Godman
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 423
- 650
Mkuu, Mimi nafikiri ifike sehemu watuletee ushahidi hapa, watuambie Magufuli ana kiasi gani cha fedha kwenye account zake iwe nje au ndani ya nchi ambazo zilikuwa kinyume na mapato yake, lakini pia watueleze Mali anazomiliki ambapo pasi na shaka zithibitike zilitokana na wizi.Kama Magufuli aliiba hivyo na bado akatuletea maendeleo yote yale; wao awamu ya nne hawakuiba mbona walishindwa kutufanyia chochote cha maana?
Awamu ya sita ambayo haiibi, imeongeza kodi, tozo, imekopa kwa namna isiyomithilika na bado inachukua misaada mbona haijafanya hata 25% tu ya aliyoyafanya Magufuli kwenye mwaka wake wa kwanza?
We need more leaders like Magufuli kuliko hawa wanaojiita watoto wa mjini wanaoiibia hii nchi bila hata aibu. Makamba acha kumtumia Zitto, njoo wewe mwenyewe utuelezee matatizo ya umeme. Tuelezeeni mna-absorb vipi shocks zinazosababishwa na athari za mgogoro wa Ukraine na Urusi.
Mwenzenu Magufuli alituvusha salama kwenye Covid-19.
Siyo kila siku kutuletea ngonjera hapa, Serikali ya awamu ya tano ilitudhihirishia kuwa nchi yetu ni tajiri na inaweza kufanya mambo makubwa ukiwa na kiongozi kama Magufuli, hawa wengine waliotangulia na waliopo wameshindwa, kazi iliyobaki ni kufadhiri propaganda ili kututoa kwenye reli.