Zitto Kabwe: Mkopo wa Benki ya Dunia kuboresha elimu, Serikali ililenga kuinufaisha CCM kwa kununua vyuo vilivyo chini ya chama hicho

Zitto Kabwe: Mkopo wa Benki ya Dunia kuboresha elimu, Serikali ililenga kuinufaisha CCM kwa kununua vyuo vilivyo chini ya chama hicho

Acheni kumlilia Zitto. Hii ni nchi tajiri, kwanini tusijenge kwa pesa zetu na tunalazimisha mkopo?

Mwambieni Meko aache kuropoka kwani ndiko kunakotucost watanzania. Nyambaaf!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaogopa CCM inaweza kuwa inajaribu kiujanja kuvipiga mnada kupata pesa za kampeni.

Si unajua wale wafadhili wa CCM siku hizi wanaitwa mafisadi. Na wengi wametumbuliwa.

Na mwaka huu hufadhili wa Tsheti na kanga na makofia utatoka wapi.

So zitto ana wivu wa kisiasa tu. kwamba CCM watafaidi na kuwa na fedha za kampeni.wakati ACT wanahangaika huko uarabuni kuomba misaada.
 
Zitto Kabwe amezuia ujenzi wa madarasa 1000, maabara na nyumba za walimu kwa madai kuwa CCM wanataka kuiuzia serikali vyuo vyake ili vibadilishwe kuwa shule za serikali.

Ndiposa namuuliza Zitto, Je kuna ubaya gani CCM kuiuzia serikali vyuo vyake kama ni kweli wana hiyo nia?!

cc: Chakaza, Pascal Mayalla, Tindo

Maendeleo hayana vyama!
WARUDISHE NA VIWANJA VYA MPIRA
 
Tanzania ikinyimwa huo mkopo nyinyi na chama chenu mnafaidika nini? Hao watoto ambao hela hizi zilikuwa zikawasaidie watafaidika nini na hio 3-0 ya Zitto?!

ID ya chama kabisa inakuja kuleta ushabiki maandazi JF.
Kwani wewe hujui kuwa watu wa CCM wanajua kusoma na kuandika ila wapinzani hawajui kusoma na kuandika? Inamaana kuna Shule za wapinzani na Shule za CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
katafuteni nchi yenu akufanyia ujinga wenu nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa sheria na katiba mtaongea sana lakini hamuwezi kushindana na sisi
Inaonekana wazi hata hiyo katiba huijui.Lugola amehujumu uchumi wa nchi ila yupo nje anakula bata,akina kabendera wamehujumu uchumi wa nchi ila wapo mahabusu na upelelezi unaendelea.Hapo hiyo katiba na Sheria vipo wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh Zitto mbunge wa kigoma mjini ameiambia BBC kuwa mkopo huo ulikuwa katika masilahi ya uchaguzi wa mwaka huu 2020 na sio elimu kwa maana katika shule zilizo orodheshwa zote sio mpya

Chanzo: BBC SWAHILI

. Zitto bila hofu azungumza mazito/ Ni kweli nliomba wa nyimwe mkopo huo


Sent using Jamii Forums mobile app

Hayo mambo ya kwamba mkopo huo utapelekwa kunufaisha CCM uchaguzi ujao ana ushahidi nayo au hisia tu?
 
Zito yuko sahihi na analipenda taifa maana anasaidia deni la taifa at least lisipae sana .


Halafu mbona huku kwetu tunaambiwa tz ni nchi tajiri au tunapigwa chenga ya siasa?

Sent from my TECNO WX3 using Tapatalk
 
Mkuu ni ubinafsi tu unawasumbua.
Hizo shule anazoita za CCM wanasoma watoto wa wanachama wa chama chochote.

Hapo Zitto ametanguliza maslahi yake binafsi, amewaza uchaguzi zaidi kuliko watanzania maskini.
Siasa za namna hii ni hatari sana kwa taifa, watanzania sio wajinga kiasi hicho.

Nimemkubali sana Mh. Mbowe alipojaribu kutafuta maridhiano, muafaka na serikali siku ya Uhuru, aliweka pembeni maslahi binafsi.
Zitto atakuja kulipia tu huu usaliti na ubinafsi wake hata kama Magufuli atakapokuwa hayupo madarakani.
Hizi video na nyaraka za harakati zake zitakuwepo daima hapa duniani na zitakuja kumhukumu yeye mwenyewe.
Ogopa hii teknolojia, ni kama alivyo mpondea Lissu kuomba Tanzania isitishiwe misaada na Jumuiya za kimataifa na yeye anafanya kile alichomkosoa Lissu na kukiita 'UMAZWAZWA'.
Leo zile comments zimerejea kwa kasi mitandaoni kwa kumdhihaki.
Mwa
Duh! Kwani WB wanesema wameinyima TZ huo mkopo? Soma na sikiliza kwanza uelewe ndiyo uje kutoa povo lako hapa kama upo umuhimu wa kulitoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Whatever the case mambo mengine ni upoyoyo. Hivi ni nchi gani inapeleka
Maneno ya mwalimu yanasimama. Mtu ukizoea kila nyama ya mtu huachi .Zitto ni msaliti by nature. Pepo mahajimuni lililosaliti akiwa Chadema ndo bado linamtafuna mpaka leo. Kwa akili yake ya huko anakotoka alidhqni ni siri na sasa huko aliko kamqsi linamtoka utadhani kafakamiwa Nan corona
 
Barua niliyoandika Benki ya Dunia ni hii. Nipo tayari kulipa gharama yeyote kwa kuandika Barua hii. Serikali ya Rais Magufuli inapaswa kujua, naikumbusha tena, kuwa SIOGOPI lolote katika lile ninaloamini.

Nataka kila Mtoto wa kike wa Tanzania awe na haki sawa ya kupata Elimu - apate Mimba ama asipate mimba. CCM waliahidi kwenye Ilani yao kuwa watoto waliopata uja uzito Wataendelea na Masomo. CHADEMA wanaamini hivyo na Act Wazalendo tunaamini hivyo.

Makamu wa Rais Bi. Samiah Suluh amenukuliwa akiamini hivyo na Waziri wa Afya pia. Wizara ya Elimu ilitunga mpaka mwongozo wa kuwezesha hilo.

Ni Rais Magufuli tu ndio hataki watoto wa kike warudi shuleni. Hii Nchi sio ya Magufuli peke yake. Hatuwezi kukaa kimya kumwona mtu mmoja analazimisha imani zake kwa Jamii nzima ya Watanzania.

Hongera nyingi kwa Watanzania waliohakikisha kuwa tunasubirisha Mkopo wa Benki ya Dunia mpaka hapo utakapoboreshwa na kutoa nafasi kwa watoto wa kike kupata Elimu bila ubaguzi wala unyanyapaa.

=======
BARUA KWENDA BENKI YA DUNIA KWA KISWAHILI:
=======

Januari 22, 2020.

Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia,
1818 H Street
Washington, DC
20433

Wapendwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia,

YAH: MKOPO WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 500 KWA AJILI YA MRADI WA UBORESHAJI WA ELIMU YA SEKONDARI NCHINI TANZANIA

Jina langu naitwa Zitto Kabwe, ni Mbunge kutoka Manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania.

Ninawaandikia barua hii kuhusu kikao cha Bodi cha tarehe 28 Januari 2020, kikao ambacho Bodi itajadili mkopo wa Tanzania kiasi cha Dola za kimarekani milioni 500 kwa ajili ya Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari Tanzania.

Katika barua yangu kwenu ya tarehe 9 mwezi Septemba, niliwakumbusha kuhusu hali mbaya ya masuala ya haki za kijinsia na kibinadamu nchini mwangu. Kwa masikitiko, inaonekana kwamba hatua ya Benki ya Dunia kuidhinisha fedha za mradi ujulikanao kama "Productive Social Safety Net" mwezi Septemba iliitia makucha serikali hii. Kwa hakika, hali imekuwa mbaya mno. Mwanahabari Erick Kabendera bado anasota rumande, vyama vya siasa havina ruhusa ya kufanya mikutano ya hadhara, nao mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar ukiwa umevurugwa hali inayopelekea majaliwa ya uchaguzi mkuu wa 2020 kukosa maana.

Ni wiki iliyopita tu, vikosi vya usalama vilinizuia mimi kufanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wapigakura wangu. Vikwazo vya jinsi hii wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Novemba mwaka jana, vilitawala kwa vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano isipokuwa chama tawala pekee, chama cha mapinduzi. Wakati wa uchaguzi huo wa Novemba, chama cha mapinduzi kiliwazuia zaidi ya wagombea 400,000 wa vyama vya upinzani wasigombeaa nafasi za uongozi kwa kuwa tu walionekana wasiokubaliana na matakwa ya serikali hii. Matokeo yake, takribani vyama vyote viliususia uchaguzi huo na kupelekea asilimia 99.6 ya viti vilivyokuwa vikigombewa kunyakuliwa na chama tawala.

Nazo fursa haba za kiuwajibikaji wa kikatiba zilizokuwa zimesalia kama vile uwepo wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nazo zimehujumiwa, kwani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amefukuzwa kutoka ofisini kinyume cha Katiba mwezi Novemba mwaka jana, hali inayoweka rehani usalama wa fedha za walipakodi na uwekezaji wa benki yenu. Mwaka 2020 tunatarajia kufanya uchaguzi mkuu ambao tunaona dalili zote kwamba utavurugwa na kuharibiwa na chama tawala ili kujihakikishia ushindi wa bwelele.

Serikali hii haina tena usafi wa kujidai kuwa serikali inayowakilisha maslahi ya watu wa Tanzania, isipokuwa inajali na kulinda maslahi ya wachache. Jambo la kusikitisha ni kwamba, si hiki kikundi kidogo cha watawala wa sasa bali ni watanzania hawa kwa wingi wao ndio ambao watalazimika baadaye kulipia mkopo huu. Kubwa zaidi, hofu yetu ni kwamba kutokana na ukosefu wa misingi ya uwajibikaji, malengo ya uwekezaji wa fedha hizi yatatumiwa vibaya na chama tawala kujinufaisha kisiasa na kuharibu mchakato wa uchaguzi.

Kwa mantiki hiyo, ninakuombeni msimamishe utolewaji wa fedha hizo kwa serikali hii mpaka pale misingi ya uwajibikaji itakaporejeshwa Tanzania. Misingi hii ya uwajibikaji ninayoizungumzia ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kukusanyika, chaguzi huru na za haki, sanjali na kumrejesha ofisini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mnamo tarehe 3-8 mwezi Februari, nitakuwa Washington DC. Nitafurahi kukutana nanyi tuweze kutazama kwa yakini namna ambavyo mchango wa Benki ya Dunia unaweza kuwa wenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu.

Ni imani yangu kuwa tutapata wasaa mzuri kujadiliana.

Wenu,

Zitto Z. Kabwe,
Mbunge,
Jimbo la Kigoma ujiji,
Kiongozi wa Chama, Alliance for Change and Transparency.


Nb: Barua hii iliandikwa katika lugha ya Kiingereza. Imetafsiriwa katika Kiswahili na Vicent Kassala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom