Zitto Kabwe: Watawala wa awamu ya sita wanamwogopa Habinder Seth wa IPTL

Zitto Kabwe: Watawala wa awamu ya sita wanamwogopa Habinder Seth wa IPTL

Zito Kabwe anayejulikana kama chawa wa serikali ya awamu ya 6 amelipuka kwa kuitolea uvivu serikali ya awamu ya 6 kwa kitendo chake cha kuendelea kumlea fisadi na gwiji la Escrow Habinder Seth.

Ikumbukwe fisadi Seth aliwekwa jela kwa miaka 4 na serikali ya awamu ya 5 , lakini mara baada ya Rais Magufuli kufariki dunia ,serikali mpya chini ya Rais Samia harakaharaka ilimwachia huru fisadi Seth na kumlipa billion 348 kinyume kabisa na maazimio ya bunge na kinyume kabisa na hukumu ya mahakama ya rufaa Tanzania, ambapo mihimili yote hiyo ilitaka Habinder Seth achukuliwe hatua kali kutokana na ufisadi alioufanya wa kuliingiza hasara taifa mabilioni ya pesa.

Kutokana na fisadi Seth kulelewa na kupetiwapetiwa na serikali ya Rais Samia, sasa amefikia hatua ya kumfungulia Zito Kabwe kesi mahakamani na kumdai fidia ya bilioni 248 kwa kosa la kumchafua mitandaoni kwamba ni fisadi wa IPTL.

Zito Kabwe ameapa kuuzika huu mzoga unaoitwa IPTL na ameonya kuwa atamuumbua kiongozi yoyote wa serikali anayeshirikiana na Habinder Seth kuliibia taifa la Tanzania. ZITO KABWE amesema safari hii haponi mtu na hataangalia usoni wala kuangalia rangi ya mtu.

View: https://youtu.be/tJcrm3gVyOI?si=Z4zQv6n2mvOCIiDU

Huyu IPTL mbona anapenda sana 48? Serikali ilimlipa bil 348, anamdai Zitto fidia ya bil 248
 
Zitto kachukua form juzi huko kwao,anataka jukwaa tu kwenye mainstream waha wenzie waone bado anawika mjini.
 
Zitto kachukua form juzi huko kwao,anataka jukwaa tu kwenye mainstream waha wenzie waone bado anawika mjini.
Unamaanisha Sethi amempeleka mahakamani ili apate kiki?
 
Zitto kamchokonoa Singasinga makusudi akitegemea hii reaction yake au akitarajia kufufua huu mjadala apate airtime!

Jiulize,kwa nini iwe leo?
Anayetakiwa kuulizwa hili swali ni Singasinga, kwa nini amshitaki Zito leo?
 
Zitto kamchokonoa Singasinga makusudi akitegemea hii reaction yake au akitarajia kufufua huu mjadala apate airtime!

Jiulize,kwa nini iwe leo?
The end justifies the means bora wanasiasa wote watake airtime kwa kuzungumzia mambo kama haya na sio kupigana vijembe...

Nadhani tutapiga hatua kama Taifa tukijikita kwenye issues mfano kwanini huyu Bwana alilipwa na je alistahili kulipwa na kwanini alililetwa in the first place, na kama aliyepita alikataa kumlipa na kumtia ndani kwanini hawa washindwe ? Je alionewa ?

Hayo ya kupata Airtime au kutokupata ni mazungumzo baada ya habari
 
Umeongea kwa busara sana
 
Zito Kabwe ameapa kuuzika huu mzoga unaoitwa IPTL na ameonya kuwa atamuumbua kiongozi yoyote wa serikali anayeshirikiana na Habinder Seth kuliibia taifa la Tanzania. ZITO KABWE amesema safari hii haponi mtu na hataangalia usoni wala kuangalia rangi ya mtu.
Too late...! Hii haimpeleki Bungeni.
 
Kweli Siasa na wanasiasa ndio Kansa ya hili taifa...

Watu badala ya kuangalia issue at hand na authenticity yake ya huyu Fisadi kulipwa na upuuzi uliofanyika mnamuongolea Zitto na usaliti wake....

Even a Broken Clock is Right twice a day na tusiangalie anasema nani bali kinasemwanini ? Zaidi ya hapo tutaendelea kuwa Cheerleaders na kushangaa Matukio
Wakati mwingine kuwafungua macho Watanzania unaweza ukajijutia,unaweza kujitoa mhanga na wakakuacha peke yako na Adui akaibuka mshindi.Tupo kwenye jamii ya Watu tusiojua hata tunataka nini.Mjadala hapa ni ufisadi wa Seth na waliopo nyuma yake,sasa ni vipi Mtu huguswi na mabilioni yanayopotea unakimbilia kumsema Zito.Kama una ya kusema kuhusu Zito fungua uzi au subiri uzi wa hayo.Hapa tujadili tunavyodhulumiwa na Watawala huku mamilioni ya Watanzania wanateseka. Huwa nahisi kuna Watu huamua tu kuhujumu uzi.
 
Nyuma ya Seth Kuna mzee mmoja hasiezeeka nilishangaa Magufuli kushidwa kummaliza hata kwa sunu huyu Seth
 
Back
Top Bottom