JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
"Suala la Rais Mwinyi kumteua mtu aliyehusika kuvuruga uchaguzi wa 2020 kuwa Mkurugenzi wa ZEC, HALIKUBALIKI. Tumeamua kurudi chini kwa Wanachama wetu. Ni wao waliotaka tuingie kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wao pia ndio watakao amua hili," kauli ya Zitto Kabwe akiwa Kata ya Mchoteka, Jimbo la Tunduru Kusini, Ruvuma.
Anasema: “Ziara hii ya Tunduru ilipaswa kufanywa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, lakini imebidi aongoze kikao cha Kamati Maalum ya Kamati Kuu ya ACT Wazalendo Zanzibar, Kujadili Suala ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Rais Mwinyi ameteua mtu aliyesimamia uchaguzi wa 2020, sisi tumeamua kurudi kwa Viongozi na Wanachama wetu ngazi ya Matawi, tutawaambia hali ilivyo, na watuambia la kufanya.”