Zitto Kabwe: Waziri afafanue kodi aliyoitangaza, kodi hailipwi na mtu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kauli kuhusu mfumo wa ulipaji kodi kwa raia wenye umri wa miaka 18 na zaidi ambaye atakuwa na TIN Namba uliopendekezwa katika Bajeti Kuu 2022/23 inatakiwa kufafanuliwa vizuri.

“Inawezekana Wananchi hawajaelewa, Waziri wa Fedha hakulieleza hili vizuri, kwani kodi haikusanywi kwa mtu, inakusanywa katika kipato au miamala ya kibiashara. Hakuna mchumi anayeweza kuja na Kodi ya Kichwa kwa Dunia ya sasa.

“Nadhani Waziri anatakiwa atumie wakati huu ambao Bunge linaendelea afafanue vizuri inawezekana alikuwa na dhamira nzuri lakini hakueleweka,” - anasema Zitto.

Binafsi napendekeza watumishi kodi wanayokatwa kwenye mishahara yao kuingizwa kwenye tin no yake
Namanisha KILA mtumishi awe na tin no, ambayo itumike pia fanyia biashara

Mfano mtumishi anakiduka pale ,analipa kodi, ya mshahara, kigamuzi ,tozo ya miamala, kabiashara kake hii sio sawa hata kidogo
 
Utaratibu wa TIN number upo muda mrefu sana,, na ukipendekeza kila mtumishi wa umma alipe kwa TIN, vipi wale wanaolipa kwa kutumia lience ya kazi!??

Hii nchi ngumu sana, nw days wenye mamlaka wanaangalia namna kumnyonya Mwananchi mpaka damu ikauke
 
Hii tabia ya wana siasa kusema uongo mfululizo ikiachwa iote mizizi bila kukemewa inaweza kuja kuleta maafa makubwa sana kwa taifa kwa kupandikiza chuki ndani ya jamii na kujikuta watanzania wazalendo wanawekwa pembeni na mafisadi ndiyo yanashika usukani wa kuongoza nchi yetu.
Kwa kuzingatia amri ya Mungu inayotutaka kutosema uongo wala kumshuhudia jirani yako uongo basi wanasiasa wafuatao wanatakiwa kujitokeza mbele ya jamii kutubu na kuwaomba radhi watanzania kwa kuwaaminisha uongo kabla ya ghazabu za mwenyezi Mungu hazijawashukia.

1. Zito Kabwe
Huyu alianza kwa kupinga ufufuaji wa shirika la ndege , akawatangazia watanzania kwamba ndege zinazonunuliwa na serikali ni mitumba hivyo hazitakuja kufanya kazi yoyote. Leo ndege hizo zimemaliza miaka 5 zikipiga kazi ya kusafirisha abiria ndani na nje ya nchi na yeye mwenyewe Zito Kabwe amekuwa mteja mkubwa wa ndege hizo.! Je ni lini Zito atatoka mbele ya jamii kukanusha uongo wake kwamba hizo ndege hazikuwa mitumba?

2. Tundu Lisu
Huyu alipinga serikali kuanzisha upya mazungumzo kuhusu mikataba mbalimbali ya madini iliyokuwa inanyonya nchi yetu. Lisu alijigeuza wakili wa kutetea Acacia na akawatisha watanzania kwamba watashitakiwa MIGA !, cha kushangaza kampuni ya Acacia walikubali matakwa ya serikali na kuunda kampuni mpya ya Twiga iliyopelekea mapato ya madini kupanda maradufu hapa nchini. Je Lisu akatubu lini kwamba aliwadanganganya watanzania?

3. Freeman Mbowe
Huyu aliwadanganya watanzania kwamba lazima wafanye lockdown ya Corona na chanjo ya Corona lazima iwe lazima Tanzania , alifikia hatua ya kuanza kufanya mikutano kwa njia ya mtandao lakini jioni akawa anaonekana bila barakoa kwenye viwanja vya bia, je alikuwa anamdanganya nani?

4. John Heche
Huyu alipinga ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) akasema watanzania waamke hakuna kipande hata cha mita moja cha reli ya kisasa kitakachojengwa,lakini sasa kipande cha Dar -Dodoma kimeshakamilika na Heche bado hajatoka hadharani kufuta uongo wake!.

5. Nape Nnauye
Huyu alitumia kila njia kupinga ujenzi wa bawawa la kufua umeme la mwl Nyerere kwamba utaleta hatari kubwa kwa wakazi wa mikoa ya kusini, lakini ujenzi wa bwawa unaendelea na umefikia 70% lakini bado Nape hajajitoleza tena kuwafafanulia wananchi hatari walizozipata mpaka sasa kutokana na mradi huo kufikia 70%. Kutokujitokeza kwake kuainisha hizo athari maana yake alisema uongo na hatujui alikuwa anasema uongo ili watanzania wasichimbe bwawa lao kwa faida ya nani.
 
Wewe ni mjinga ova!
 
Back
Top Bottom