi maridhiano, bali mwenye nguvu ndio huomba maridhiano pindi anapoona nguvu zake zinataka kupunguzwa na wafuasi wavyama vingine.
Chadema jana mmejidhalilisha na naamini JPM hatawapa nafasi ya maridhiano bali atawananga kwenye mikutano yake ijayo.
Inawezekana mlikuwa na lengo zuri, lkn sikwawakati huu baada yakususia uchanguzi wa vitongoji na vijiji.
Labda niulize tu Chadema wanaomba maridhiano ya nini?.
Waruhusiwe na Magufuli kufanya mikutano ya siasa?.
Wawaruhusu Wananchi kutambua viongozi wa serikali za mitaa?.
Mtu mnamtuhumu kawaua ndugu zenu kina Mawazo,Ben Saanane,kawapiga risasi ndugu zenu,kawafunga viongozi wenu,na anawambia mjaribu hata kumwaga mkojo muone chamtema kuni.
Mnamtuhumu ananunua viongozi wenu,mliomba viongozi wa dini wawaombee maridhiano lakin aliwapuuza leo mnaenda hadharani kuomba maridhiano.
Kipindi nyie mnataka kuacha siasa za kiharakati mrudi kwenye siasa za Zitto kabwe, mnaemuomba msamaha yeye anafanya siasa za kiharakati bila kujali nyie mtamuonaje.
Maridhiano hayaombwi bali yataletwa na mawazo Kama ya ukuta ukuta.
Yetu waungwana macho, tunasubir tuone itakuwaje, muda huwa mwalimu mzuri.