Maswa Yetu
JF-Expert Member
- Mar 18, 2023
- 1,398
- 2,619
Zito Kabwe anayejulikana kama chawa wa serikali ya awamu ya 6 amelipuka kwa kuitolea uvivu serikali ya awamu ya 6 kwa kitendo chake cha kuendelea kumlea fisadi na gwiji la Escrow Habinder Seth.
Ikumbukwe fisadi Seth aliwekwa jela kwa miaka 4 na serikali ya awamu ya 5 , lakini mara baada ya Rais Magufuli kufariki dunia ,serikali mpya chini ya Rais Samia harakaharaka ilimwachia huru fisadi Seth na kumlipa billion 348 kinyume kabisa na maazimio ya bunge na kinyume kabisa na hukumu ya mahakama ya rufaa Tanzania, ambapo mihimili yote hiyo ilitaka Habinder Seth achukuliwe hatua kali kutokana na ufisadi alioufanya wa kuliingiza hasara taifa mabilioni ya pesa.
Kutokana na fisadi Seth kulelewa na kupetiwapetiwa na serikali ya Rais Samia, sasa amefikia hatua ya kumfungulia Zito Kabwe kesi mahakamani na kumdai fidia ya bilioni 248 kwa kosa la kumchafua mitandaoni kwamba ni fisadi wa IPTL.
Zito Kabwe ameapa kuuzika huu mzoga unaoitwa IPTL na ameonya kuwa atamuumbua kiongozi yoyote wa serikali anayeshirikiana na Habinder Seth kuliibia taifa la Tanzania. ZITO KABWE amesema safari hii haponi mtu na hataangalia usoni wala kuangalia rangi ya mtu.
View: https://youtu.be/tJcrm3gVyOI?si=Z4zQv6n2mvOCIiDU