Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe ndiye atakayesababisha CCM waingie Ikulu kiulaini 2020

Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe ndiye atakayesababisha CCM waingie Ikulu kiulaini 2020

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Mimi si mwandishi mzuri,ni mvivu kuandika mambo kwa undani. Nitaandika short & clear.

Ndani ya miaka 5 ya uongozi wa Mh. Magufuli Watanzania kama wafanyabiashara, watumishi wa umma na watumishi wa sekta binafsi, wakulima wa mazao mbalimbali wamepitia kipindi kigumu.

Hata wananchi wa kawaida nao wamekuwa wakiushangilia utawala wa Mh. Magufuli kwa mihemko tu lakini hali zao zimekuwa ngumu.

Karibu kila ukoo au familia wameshuhudia ndugu au watoto wao wakiishia kuwa jobless baada ya kukosa ajira.

Classmates wangu wa advance ambao karibu 98 % walihitimu shahada ya kwanza 2016 na 2017 wengi hawako ktk ajira rasmi. Wanasubiri miujiza.

Uchaguzi mkuu wa October 25 ,2020 ndio ulikuwa wa kumnyima kura za ndio Mheshimiwa Magufuli na kumpa Mh.Tundu Lissu au mpinzani yeyote aliye thabiti.

Sasa Mh. Zitto Kabwe anapotaka kutuletea huyu Mh. Membe anakwenda kuzigawa kura za upinzani na kuifanya CCM iendelee kututawala bila ridhaa yetu.

Membe (mgeni) karibu upinzani ila nafasi ya kugombea Urais hustahili kwasasa, labda miaka 5 ijayo.

Hatutaki ya Lowasa, si kwamba una uchungu sana na Watanzania bali unauchungu na ndoto zako za kuwa Rais ambazo zilizimwa na wamafia kule Dodoma 2015.
Kuna brother mmoja ni senior officer TISS aliwahi kuniuliza swali moja wakati tunajadili jambo fulani. Aliniuliza " Hivi kwanini Lowasa katika kipindi chote alichokuwa upinzani hakuwahi kutoa siri yoyote ya serikali?".
Hili swali ni fupi na jepesi ila lina majibu mengi kwa ndani.
Tusiwaamini hawa half cast wa kisiasa kwa 100%.
 
Hivi Magufuli kasababishaje tatizo la ajira?

Au tunamtumia baada ya kuzikosa sababu tu za tatizo la ajira. Maana tatizo la ajira nchi hii lipo toka enzi za JK.

Tumesahau kabla ya Magufuli kuanza kutawala mzee Lowassa alikuwa analalamikia bomu litakalolipuka? Ajira ni tatizo la Dunia na karibia kila nchi inahangaika na ajira.
 
Hivi Magufuli kasababishaje tatizo la ajira?

Au tunamtumia baada ya kuzikosa sababu tu za tatizo la ajira. Maana tatizo la ajira nchi hii lipo toka enzi za JK.

Tumesahau kabla ya Magufuli kuanza kutawala mzee Lowassa alikuwa analalamikia bomu litakalolipuka? Ajira ni tatizo la Dunia na karibia kila nchi inahangaika na ajira.
Kwahiyo unemployment rate ina uwiano sawia kati ya kipindi cha Jk na jpm?
 
Daby

Tatizo la ajira lipo na litakuwepo, na kama ajira ni chakula basi wakati wa JK kulikuwa na upungufu, ila Magufuli yeye badala ya upungufu wa chakula, yeye hatoi CHAKULA KABISA.

Magufuli haajiri kabisa.

Ukimaliza Chuo, Nenda Kwenu.

Ukijifanya unaenda sekta binafsi, unakuta inapumulia mashine kwa sababu kibao ikiwemo serikali kufanya biashara yenyewe.

Hata tuambie siyo jukumu la serikali kutengeneza Ajira ?

Kama Ni Jukumu Lake, Ni Sahihi Serikali Kuajiri Watanzania LAKI 5 tu kati ya watu MILIONI 60 Huku Ikishindwa Kuwahudumia ?
 
Back
Top Bottom