Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Sijui watu mnashida gani au uvivu wakusoma au mazara ya tuition? Haya nimekutafunia soma hiki kipanda;

Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.

Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.
 


Huo mkataba wa bandari ya Bagamoyo uliwekwa kwenye web site gani ili Zitto aelekezwe atulete hapa tuujadili
 
Doh!! Haya mafumbo nimechemkaa mkuu


Tafuta ile clip inayoitwa fake ya mazunguzo part 3. Yuko fake mmoja chambo wa familia aliahidiwa tunu kutokana na pendekezo la mama mtu. Kwa kawaida wa africa tuko na extended family ndio nikauliza jina atapewa nani?
 
Kwa taarifa hii,inabidi tujiulize hali ikoje katika mikataba ya ujenzi wa SGR,Stiegler'"s Gorge,ununuzi wa ndege,n.k.
 
Ziko taarifa mbili, si Barick walisha weka. Subiri ufafanuzi.
Ufafanuzi wa nini wakati umeseme how come upande wa pili (serikali) wafanye siri! Ndo nakuambia kama serikali hawajafanya siri, weka taarifa ya serikali hapa! Kama ni mfuatiliaji mzuri wa haya mambo, back 2018 (or 2017 sikumbuki) wakati linatangazwa suala la 50/50, Kabudi alidanganya hadharani kuhusu arrangement ya hiyo 50/50. Tulipoingia website ya Acacia, ndipo tukagundua alichosema Kabudi ni kingine na makubalino yanasema vingine!

Kwahiyo hoja kwamba, serikali haiwezi kufanya siri kwa sababu ni makubaliano ya pande mbili, wala sio hoja sahihi kwa sababu ndo vile tu serikali hawana namna ya kuwaambia Barrick wasiweke hadharani hizi taarifa lakini wangependa sana zisiwe hadharani ili waje kutudanganya!!
 
K
Kuna wizara nchi hi nchi inaendeshwa na personalities mjomba, wewe angalia makonda alivyo na power ya kuvuka ukuu wa mkoa, same with kabudi acha kushangaa mjomba, karibu tanzania

Pole kama umesahau kuanza jina la nchi yako kwa herufi kubwa.
 


Wewe unafikiri serikali ingefanya siri kitu ambacho kisheria hakiwezi kuwa siri na kinahusisha pande mbili? Ndio maana nimesema kinacho takiwa ni ufafanuzi wa mkataba ni nini kilijiri mpaka ukaonekana kama ulivyo.
 
Zitto ametafsiri alichokisoma kwa namna livyoona yeye japo sivyo ilivyo katika uhalisia wake. Msioelewa Kiingereza na/au misamiati/lugha ya uwekezaji katika tasnia ya uziduaji mtachotwa sana na hekaya hizi za akina Zitto.
Tufafanulie wewe sasa unayezielewa hizo terminologies za uwekezaji ili tuupate ukweli ambao mh. Zitto ameupotosha.
 
Wewe unafikiri serikali ingefanya siri kitu ambacho kisheria hakiwezi kuwa siri na kinahusisha pande mbili? Ndio maana nimesema kinacho takiwa ni ufafanuzi wa mkataba ni nini kilijiri mpaka ukaonekana kama ulivyo.
Ufafanuzi upi wakati nimeshakumbia huko nyuma Kabudi alishawahi kutoa ufafanunzi na kudanganya?! Msikilize Kabudi hapa: akizungumzia suala la 50/50 litakavyokuwa! Wakati official report inasema 50 ya serikali inatokana na tax, royalties, levies, 16% na other incomes, Kabudi anasema 50% ya serikali itapatikana baada ya vyote hivyo kuondolewa, na basically serikali itakuwa inapata 70% na Acacia 30%!

Yaani ndo ufafanuzi kutoka watu kama hao ndio mara kwa mara unasisitiza tusubiri ufafanuzi wakati najua watadanganya tu?!
 
Mtu mwenyewe katoka jalalani, sasa unataraji nini kwa mtu wa aina hii?
 
Duh...Inatisha...Yawezekana mheshimiwa Zitto yuko sawa, hakuna aliyetokea kuyapinga anayosema! Prof Kabudi na kundi lao tuliokuwa tunawaamini wako kimya?!
Zile Noah kweli zilikuwa ndoto za alinacha...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…