Zitto Kabwe: Mkopo wa Benki ya Dunia kuboresha elimu, Serikali ililenga kuinufaisha CCM kwa kununua vyuo vilivyo chini ya chama hicho

Zitto Kabwe: Mkopo wa Benki ya Dunia kuboresha elimu, Serikali ililenga kuinufaisha CCM kwa kununua vyuo vilivyo chini ya chama hicho

Hivi huyu Zitto si ndo aliyeenda kwa mabeberu kushinikiza kuzuia mradi wa Bonde la Nyerere (Stiglars Gorge) usianze? Je alifanikiwa? Mradi si unaendelea? Kelele za chura hazizuii chura kunywa maji! Hao wanafunzi wapenda ngono na kuzaliana shuleni akaanzishe shule yake akawasomeshe! Hatujakataza NGO na shule binafsi kusomesha wazazi! Tumekataa shule za umma zinazoendeshwa kwa kodi za wananchi kushabikia ngono mashuleni kuzaliana na kuruhusiwa kuendelea! Zitto na mabeberu wanaokussuport anzisheni hizo shule si tu za kusomesha wazazi lakini pia za kusomesha mashoga! Prof. Assad tayari kaishatumbuliwa na tumeishamsahau!
Nchi haziongozwi kwa akili ndogo kama yako! Hujui chochote kojoa ukalale!
 
Muhtasari,

Zitto Kabwe kaomba mkopo wa trilioni usitishwe kwa sababu hizi,

  • Mwanahabari Erick Kabendera bado anasota rumande
  • vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano isipokuwa chama tawala pekee,
  • mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar ukiwa umevurugwa
  • kuwazuia zaidi ya wagombea 400,000 wa vyama vya upinzani wasigombeaa nafasi za uongozi
  • C.A.G kufukuzwa kutoka ofisini kinyume cha Katiba mwezi Novemba
  • uchaguzi mkuu 2020 kuwa na dalili utavurugwa na kuharibiwa
  • fedha za mkopo uliokataliwa zingetumika kinyume na lengo (ufisadi)
  • watanzania kulazimika baadaye kulipia mkopo huu
Binafsi Nadhani angewasilisha bungeni hoja hizi ili zijadiliwe kama zina uzito au la, ukweli au la, n.k Hakuwa na sababu ya kuhofia wala kutilia mashaka kuwasilisha hizo hoja zake katika serikali yetu tukufu yenye haki,
[/QUOTE Usiogope mkuu kwa vile Serikali yetu tukufu ni yenye kutenda haki kama ulivyosema bila shaka hayo madai ya Zito hayatasikilizwa kwa kuwa madai hayana ukweli. Hakuna haja ya kupanic.
 
Muhtasari,

Zitto Kabwe kaomba mkopo wa trilioni usitishwe kwa sababu hizi,

  • Mwanahabari Erick Kabendera bado anasota rumande
  • vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano isipokuwa chama tawala pekee,
  • mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar ukiwa umevurugwa
  • kuwazuia zaidi ya wagombea 400,000 wa vyama vya upinzani wasigombeaa nafasi za uongozi
  • C.A.G kufukuzwa kutoka ofisini kinyume cha Katiba mwezi Novemba
  • uchaguzi mkuu 2020 kuwa na dalili utavurugwa na kuharibiwa
  • fedha za mkopo uliokataliwa zingetumika kinyume na lengo (ufisadi)
  • watanzania kulazimika baadaye kulipia mkopo huu
Binafsi Nadhani angewasilisha bungeni hoja hizi ili zijadiliwe kama zina uzito au la, ukweli au la, n.k Hakuwa na sababu ya kuhofia wala kutilia mashaka kuwasilisha hizo hoja zake katika serikali yetu tukufu yenye haki,
1. Wangeleta bungeni kabla ya kuomba mkopo.
2. Mkopo usha ombwa, kuleta bungeni ni kuruhusu utolewe wkt mkiendelea na majadiliano
3. Hakuna bunge la kupinga uamuzi wa serikali uwe mzuri au mbaya
4. Spika mwenyewe anaongoza kwa kupewa maelekezo.
5. Tayari serikali imetangaza mara nyingi haitaki pesa za makaburu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe si unajiamini?,na huogopi?,sawa
Barua niliyoandika Benki ya Dunia ni hii. Nipo tayari kulipa gharama yeyote kwa kuandika Barua hii. Serikali ya Rais Magufuli inapaswa kujua, naikumbusha tena, kuwa SIOGOPI lolote katika lile ninaloamini.

Nataka kila Mtoto wa kike wa Tanzania awe na haki sawa ya kupata Elimu - apate Mimba ama asipate mimba. CCM waliahidi kwenye Ilani yao kuwa watoto waliopata uja uzito Wataendelea na Masomo. CHADEMA wanaamini hivyo na Act Wazalendo tunaamini hivyo.

Makamu wa Rais Bi. Samiah Suluh amenukuliwa akiamini hivyo na Waziri wa Afya pia. Wizara ya Elimu ilitunga mpaka mwongozo wa kuwezesha hilo.

Ni Rais Magufuli tu ndio hataki watoto wa kike warudi shuleni. Hii Nchi sio ya Magufuli peke yake. Hatuwezi kukaa kimya kumwona mtu mmoja analazimisha imani zake kwa Jamii nzima ya Watanzania.

Hongera nyingi kwa Watanzania waliohakikisha kuwa tunasubirisha Mkopo wa Benki ya Dunia mpaka hapo utakapoboreshwa na kutoa nafasi kwa watoto wa kike kupata Elimu bila ubaguzi wala unyanyapaa.

=======
BARUA KWENDA BENKI YA DUNIA KWA KISWAHILI:
=======

Januari 22, 2020.

Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia,
1818 H Street
Washington, DC
20433

Wapendwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia,

YAH: MKOPO WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 500 KWA AJILI YA MRADI WA UBORESHAJI WA ELIMU YA SEKONDARI NCHINI TANZANIA

Jina langu naitwa Zitto Kabwe, ni Mbunge kutoka Manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania.

Ninawaandikia barua hii kuhusu kikao cha Bodi cha tarehe 28 Januari 2020, kikao ambacho Bodi itajadili mkopo wa Tanzania kiasi cha Dola za kimarekani milioni 500 kwa ajili ya Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari Tanzania.

Katika barua yangu kwenu ya tarehe 9 mwezi Septemba, niliwakumbusha kuhusu hali mbaya ya masuala ya haki za kijinsia na kibinadamu nchini mwangu. Kwa masikitiko, inaonekana kwamba hatua ya Benki ya Dunia kuidhinisha fedha za mradi ujulikanao kama "Productive Social Safety Net" mwezi Septemba iliitia makucha serikali hii. Kwa hakika, hali imekuwa mbaya mno. Mwanahabari Erick Kabendera bado anasota rumande, vyama vya siasa havina ruhusa ya kufanya mikutano ya hadhara, nao mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar ukiwa umevurugwa hali inayopelekea majaliwa ya uchaguzi mkuu wa 2020 kukosa maana.

Ni wiki iliyopita tu, vikosi vya usalama vilinizuia mimi kufanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wapigakura wangu. Vikwazo vya jinsi hii wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Novemba mwaka jana, vilitawala kwa vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano isipokuwa chama tawala pekee, chama cha mapinduzi. Wakati wa uchaguzi huo wa Novemba, chama cha mapinduzi kiliwazuia zaidi ya wagombea 400,000 wa vyama vya upinzani wasigombeaa nafasi za uongozi kwa kuwa tu walionekana wasiokubaliana na matakwa ya serikali hii. Matokeo yake, takribani vyama vyote viliususia uchaguzi huo na kupelekea asilimia 99.6 ya viti vilivyokuwa vikigombewa kunyakuliwa na chama tawala.

Nazo fursa haba za kiuwajibikaji wa kikatiba zilizokuwa zimesalia kama vile uwepo wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nazo zimehujumiwa, kwani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amefukuzwa kutoka ofisini kinyume cha Katiba mwezi Novemba mwaka jana, hali inayoweka rehani usalama wa fedha za walipakodi na uwekezaji wa benki yenu. Mwaka 2020 tunatarajia kufanya uchaguzi mkuu ambao tunaona dalili zote kwamba utavurugwa na kuharibiwa na chama tawala ili kujihakikishia ushindi wa bwelele.

Serikali hii haina tena usafi wa kujidai kuwa serikali inayowakilisha maslahi ya watu wa Tanzania, isipokuwa inajali na kulinda maslahi ya wachache. Jambo la kusikitisha ni kwamba, si hiki kikundi kidogo cha watawala wa sasa bali ni watanzania hawa kwa wingi wao ndio ambao watalazimika baadaye kulipia mkopo huu. Kubwa zaidi, hofu yetu ni kwamba kutokana na ukosefu wa misingi ya uwajibikaji, malengo ya uwekezaji wa fedha hizi yatatumiwa vibaya na chama tawala kujinufaisha kisiasa na kuharibu mchakato wa uchaguzi.

Kwa mantiki hiyo, ninakuombeni msimamishe utolewaji wa fedha hizo kwa serikali hii mpaka pale misingi ya uwajibikaji itakaporejeshwa Tanzania. Misingi hii ya uwajibikaji ninayoizungumzia ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kukusanyika, chaguzi huru na za haki, sanjali na kumrejesha ofisini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mnamo tarehe 3-8 mwezi Februari, nitakuwa Washington DC. Nitafurahi kukutana nanyi tuweze kutazama kwa yakini namna ambavyo mchango wa Benki ya Dunia unaweza kuwa wenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu.

Ni imani yangu kuwa tutapata wasaa mzuri kujadiliana.

Wenu,

Zitto Z. Kabwe,
Mbunge,
Jimbo la Kigoma ujiji,
Kiongozi wa Chama, Alliance for Change and Transparency.

Nb: Barua hii iliandikwa katika lugha ya Kiingereza. Imetafsiriwa katika Kiswahili na Vicent Kassala.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhtasari,

Zitto Kabwe kaomba mkopo wa trilioni usitishwe kwa sababu hizi,

  • Mwanahabari Erick Kabendera bado anasota rumande
  • vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano isipokuwa chama tawala pekee,
  • mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar ukiwa umevurugwa
  • kuwazuia zaidi ya wagombea 400,000 wa vyama vya upinzani wasigombeaa nafasi za uongozi
  • C.A.G kufukuzwa kutoka ofisini kinyume cha Katiba mwezi Novemba
  • uchaguzi mkuu 2020 kuwa na dalili utavurugwa na kuharibiwa
  • fedha za mkopo uliokataliwa zingetumika kinyume na lengo (ufisadi)
  • watanzania kulazimika baadaye kulipia mkopo huu
Binafsi Nadhani angewasilisha bungeni hoja hizi ili zijadiliwe kama zina uzito au la, ukweli au la, n.k Hakuwa na sababu ya kuhofia wala kutilia mashaka kuwasilisha hizo hoja zake katika serikali yetu tukufu yenye haki,
Bunge lipi? Kwani kuna Mbunge hata mmoja wa CCM kwenye Bunge la Ndugai anayejitambua? Bunge halina uhuru kabisa kwa vile Ndugai ana amrishwa na Jiwe nyuma ya la
pazia kukandamiza wawakilishi wa wananchi
 
Halafu wana jf wengi mlikuwa hamjaifatilia hii barua, neno lililokuwa kipaumbele ni mabinti wakipata mimba warudi shule.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana.

Mabinti waliopata mimba na kusimamisha masomo walikuwepo tokea enzi za uhuru wetu. Hakuna lolote hapo lililobadilika katika awamu zote zilizopita.

Tofauti ni moja tu ambayo wengi wenu mnaoshupalia hili hamtaki kuikubali.

Hilo moja la hao watoto limeunganika na mengi mengine kama yalivyoorodheshwa kwenye barua hiyo.

Hiyo ndiyo tofauti mnayotakiwa kuitilia maanani; lakini mnaikwepa! Kwa nini?
 
Alitoa ahadi lini?
Wakati anatuomba kura kutokana na muongozo wa ilani yao
tapatalk_1580495035794.jpg
 
Nani angemsikiliza ama kuzipokea hizo hoja?
 
Mimi nasubiri mrejesho wa huko Washington nadhan sisi wana lumumba ni vizuri tukamtuma balozi wetu akatupangulie hoja za Zitto
 
Kumzuia Mtanzania kupata elimu ni kukiuka katiba. Wanafunzi wenye ujauzito wana haki ya kuendelea na elimu baada ya kujifungua.
Kwaiyo wakipata mimba na kuzaa, mtoto nani analea?
 
Nasi weupe kichwani tumeelewa.chanja mbuga zitto tungepata kama huyu wa5 wanashambulia kwa umoja ingekuwa poa
 
Tuache siasa watoto wanaopata mimba hawajawai kuruhusiwa kuendelea na masomo kwenye shule za umma toka Mkapa, Kikwete Sema kilichomponza Magufuli ni kuropoka na dunia ikajua.
Uko poa sana we jamaa,Magufuli analopoka sana
 
Kuna binti a najiandaa kushika mimba usiku huu akijua atapata msamaha
 
Back
Top Bottom