Zitto Kabwe: Mkopo wa Benki ya Dunia kuboresha elimu, Serikali ililenga kuinufaisha CCM kwa kununua vyuo vilivyo chini ya chama hicho

Barua niliyoandika Benki ya Dunia ni hii. Nipo tayari kulipa gharama yeyote kwa kuandika Barua hii. Serikali ya Rais Magufuli inapaswa kujua, naikumbusha tena, kuwa SIOGOPI lolote katika lile ninaloamini. Nataka kila Mtoto wa kike wa Tanzania awe na haki sawa ya kupata Elimu - apate Mimba ama asipate mimba. CCM waliahidi kwenye Ilani yao kuwa watoto waliopata uja uzito Wataendelea na Masomo. CHADEMA wanaamini hivyo na Act Wazalendo tunaamini hivyo. Makamu wa Rais Bi. Samiah Suluh amenukuliwa akiamini hivyo na Waziri wa Afya pia. Wizara ya Elimu ilitunga mpaka mwongozo wa kuwezesha hilo. Ni Rais Magufuli tu ndio hataki watoto wa kike warudi shuleni. Hii Nchi sio ya Magufuli peke yake. Hatuwezi kukaa kimya kumwona mtu mmoja analazimisha imani zake kwa Jamii nzima ya Watanzania.

Hongera nyingi kwa Watanzania waliohakikisha kuwa tunasubirisha Mkopo wa Benki ya Dunia mpaka hapo utakapoboreshwa na kutoa nafasi kwa watoto wa kike kupata Elimu bila ubaguzi wala unyanyapaa.

.......

Januari 22, 2020.

Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia,
1818 H Street
Washington, DC
20433

Wapendwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia,

YAH: MKOPO WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 500 KWA AJILI YA MRADI WA UBORESHAJI WA ELIMU YA SEKONDARI NCHINI TANZANIA

Jina langu naitwa Zitto Kabwe, ni Mbunge kutoka Manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania.

Ninawaandikia barua hii kuhusu kikao cha Bodi cha tarehe 28 Januari 2020, kikao ambacho Bodi itajadili mkopo wa Tanzania kiasi cha Dola za kimarekani milioni 500 kwa ajili ya Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari Tanzania.

Katika barua yangu kwenu ya tarehe 9 mwezi Septemba, niliwakumbusha kuhusu hali mbaya ya masuala ya haki za kijinsia na kibinadamu nchini mwangu. Kwa masikitiko, inaonekana kwamba hatua ya Benki ya Dunia kuidhinisha fedha za mradi ujulikanao kama "Productive Social Safety Net" mwezi Septemba iliitia makucha serikali hii. Kwa hakika, hali imekuwa mbaya mno. Mwanahabari Erick Kabendera bado anasota rumande, vyama vya siasa havina ruhusa ya kufanya mikutano ya hadhara, nao mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar ukiwa umevurugwa hali inayopelekea majaliwa ya uchaguzi mkuu wa 2020 kukosa maana.

Ni wiki iliyopita tu, vikosi vya usalama vilinizuia mimi kufanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wapigakura wangu. Vikwazo vya jinsi hii wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Novemba mwaka jana, vilitawala kwa vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano isipokuwa chama tawala pekee, chama cha mapinduzi. Wakati wa uchaguzi huo wa Novemba, chama cha mapinduzi kiliwazuia zaidi ya wagombea 400,000 wa vyama vya upinzani wasigombeaa nafasi za uongozi kwa kuwa tu walionekana wasiokubaliana na matakwa ya serikali hii. Matokeo yake, takribani vyama vyote viliususia uchaguzi huo na kupelekea asilimia 99.6 ya viti vilivyokuwa vikigombewa kunyakuliwa na chama tawala.

Nazo fursa haba za kiuwajibikaji wa kikatiba zilizokuwa zimesalia kama vile uwepo wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nazo zimehujumiwa, kwani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amefukuzwa kutoka ofisini kinyume cha Katiba mwezi Novemba mwaka jana, hali inayoweka rehani usalama wa fedha za walipakodi na uwekezaji wa benki yenu. Mwaka 2020 tunatarajia kufanya uchaguzi mkuu ambao tunaona dalili zote kwamba utavurugwa na kuharibiwa na chama tawala ili kujihakikishia ushindi wa bwelele.

Serikali hii haina tena usafi wa kujidai kuwa serikali inayowakilisha maslahi ya watu wa Tanzania, isipokuwa inajali na kulinda maslahi ya wachache. Jambo la kusikitisha ni kwamba, si hiki kikundi kidogo cha watawala wa sasa bali ni watanzania hawa kwa wingi wao ndio ambao watalazimika baadaye kulipia mkopo huu. Kubwa zaidi, hofu yetu ni kwamba kutokana na ukosefu wa misingi ya uwajibikaji, malengo ya uwekezaji wa fedha hizi yatatumiwa vibaya na chama tawala kujinufaisha kisiasa na kuharibu mchakato wa uchaguzi.

Kwa mantiki hiyo, ninakuombeni msimamishe utolewaji wa fedha hizo kwa serikali hii mpaka pale misingi ya uwajibikaji itakaporejeshwa Tanzania. Misingi hii ya uwajibikaji ninayoizungumzia ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kukusanyika, chaguzi huru na za haki, sanjali na kumrejesha ofisini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mnamo tarehe 3-8 mwezi Februari, nitakuwa Washington DC. Nitafurahi kukutana nanyi tuweze kutazama kwa yakini namna ambavyo mchango wa Benki ya Dunia unaweza kuwa wenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu.

Ni imani yangu kuwa tutapata wasaa mzuri kujadiliana.

Wenu,

Zitto Z. Kabwe,
Mbunge,
Jimbo la Kigoma ujiji,
Kiongozi wa Chama, Alliance for Change and Transparency.

Nb: Barua hii iliandikwa katika lugha ya Kiingereza. Imetafsiriwa katika Kiswahili na Vicent Kassala.

Sent using Jamii Forums mobile app
No fear,no hate.
Watu jasiri kama hawa wanahitajika sasa kuliko wakati mwingine. Hongera kwa mbiu.
 
Mie napita naelekea mbinguni kwa mbele

Sent from my SM-P585 using Tapatalk
 
JITU MOJA LIMEWAHI KUSEMA HAYA CHINI

Ndugu zangu niwaambie ukweli tena ukweli mtupu nchi yetu ni tajiri sana sisi sio maskini kila siku tunaombaomba tumechokwa tunataka ifike hatuwa wao ndio watuombe tena ikiwezekana na mitumba tuwauzie wao huu ndio ukweli usiopingika sio maneno yangu.....
 
Hivi huyu Zitto si ndo aliyeenda kwa mabeberu kushinikiza kuzuia mradi wa Bonde la Nyerere (Stiglars Gorge) usianze? Je alifanikiwa? Mradi si unaendelea? Kelele za chura hazizuii chura kunywa maji! Hao wanafunzi wapenda ngono na kuzaliana shuleni akaanzishe shule yake akawasomeshe! Hatujakataza NGO na shule binafsi kusomesha wazazi! Tumekataa shule za umma zinazoendeshwa kwa kodi za wananchi kushabikia ngono mashuleni kuzaliana na kuruhusiwa kuendelea! Zitto na mabeberu wanaokussuport anzisheni hizo shule si tu za kusomesha wazazi lakini pia za kusomesha mashoga! Prof. Assad tayari kaishatumbuliwa na tumeishamsahau!
 
Kwa mantiki hiyo, ninakuombeni msimamishe utolewaji wa fedha hizo kwa serikali hii mpaka pale misingi ya uwajibikaji itakaporejeshwa Tanzania. Misingi hii ya uwajibikaji ninayoizungumzia ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kukusanyika, chaguzi huru na za haki, sanjali na kumrejesha ofisini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Wale wote wanaomponda Zitto na kumuita Msaliti, wamejitia upofu na hawataki kusoma wala kusikia chochote kuhusu hii paragraph
 
Hongera Zitto,
CCM kama mna hoja za msingi jibuni au andikeni barua na nyinyi za kutetea,

Mipasho na maneno ya Kanga ndio yanawafanya muonekane hamjielewi,

Andikeni hoja nzito kujibu hizo tuhuma hapo,acheni kumshambulia mtu binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom