Zitto Kabwe: Vitabu nilivyosoma Mwaka 2022

Safi sana Zitto, Sababu mojawapo ya kuwa na Watanzania wengi vilaza mitaani na katika nafasi muhimu za uongozi ni kwa sababu hawasomi vitabu.
Mbona ye msoma vitabu kawa mlamba viatu vya asiyesoma hata miongozo ya kuongoza nchi.
 
Bora hata ungesoma Quran tukufu! Ungepata nafasi ya kuiponya nafsi yako! Umejaa unafiki,udini,ukabila na udanganyifu! Endelea kulamba asali ya Hangaya huna lolote!
Na anapenda ukuu na sifa.
 


Ama kwa hakika Muheshimiwa hongera sana kwa usomaji wa idadi ya vitabu hivyo na hili limenipa hamasa nami nijitahidi angalau kwa mwaka niweze kusoma vitabu japo vichache, kulingana na muda, vitakavyoweza kukuza ufahamu wangu wa mambo mbalimbali.

Elimuni ufunguo wa maisha, Elimu ni chakula cha ubongo na elimu zinapatikana katika njia mbalimbali ikiwemo njia ya kusoma vitabu, nataka niamini kupitia vitabu nk ndio siku zote umepata nguvu ya kujenga na kutetea hoja zako katika uwanja wa kisiasa na kijamii, kudos.

Muheshimiwa, Waafrika wengi na hususan Watz ni wavivu sana katika kusoma vitabu, ni wavivu katika kusoma hata vitabu vilivyoandikwa katika lugha ya Kiswahili (lugha mama) sembuse Lugha ya kiingereza!!, ni wavivu kusoma hata maandiko ya Dini, katiba ya nchi nk.

Muheshimiwa, tufanye nini ili kahamasisha watu kujenga tabia na tamaduni ya kusoma vitabu vyenye elimu za manufaa??--- Watz wanapenda kusoma magazeti, majarida ya udaku na tamthiliya zaidi kuliko kusoma vitabu vya elimu.

Hilo ndilo jambo muhimu sana jamii inatakiwa ihamasishwe kusoma vitabu kuliko kuelezea idadi ya vitabu ulivyosoma na matokeo yake umeyaona asilimia kubwa ya watu wametoa maoni ya kukushambulia kama kwamba wewe unaonyesha majivuno mbele yao Kwamba "you are a plorific reader", hii ni sawa na uende kijijini kwa watu wasiosoma kabisa na kuanza kuongelea jambo la muhimu kwa ajili yao katika lugha ya kiingereza 🤣 watakushangaa!!!, ndio maana badala ya watu humu kuhamasika na usomaji wako wa vitabu wamekuwa mbogo na hapohapo kukushutumu na kuingiza siasa kuhusiana na ugumu wa maisha tunayopitia nchini wakijua kwamba wewe ni political figure kitu ambacho ni irrelevant mada uliyoileta.
 
Hiki kimemkimbiza mleta mada
 
Hongera sana Mwami kwa kusoma na kuweka wazi vitabu ulivyosoma kila mwaka.

Ni utaratibu mzuri na ambao mimi binafsi nimeuiga kutoka kwako na kwa mwaka huu nimesoma vitabu 40
 
Watu mpo depressed Sana
Mnasahau mwenzenu kajitoa na siasa ndo Kazi anayoitegemea kulisha Familiya na kulipa bill zake , nyie mkaa huko mnasubiri zitto awatetee ili Familiya ikose mkate wa kila siku!!
 
Hivi vitabu vimekusaidia vipi kutatua changamoto lukuki zinazowakabili watanzania kwa sasa zikiwemo mfumuko wa bei, hali duni za vipato vya watu, huduma hafifu za jamii zikiwemo maji na umeme na kuongezeka kwa kasi kwa deni la taifa kunakotishia uhimilivu wa uchumi wetu kuweza kulibeba.
 
Zitto ni mzalendo anayeipenda Tanzania zadi kuliko maslahi yake binafsi, tatizo huenda ni njia anazochagua kufikia malengo yake ya kisiasa.
Hata mimi naliamini hilo huwa natamani sana huyu bwana akiishi na kukifanyia kazi kile alichojaaliwa na Mungu watu wanaumia sana ni basi tu.
 
Hana kazi ya kufanya, Kwa nini wana siasa wengi wa Tz ni masikini sana? Jibu ni simple tu wana tegemea siasa siku zote, akitoka hapo hawezi kujiendeleza hata kibiashara, hapo zito mdomo na maneno mengi usikute Hana hata kampuni so Yuko iddle tu.

Wakati ndugu zetu wakenya wana siasa wako na pesa na wana fanya biashara, wame wekeza nchini kwao, hata kama ni pesa ya wizi Bado Ina circulate within, mfano mchukue lipumba vs odinga, odinga hadi ana chopper yake binafsi, Kwa wastani ana mawe na apartment za kutosha.

Angalia hata kina sonko wako mbali na ni watu wa kawaida, most of Kenyans politicians ni business men huo muda wa kusoma taka taka wana zitoa wapi? , Hawa wana siasa wetu ni chanzo Cha umasikini Tanzania.
 
Chadema hakuna mtu wanaemshambulia kama Zitto...kama Wana "hidden reason"...
Lowasa,Sumaye..wote kwao sio wasaliti...Dr Slaa sio msaliti...wao Zitto ndo "msaliti" wao....hata thread inahusu vitabu ...all the can share is hate
 
Badala ya kujadili vitabu watu mmeamua kumshambulia mleta vitabu, It is not fair!
Kwani vitabu vimefanyaje mkuu? maana mleta mada hajavichambua, nadhani lengo kuu la mleta mada ni kujizungumzia yeye kuwa ni msoma vitabu na ndio maana watu wanapita humo humo.
 
Kwani vitabu vimefanyaje mkuu? maana mleta mada hajavichambua, nadhani lengo kuu la mleta mada ni kujizungumzia yeye kuwa ni msoma vitabu na ndio maana watu wanapita humo humo.
Ndio ni msoma vitabu, ili awaelekeze kuhusu vitabu, mjadili vitabu, mlivyosoma na alivyosoma.
Sio kumjadili yeye binafsi au maisha yake ya siasa.
 
Chadema hakuna mtu wanaemshambulia kama Zitto...kama Wana "hidden reason"...
Lowasa,Sumaye..wote kwao sio wasaliti...Dr Slaa sio msaliti...wao Zitto ndo "msaliti" wao....hata thread inahusu vitabu ...all the can share is hate
Nadhani Thread inamuhusu Zitto zaidi kuliko vitabu, ameonyesha kuwa yeye ni msoma vitabu anaeleza vitabu vingapi amesoma na kupewa zawadi ya vitabu basi.
 
Ndio ni msoma vitabu, ili awaelekeze kuhusu vitabu, mjadili vitabu, mlivyosoma na alivyosoma.
Sio kumjadili yeye binafsi au maisha yake ya siasa.
Labda tuseme kwamba mleta mada yeye anasoma vitabu kama hobby tu na ndio maana kaishia kutaja idadi ya vitabu na kuzungumzia kupewa zawadi ya vitabu, ila members humu wao wameenda kwenye upande wa maarifa yanayopatikana kwenye usomaji vitabu na hapo ndio ikawa sababu ya kumjadili Zitto mwenyewe kama msomaji wa vitabu ambaye ni mwanasiasa na ni kiongozi wa chama cha siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…