Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

kwahiyo alitaka kawilaya kenye watu chini ya 2m kapate sawa na nchi yenye watu 58m? ni haki yake aseme hivyo kwasababu ACT WAZALENDO wapo zenji pekee huku bara hawapo. na huko ndiko anapatia ruzuku. opportunist mno huyu, na anatafuta upendeleo kwa ccm wampe tena pesa amalizie kale kagorofa kalikosimama ujenzi pale dodoma karibu na kisasa.
Kapate Kwa uwiano sawa na kanachochangia
 
Zito Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zito ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785636663323996254?t=s92jVBKH81hHu1XZDDDIwg&s=19

My Take
Naunga mkono hoja ya Zito,Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lisu.

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785629244741005525?t=aa-cd8j2wSKWNuS9EY_8Dw&s=19

Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?

Nafkiri angeweka takwimu rasmi watu wakokotoe hapo, namba huwa hazidanganyi...
Hata nawe ni mchumi unaweza saidia weka takwimu...Tanzania sasa ina wasomi
 
Zito Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zito ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785636663323996254?t=s92jVBKH81hHu1XZDDDIwg&s=19

My Take
Naunga mkono hoja ya Zito,Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lisu.

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785629244741005525?t=aa-cd8j2wSKWNuS9EY_8Dw&s=19

Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?

Hili nalo si Lirundi, linaongea nini?
 
sawa jibu hoja za lissu kama mgawanyo uwe sawa!
Lisu hajatoa hoja zaidi ya kuhubiri chuki na mgawanyiko.

Mbona Mkapa mlisema anauza Nchi,alikuwa ni Mzanzibari?

Tangu lini ubinafsishaji ukawa kuuza Mali?

Pili tangu lini kuhamisha Masai kuwatoza kwenye Hifadhi Ili kuilinda ikawa kufukuza watu? Maana wanaohamishwa Kwa staha na stahiki zote,kufukuza kunatokea wapi?

Hapo Kuna hoja au upunguani?

Mwisho uvunje Muungano Kwa maslahi ya nani? Ili kitokee nini hasa?
 
Zito ni mchumi mwenzangu, takwimu zinaongea hatutaki porojo.
Hapo kataja % tu,ambapo
  • Hatujui kama hizo % ni za kweli
  • Jumla ya hayo makusanyo kwenda serikali kuu
  • Jumla pesa Zanzibar inazopokea kutoka serikali kuu
  • Data ni za mwaka gani
  • Chanzo cha hizo data zake
Wekeni data zilizokamilika hapa, watu wapitie, hapo ndipo mjadala utakuwa sawa.
 
Zenj wangejitawala wangekuwa mbali sana,wanapiga kazi ila Bara watu Wana mdomo na fitina hatari.

Just imagine licha ya Samia kutoka Zanzibar kuwaokoa kwenye uchumi ulikokuwa unakuta wameishia kumjazia fitina 😁😁
Sheri Sheri au madagasca wako mbali?
 
Onyesha hiyo 20% ulikoitoa maana hiyo hoja ndio Zito kaioinga hapo Juu Kwa kusema ni 4.5% only.

Pili mbona huzungumzii hoja yake ya kwanza?

Msitafute excuses TRA peke yake inakusanya zaidi ya Bilioni 400 kutoka Zanzibar hapo sijataja taasisi zingine za Muungano mfano Uhamiaji nk.

Hiyo figure ya bilioni 400 haina maana yoyote kama huelezi Zanzibar inapata nini kutoka Serikali ya JMT. Kwenye makusanyo ya TRA umetaja figure ya makusanyo. Kwenye mgawanyo wa makusanyo unataja asilimia! Unaficha nini? Ndiyo maana nasema kuwa hoja ya Zito ni kwaajili ya wajinga.

Kama hujui, makusanyo ya TRA ya JMT ni wastani wa trilioni 3 kwa mwezi. Kwa mwaka ni takribani trilioni 36. Bilioni 400 ni only 1%. Hivyo, hata maneno yamo ya kusrma kuwa Zanzibar inapata 4.5% yangekuwa ni ya kweli, bado Zanzibar inapata kikubwa sana ukilinganisha na inachochangia. Zanzibar inachangia 1%, halafu inapata 4.5%.

Yaelekea wewe siyo mfuatiliaji wa mambo. Hata ile pesa ya mkopo wa Covid toka Jumuia ya Ulaya, Zanzibar ilipata 20%, na watu walilalamika, na hata hapa JF kulikiwa na mada iliyohusiana na mgawanyo huo usiozingatia uhalisia.
 
Changamoto
pesa ndogo sana hiyo,Tena wazanzibar wanatupunja,hiyo ina maana TRA Kila mwezi huchukua billion 33.3🤣🤣🤣,halafu hela hiyohiyo tuwalipe wabunge wao 80 wanaofika huku,wanajeshi,police na uhamiaji walioko kule,wizara zote za muungano na hapohapo wanapata asilimia mbili Tena aisee mbona tunapunjwa sisi wabara
 
Zito Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zito ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785636663323996254?t=s92jVBKH81hHu1XZDDDIwg&s=19

My Take
Naunga mkono hoja ya Zito,Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lisu.

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785629244741005525?t=aa-cd8j2wSKWNuS9EY_8Dw&s=19

Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?

Kama ndivyo hivyo kuna haja ya kupata Katiba Mpya haraka mwaka huu ili kuponya majeraha ya pande zote mbili,Zanzibar na Tanganyika na kabla mambo hayajaharibika
 
Onyesha hiyo 20% ulikoitoa maana hiyo hoja ndio Zito kaioinga hapo Juu Kwa kusema ni 4.5% only.

Pili mbona huzungumzii hoja yake ya kwanza?

Msitafute excuses TRA peke yake inakusanya zaidi ya Bilioni 400 kutoka Zanzibar hapo sijataja taasisi zingine za Muungano mfano Uhamiaji nk.
Jeshi la wananchi mnataka bara tugharimie pekeyetu?
 
Zanzibar inajitegemea Kwa Mapato yake ,kinachotoka Bara kwenda huko ni 2% tuu na wakati Bara mnakomba 98% ya Mapato yanayotokana na Muungano zikiwemo zaidi ya Bilioni 400 ambazo TRA anakusanya Bado taasisi zingine kama uhamiaji ,Utalii nk.
Sasa kama inajitegemea kwa mapato yake,hyo asilimia 2 inaenda Zanzibar kufanya nini?? Huoni kama inawanyonya watanganyika??
 
Lisu hajawahi kuwa mropokaji hata siku moja. Lolote alinenalo Lisu, huwa amelifanyia kazi kwa umakini. CCM ndiko huwa wamejaa waropokaji na wapiga kelele.
Lisu ni mahiri wa sheria sio masuala ya Uchumi.

Pili ubinafsishaji ni sawa na kuuza Nchi? Huku sio kuropoka?
 
Sasa kama inajitegemea kwa mapato yake,hyo asilimia 2 inaenda Zanzibar kufanya nini?? Huoni kama inawanyonya watanganyika??
Kugharania shughuli za Muungano(Tanganyika) Zanzibar
 
Ni haki yao kupata kiasi hicho kutokana na population yao ndogo na ukubwa wa nchi ulivyo na pia shughuli za kiuchumi zilivyo, kama kuna kuna kupunjana itoeni Tanganyika kwenye koti la muungano iwe na serikali yake,katiba yake na kisha tuunde shirikisho hiyo ndiyo suluhisho ya malalamiko ya Zanzibar na Bara pia
 
Back
Top Bottom