Zitto Kabwe: Mkopo wa Benki ya Dunia kuboresha elimu, Serikali ililenga kuinufaisha CCM kwa kununua vyuo vilivyo chini ya chama hicho

Zitto Kabwe: Mkopo wa Benki ya Dunia kuboresha elimu, Serikali ililenga kuinufaisha CCM kwa kununua vyuo vilivyo chini ya chama hicho

Serikali inapata wapi hela kama siyo kodi kutoka kwa wananchi wake wote?
Serikali Ina vyanzo vingi, mirabaha ya madini makusanyo ya maduhuli tozo za mbugani na bandarini, huyu mja mzito anasubiri kujifungua bure na kusomeshewa bure hawezi lips hats Mia ya mkopo
 
Hivi hili suala la mjamzito kutorudi shule kwani lomeanza awamu hii?

Mbona miaka yote ipo hivyo, haikuwahi kupingwa na kushadadiwa kama hivi karibuni. Au kisa JPM alitilia mkazo?

Ingekuwa ni haki za watoto wa kike, basi wangeipinga toka zamani. Vinginevyo ni kulifanya mtaji wa kisiasa jambo hili.

Toka Mkapa yupo mdarakani, naju hii sheria ipo na mjamzito harudishwi akijifungua. Ila sikuwahi kuona upinzani wakiisema hii. na hata alipokuja mkwere mambo yalikuwa ni hivyohivyo...... Ila kuja kutiliwa mkazo na JPM imekuwa ndiyo jambo la kufanyia siasa.
 
Mwa
Whatever the case mambo mengine ni upoyoyo. Hivi ni nchi gani inapeleka
Maneno ya mwalimu yanasimama. Mtu ukizoea kila nyama ya mtu huachi .Zitto ni msaliti by nature. Pepo mahajimuni lililosaliti akiwa Chadema ndo bado linamtafuna mpaka leo. Kwa akili yake ya huko anakotoka alidhqni ni siri na sasa huko aliko kamqsi linamtoka utadhani kafakamiwa Nan corona
Hivi kile kisiwa Cha mafia nyerere alikokuwa anawaficha bado kipo?
 
hivi hao WB wametoa majibu gani tokea wapokee barua ya Zitto?
 
Muhtasari,

Zitto Kabwe kaomba mkopo wa trilioni usitishwe kwa sababu hizi,

  • Mwanahabari Erick Kabendera bado anasota rumande
  • vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano isipokuwa chama tawala pekee,
  • mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar ukiwa umevurugwa
  • kuwazuia zaidi ya wagombea 400,000 wa vyama vya upinzani wasigombeaa nafasi za uongozi
  • C.A.G kufukuzwa kutoka ofisini kinyume cha Katiba mwezi Novemba
  • uchaguzi mkuu 2020 kuwa na dalili utavurugwa na kuharibiwa
  • fedha za mkopo uliokataliwa zingetumika kinyume na lengo (ufisadi)
  • watanzania kulazimika baadaye kulipia mkopo huu
Binafsi Nadhani angewasilisha bungeni hoja hizi ili zijadiliwe kama zina uzito au la, ukweli au la, n.k

Bunge lipi, hili ambalo liko kashabiki na kujikita kwenye kuwakomoa wapinzani zaidi? Wote tunaona kinachoendelea hivi sasa hapa nchini dhidi ya wapinzani, je ni hoja ipi ingejadiliwa hapo? Uchaguzi juzi umevurugwa na cdm jana wameomba uchaguzi huo urudiwe lakini serikali imegoma. Kwanini Zito asichukue hatua stahiki huko nje? Kama humu ndani hatusukilizwi acha twende nje tukapate msaada wa nchi za nje.
 
Hivi hili suala la mjamzito kutorudi shule kwani lomeanza awamu hii?
JPM alituahidi kuwa watarudi shule na watapata haki sawa kama wengine na lipo kwenye ilani yao. Sasa mbona anatuacha solombe na ahadi hii...? Tudai ahadi yetu, tumpinge.
 
Barua niliyoandika Benki ya Dunia ni hii. Nipo tayari kulipa gharama yeyote kwa kuandika Barua hii. Serikali ya Rais Magufuli inapaswa kujua, naikumbusha tena, kuwa SIOGOPI lolote katika lile ninaloamini.

Nataka kila Mtoto wa kike wa Tanzania awe na haki sawa ya kupata Elimu - apate Mimba ama asipate mimba. CCM waliahidi kwenye Ilani yao kuwa watoto waliopata uja uzito Wataendelea na Masomo. CHADEMA wanaamini hivyo na Act Wazalendo tunaamini hivyo.

Makamu wa Rais Bi. Samiah Suluh amenukuliwa akiamini hivyo na Waziri wa Afya pia. Wizara ya Elimu ilitunga mpaka mwongozo wa kuwezesha hilo.

Ni Rais Magufuli tu ndio hataki watoto wa kike warudi shuleni. Hii Nchi sio ya Magufuli peke yake. Hatuwezi kukaa kimya kumwona mtu mmoja analazimisha imani zake kwa Jamii nzima ya Watanzania.

Hongera nyingi kwa Watanzania waliohakikisha kuwa tunasubirisha Mkopo wa Benki ya Dunia mpaka hapo utakapoboreshwa na kutoa nafasi kwa watoto wa kike kupata Elimu bila ubaguzi wala unyanyapaa.

=======
BARUA KWENDA BENKI YA DUNIA KWA KISWAHILI:
=======

Januari 22, 2020.

Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia,
1818 H Street
Washington, DC
20433

Wapendwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia,

YAH: MKOPO WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 500 KWA AJILI YA MRADI WA UBORESHAJI WA ELIMU YA SEKONDARI NCHINI TANZANIA

Jina langu naitwa Zitto Kabwe, ni Mbunge kutoka Manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania.

Ninawaandikia barua hii kuhusu kikao cha Bodi cha tarehe 28 Januari 2020, kikao ambacho Bodi itajadili mkopo wa Tanzania kiasi cha Dola za kimarekani milioni 500 kwa ajili ya Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari Tanzania.

Katika barua yangu kwenu ya tarehe 9 mwezi Septemba, niliwakumbusha kuhusu hali mbaya ya masuala ya haki za kijinsia na kibinadamu nchini mwangu. Kwa masikitiko, inaonekana kwamba hatua ya Benki ya Dunia kuidhinisha fedha za mradi ujulikanao kama "Productive Social Safety Net" mwezi Septemba iliitia makucha serikali hii. Kwa hakika, hali imekuwa mbaya mno. Mwanahabari Erick Kabendera bado anasota rumande, vyama vya siasa havina ruhusa ya kufanya mikutano ya hadhara, nao mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar ukiwa umevurugwa hali inayopelekea majaliwa ya uchaguzi mkuu wa 2020 kukosa maana.

Ni wiki iliyopita tu, vikosi vya usalama vilinizuia mimi kufanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wapigakura wangu. Vikwazo vya jinsi hii wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Novemba mwaka jana, vilitawala kwa vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano isipokuwa chama tawala pekee, chama cha mapinduzi. Wakati wa uchaguzi huo wa Novemba, chama cha mapinduzi kiliwazuia zaidi ya wagombea 400,000 wa vyama vya upinzani wasigombeaa nafasi za uongozi kwa kuwa tu walionekana wasiokubaliana na matakwa ya serikali hii. Matokeo yake, takribani vyama vyote viliususia uchaguzi huo na kupelekea asilimia 99.6 ya viti vilivyokuwa vikigombewa kunyakuliwa na chama tawala.

Nazo fursa haba za kiuwajibikaji wa kikatiba zilizokuwa zimesalia kama vile uwepo wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nazo zimehujumiwa, kwani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amefukuzwa kutoka ofisini kinyume cha Katiba mwezi Novemba mwaka jana, hali inayoweka rehani usalama wa fedha za walipakodi na uwekezaji wa benki yenu. Mwaka 2020 tunatarajia kufanya uchaguzi mkuu ambao tunaona dalili zote kwamba utavurugwa na kuharibiwa na chama tawala ili kujihakikishia ushindi wa bwelele.

Serikali hii haina tena usafi wa kujidai kuwa serikali inayowakilisha maslahi ya watu wa Tanzania, isipokuwa inajali na kulinda maslahi ya wachache. Jambo la kusikitisha ni kwamba, si hiki kikundi kidogo cha watawala wa sasa bali ni watanzania hawa kwa wingi wao ndio ambao watalazimika baadaye kulipia mkopo huu. Kubwa zaidi, hofu yetu ni kwamba kutokana na ukosefu wa misingi ya uwajibikaji, malengo ya uwekezaji wa fedha hizi yatatumiwa vibaya na chama tawala kujinufaisha kisiasa na kuharibu mchakato wa uchaguzi.

Kwa mantiki hiyo, ninakuombeni msimamishe utolewaji wa fedha hizo kwa serikali hii mpaka pale misingi ya uwajibikaji itakaporejeshwa Tanzania. Misingi hii ya uwajibikaji ninayoizungumzia ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kukusanyika, chaguzi huru na za haki, sanjali na kumrejesha ofisini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mnamo tarehe 3-8 mwezi Februari, nitakuwa Washington DC. Nitafurahi kukutana nanyi tuweze kutazama kwa yakini namna ambavyo mchango wa Benki ya Dunia unaweza kuwa wenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu.

Ni imani yangu kuwa tutapata wasaa mzuri kujadiliana.

Wenu,

Zitto Z. Kabwe,
Mbunge,
Jimbo la Kigoma ujiji,
Kiongozi wa Chama, Alliance for Change and Transparency.


Nb: Barua hii iliandikwa katika lugha ya Kiingereza. Imetafsiriwa katika Kiswahili na Vicent Kassala.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamani aliyeona kipengele cha mimba anisaidie?

Pili tunaombeni na barua ya kingereza tuisome tuone maana kiswahili bwana hakieleweki barabara na bara bara eti ni tofauti
 
Nataka kila Mtoto wa kike wa Tanzania awe na haki sawa ya kupata Elimu - CCM waliahidi kwenye Ilani yao kuwa watoto waliopata uja uzito Wataendelea na Masomo.
Makamu wa Rais Bi. Samiah Suluh amenukuliwa akiamini hivyo na Waziri wa Afya pia. Wizara ya Elimu ilitunga mpaka mwongozo wa kuwezesha hilo.

Ni Rais Magufuli tu ndio hataki watoto wa kike warudi shuleni. Hii Nchi sio ya Magufuli peke yake. Hatuwezi kukaa kimya kumwona mtu mmoja analazimisha imani zake kwa Jamii nzima ya Watanzania.

Zitto Z. Kabwe,
Mbunge,
Jimbo la Kigoma ujiji,
Kiongozi wa Chama, Alliance for Change and Transparency.
P
 
Watoto waliopata mimba kuendelea na masomo sio tatizo, ila wanaendelea vipi? Je wanarudi katika shule yake ile ile aliyokua akisoma awali au atafutiwe shule nyingine?

Leo nilikua nawauliza wanafunzi, je wana mtazamo gani juu ya kuruhusiwa kwa watoto waliopata ujauzito kuendelea na masomo? Walioonekana kuunga mkono hili na kulifurahia kama lingekuwepo ni wavulana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hassan Mambosasa kinachoongelewa siyo sheria inayokataza mtoto wa kike kurudi shule baada ya kujifungua bali mkopo kulipwa na huyo mtoto ama wazazi wake. Huo mkopo hautalipwa na hao mabinti mnaowafukuza na kuwazuia wasirudi shule?
 
Muhtasari,

Zitto Kabwe kaomba mkopo wa trilioni usitishwe kwa sababu hizi,

  • Mwanahabari Erick Kabendera bado anasota rumande
  • vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano isipokuwa chama tawala pekee,
  • mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar ukiwa umevurugwa
  • kuwazuia zaidi ya wagombea 400,000 wa vyama vya upinzani wasigombeaa nafasi za uongozi
  • C.A.G kufukuzwa kutoka ofisini kinyume cha Katiba mwezi Novemba
  • uchaguzi mkuu 2020 kuwa na dalili utavurugwa na kuharibiwa
  • fedha za mkopo uliokataliwa zingetumika kinyume na lengo (ufisadi)
  • watanzania kulazimika baadaye kulipia mkopo huu
Binafsi Nadhani angewasilisha bungeni hoja hizi ili zijadiliwe kama zina uzito au la, ukweli au la, n.k Hakuwa na sababu ya kuhofia wala kutilia mashaka kuwasilisha hizo hoja zake katika serikali yetu tukufu yenye haki,
Sasa mbona WB wanasema wamezuia kisa mimba sasa mbonq hatuoni hoja ya mimba hapo au ndio upepo wa kisurisuri umemkuta zito kamua tembea nao yani kakutana na mtaji wa kiki ya kisiasa kamua tembea nayo
 
Ndugai na CCM wamekosa hoja, hoja sio Zitto kuomba WB wazuie Mkopo, Hoja ni je alichoandila Zitto na WB wakakielewa ni Uongo?

Nashangaa hawataki kugusa content ya barua ya Zitto Kabwe wanagusia tu Matokeo ya Barua husika.

CCM na ndugai wajibu hoja kuwa tunasitahili mikopo
1. Kwakuwa wasichana wanaruhusiwa kuendelea na masomo baada ya Kujifungua

2. Wathibitishe bila shaka kuwa Tanzania kuna uhuru wa habari

3. Kuwa Siasa Tanzania zinafanyika kwa uhuru kea mujibu wa katiba

4. Kuwa Kupotea, kukamatwa na kuwekwa vizuizini ikiwepo kuteka Raia na Waandishi wa Habari, Serikali haihusiki na unachukua hatua.

Hizi ni baadhi ya hoja wanazopaswa kuzijibu au kukanusha toka kwenye maďai ya ZZK kwenda kwa WB. Vinginevyo hawana hoja.

Viva ZZK tupo kukupa Sapoti sisi Wananchi

Dumelang
 
Back
Top Bottom