Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe: Tutaandamana nchi nzima kudai haki ya wagombea wetu walio enguliwa kwenye uchaguzi

Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe: Tutaandamana nchi nzima kudai haki ya wagombea wetu walio enguliwa kwenye uchaguzi

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Anaandika mhe Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba chama chake kitafuata taratibu zote za kisheria kudai haki pia wanaunga mkono tamko la mwenyekiti wa chama hicho pamoja mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA mhe Tundu Lissu kwamba lazima wananchi wafanye maandamano ya kudai haki ya wagombea wao na usawa katika uchaguzi kutokana na wagombea wengi wa vyama vya upinzani kuenguliwa.

Wakati tunaendelea na hatua zote za kisheria ( hatutaacha hata moja ) pia tunaunga mkono wito wa Mwenyekiti wa Chama Taifa @SeifSharifHamad na Mgombea wa @ChademaTz @TunduALissu kuandamana Nchi nzima kutaka wagombea wetu warejeshwe. @TumeUchaguziTZ iwe makini sana sana.

Screenshot_20200829-100719.png

MY TAKE: Kudai haki ni jambo la lazima mahala popote pale duniani ambapo haki za wengine zinakandamizwa lakini vyama pinzani vinatakiwa kutambua kwamba vitisho dhidi ya serikali sio njia sahihi ya kudai haki.
 
Kwa hiyo tamko la seif ni tifauti na la ACT? Mbn anasema tunaunga mkono tena wakati maalim alitoa kwa miguu ya Act? Ina maana kuna ACT mbili?
 
Labda Kama wataandamana huko Twita Ila siyo huku mtaani.

Sasahivi hatupoi leo tukishamaliza tu kukiwasha Dodoma tunahamia kesho kwa mkapa kuungana na timu ya Wananchi.

Sasa kwa jinsi Wananchi tulivyo busy na Mambo ya Furaha na mhimu kama haya tutapata Muda wa kuandamana kwa ajili ya upuuzi wa wachimia njaa Wachache tu.

Hatupo tayari mtusamehe.
 
Uchaguzi wa mwaka huu ni mwepesi sana.

Wapinzani wamechoka mapema sana wanapanga kuvuruga uchaguzi

Kuandamana kwa ajili ya majimbo 18 wakati Kuna viti zaidi 250 ni uamuzi wa hovyo sana

Ni dhahiri wapinzani wamegundua hawamuwezi Magufuli kwenye sanduku,wanatafuta kila mbinu ya kuharibu uchaguzi,ili ionekane wameonewa
 
Maandamano wakati wenzenu wanaendelea na kampeni hawana habari, Zitto kuwa serious bhana.

Kwanini turuhusu uchaguzi kufanyika kama wagombea wao wanapitishwa pekeyao bila uchaguzi??
 
Haki haiombwi
Haki haina kubembelezana

Hatua zote za kisheria zifatwe then maamumuzi magumu yatafuatwa.

Ofa ya lowasa ilikuwa kubwa ila mkamdhalau sasa mna kibalaka wa beberu ambae mlimpigania na kumpa sifa kuliko wengine hapo ufipa, sasa cha moto mnakiona. Badala ya kutoa tambo za mafuliko yasiyo zuilika kwa mikono, sasa manapanga kufanya fujo, mmekata tamaa mapema sana hata jogoo halijawika?

Matamshi yenu ni ya hasira baada ya kuona hali jana.

Plei makamada.
 
CCM wamekuwa wakiendesha siasa za hila. Mwanademokrasia hawezi kupoteza muda wake kumwengua mpinzani wake bali hutumia muda wake mwingi kushindana kwa kupigiwa kura.

Mara nyingi kiongozi wako akiwa ni mtu wa tabia fulani, na wafuasi wake humfuata.

Rais hajui demokrasia, hajui haki, siyo mcha Mungu bali ni muigizaji, wakati wote alipokuwa mbunge alikuwa akipita kwa hila bila ya kupigiwa kura na wapiga kura. Sasa ameondoka na hulka yake yote na kuiingiza ndani ya chama. Leo wafuasi wake, hata wale ambao mwanzoni walionekana kuwa ni timamu katika mambo mengi, wametekwa na matendo na tabia zisizo za kistaarabu za kiongozi wao. Wanashangilia na kukumbatia uovu.

Kufuata taratibu za kisheria ni kupoteza muda. Rais amenajisi mihili mikuu ya Jamhuri. Mahakama na bunge zimefanywa kuwa ni taasisi za Chama.

Wananchi ni lazima tuidai haki kwa nguvu. Na watu wajue kuwa njia za kistaarabu kuweza kufanya kazi endapo tu unakabiliana na mtu mstaarabu, siyo huyu wa sasa. Huyu ni kiongozi anayependa kutumia nguvu na mabavu, hawezi kuelewa mpaka na sisi tututmie nguvu na mabavu.

Zito usipoteze muda kufuata hizo taratibu za kisheria. Fanyeni kampeni kubwa nchi nzima hada kwenye miji yote angalao kwa siku 10 kwaajili ya kuiandaa kazi takatifu ya kujenga utawala wa sheria, haki na demokrasia. Baada ya hapo maandamano yaanze ya kumlazimisha Rais kutii katiba na sheria na kuacha siasa za hila.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchaguzi wa mwaka huu ni mwepesi sana.
Wapinzani wamechoka mapema sana wanapanga kuvuruga uchaguzi.
Kuandamana kwa ajili ya majimbo 18 wakati Kuna viti zaidi 250 ni uamuzi wa hovyo sana.
Ni dhahiri wapinzani wamegundua hawamuwezi Magufuli kwenye sanduku,wanatafuta kila mbinu ya kuharibu uchaguzi,ili ionekane wameonewa.

Kama uchaguzi wa mwaka huu ni mwepesi ndiyo muwaache wagombee ili washindwe kwenye sanduku la kura. CCM ndiyo inaleta vurugu maana nyinyi ndiyo mnamiliki vyombo vyote vya ulinzi na usalama,NEC na mahakama. Tumeona NEC inajibu pingamizi kwa niaba ya mgombea wa CCM.

CCM mpo tayari damu imwagike ili muendelee kutawala.
 
Ofa ya lowasa ilikuwa kubwa ila mkamdhalau sasa mna kibalaka wa beberu ambae mlimpigania na kumpa sifa kuliko wengine hapo ufipa, sasa cha moto mnakiona,
Badala ya kutoa tambo za mafuliko yasiyo zuilika kwa mikono, sasa manapanga kufanya fujo, mmekata tamaa mapema sana hata jogoo halijawika?
Matamshi yenu ni ya hasira baada ya kuona hali jana.
Plei makamada.
mkamdhalau - mkamdharau
mafuliko - mafuriko
kibalaka - kibaraka
 
Wapi serikali katishwa?

Kupashwa ukweli huo ni wajibu.

Kudos Maalim, kudos Lissu na kudos Zitto.

Mlipo tupo na hatuko wachache.

Pimbi pimbi to kule, bila kujali jinsia zao.
 
Back
Top Bottom