Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe amewashutumu viongozi wa upinzani walioenda kwenye sherehe za uhuru, Mwanza na kupanda jukwaani kuomba maridhiano ya kisiasa kwa Rais Magufuli.

Ametoa shutuma hizo kupitia mitandao ya kijamii akidai walichofanya ni kujipendekeza kwa Rais ili waachiwe nafasi chache za ubunge mwaka 2020 huku wakiwaacha njia panda wanachama wa vyama vyao waliowaambia wajitoe kwenye chaguzi za serikali za mitaa.

Zitto ameenda mbali zaidi na kudai kinachohitajika kwa sasa Tanzania Bara ni siasa kali kama zilizofanywa na wapinzani huko Zanzibar mwaka 2001 ambako kulipelekea CCM kutaka maridhiano (ametumia neno kuomba poo).

Amemaliza kwa kusema, maridhiano hayaombwi bali yanadaiwa.

====
Hoja za wadau
Wachumia tumbo wa Lumumba mnaumia sana kuona Chadema wanataka maridhiano. Mumejaa ushetani tupu na ubinafsi
 
Mbowe ni mnafiki sana hili liko wazi, kasusia uchaguzi , CCM wakachukua ushindi wa 99% tena na vijembe juu vya Polepole , leo eti unaomba nao maridhiano huu ni ujinga mkubwa , yaani mtu akufanyie ubaya tena wala samahani asikuombe , wewe uliofanyiwa ubaya ndio utoke kuomba samahani , nakwambia chadema imekubali kuwa kibaraka wa CCM , huu ni ukweli mchungu kabisa
Hivi mnataka kusiwe Na maridhiano ili kuwe Na nn? Nimeamini watanzania wengi sio wazalendo
 
Hivi msimamo wa Zitto Kabwe ndio msimamo wa ACTwazalendo? kama ndio basi akina Maalim wataburuzwa sana
Maalim anatakiwa ashtuke haraka kabla ya kung'amua kuwa amejiunga na chama cha kwenye Briefcase na Instagram hatari sana
 
Hivi msimamo wa Zitto Kabwe ndio msimamo wa ACTwazalendo? kama ndio basi akina Maalim wataburuzwa sana
Maalim anatakiwa ashtuke haraka kabla ya kung'amua kuwa amejiunga na chama cha kwenye Briefcase hatari sana
Vipi ndani ya CHADEMA kuna wa kupinga msimamo wa Mbowe.?
 
Vipi ndani ya CHADEMA kuna wa kupinga msimamo wa Mbowe.?
Kamati kuu ilikaa na kuamua kuwepo na maridhiano kwa hiyo maridhiano ni msimamo wa chama tofauti na Zitto ambaye matamko yake ya Instagram ndio (ninavyofikiria mimi) msimamo rasmi wa ACTwazalendo.
Hebu angalia tofauti kati ya Chadema na Actwazalendo
 
Kwa hiyo kamati kuu ndio ilikaa na kuamua kuwapigia simu CCM na kuomba maridhiano.?

Pamoja na kufanyiwa umafia kwenye uchaguzi serikali za mitaa bado mmewapigia simu na kuomba maridhiano.?
 
Kwa hiyo kamati kuu ndio ilikaa na kuamua kuwapigia simu CCM na kuomba maridhiano.?

Pamoja na kufanyiwa umafia kwenye uchaguzi serikali za mitaa bado mmewapigia simu na kuomba maridhiano.?
Je kama ndio njia ya mwisho kabla ya kuingia msituni mwishoni nchi ikisha angamia ndio tutawaambia kuwa... look tulijaribu kila njia mkajimwambafy.
 
Kwa hiyo kamati kuu ndio ilikaa na kuamua kuwapigia simu CCM na kuomba maridhiano.?

Pamoja na kufanyiwa umafia kwenye uchaguzi serikali za mitaa bado mmewapigia simu na kuomba maridhiano.?
Mkuu siku zinavyokwenda ndiyo unazidisha upopoma,kama vipi mfuate huyo jamaa yako huko Sweden.
 
Kwa hiyo kamati kuu ndio ilikaa na kuamua kuwapigia simu CCM na kuomba maridhiano.?

Pamoja na kufanyiwa umafia kwenye uchaguzi serikali za mitaa bado mmewapigia simu na kuomba maridhiano.?
Umafia hata kwa baba wa demokrasia upo. Watanzania tufunguke akili.
 
Back
Top Bottom