Zitto Kabwe: Sitagombea tena Uongozi ndani ya ACT WAZALENDO, najikita kwenye Ubunge. Malengo yangu ni kuwa Rais wa Tanzania

Hao sio wanachama wa ACT ni wafuasi wa Maalim Seif. Mnapenda kudandia mambo. ACT ya Sasa ni dhoofu bin tabu.
 
Zitto msaliti tu Hana jipya.
 
Mrejeshi wa Nini? Nimeshamjibu. Ukiona kiongozi wa chama Cha siasa yupo madarakani Ina maana Katiba inamruhusu kuendelea. Huyo Zitto Katiba ya ACT ilimwekea limit ya miaka kumi. Sasa unafiki wenu mnadhani ni hiari yake. Acheni hizo.

Huo ni mrejesho wa hitaji hili?

"Nipe mfano wa chama kingine cha upinzani ambapo mwenyekiti au kiongozi wake ameheshimu ukomo wa uongozi kikatiba hapa Tanzania!..
Ukishindwa jitambue kuwa wew ni zwazwa."

Kwa hiyo mfano uko wapi ndugu?


Cc: 1120ulimwengu
 
Hao sio wanachama wa ACT ni wafuasi wa Maalim Seif. Mnapenda kudandia mambo. ACT ya Sasa ni dhoofu bin tabu.

1. Kwani Maalim Seif alikuwa mwanachama wa CUF au CCM?

2. Udhaifu wa mpinzani mwingine si tija kwa yeyote zaidi ya CCM na vibaraka wake (kwa kujitambua au kutokujitambua kwao).
 
Kama ukomo haupo? Utaheshimu Nini?
 

CCM watakuwa na furaha sana kokote kule waliko. Makasiriko yote ya nini ndugu?
 

..nasubiri ACT Wazalendo wajitoe ktk serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

..mtakumbuka CDM nao wamejitoa ktk mazungumzo ya maridhiano na CCM.
 
1. Kwani Maalim Seif alikuwa mwanachama wa CUF au CCM?

2. Udhaifu wa mpinzani mwingine si tija kwa yeyote zaidi ya CCM na vibaraka wake (kwa kujitambua au kutokujitambua kwao).
Ninaamini ACT sio wapinzani. Mpinzani alikuwa maalim seif pekee.
 
Miaka 10 iliyopita alikuwa anadai apewe nafasi ya kugombea urais Sasa hivi anarudi kwenye ubunge, tukisema kipindi kile alikuwa anatumika tutakuwa tunakosea.
Nakumbuka akiwa CHADEMA 2010 kwenye kampeni za ubunge alidai akirudi 2015 atakuja kugombea urais na sio ubunge. Ila ilipofika 2015 akarudisha nyuma majeshi.
 
..nasubiri ACT Wazalendo wajitoe ktk serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

..mtakumbuka CDM nao wamejitoa ktk mazungumzo ya maridhiano na CCM.

1. Inafahamika wengine hatukuyapenda maridhiano tokea day 1.

2. Hapo #1 tukakubaliana kutofautiana.

3. Kulikoni tusiendelee kukubaliana kutofautiana: watoke au wasitoke?
 
Imani yako haiwezi kuwa ndiyo msahafu rasmi au vipi?
Ndio maana nikasema ninaamini. Kwa sababu huyo Zito na kundi lake lote waliohamia CCM akina Kitila, mwigamba, Mkumbo, mgwira nk. Waliposhindwa kuiangusha CHADEMA wakakimbilia CCM kupewa teuzi. Leo utaniamisha vipi kwamba ACT ni wapinzani?
 
Mfano nitoe wapi?. Maana kama katiba haijatoa limit ya muda unalazimisha watu wastaafu?
Na ndipo mleta hoja alipokwambia utoe mfano. Ukiupata nilimwomba, sina shaka utakapompa atanambia. Tatizo liko wapi ndugu?

Haya ya kuiangusha Chadema ni mawazo yako. Binafsi nachukizwa na wasiotaka umoja.
 
1. Inafahamika wengine hatukuyapenda maridhiano tokea day 1.

2. Hapo #1 tukakubaliana kutofautiana.

3. Kulikoni tusiendelee kupenda kukubaliana kutofautiana: watoke au wasitoke?

1. ACT hawajapata walichotegemea kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

2. CDM hawajapata walichokitegemea kupitia mazungumzo ya maridhiano.

3. Wote wajipange upya na kuja na mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…