Lowassa alikuwa hajui kumwaga sumu kwa kutumia mdomo wake. Lissu anamwaga sumu acha kabisa.Hapo CCM wanatamani wamuue tu.
Sheria na kanuni za kampeni zinakataza lugha zisizo za kiustaarabu wala staha, lugha zisizo na heshima kwa wagombea wenzako wala kwa mamlaka halali za nchi, lugha za matusi, za uwongo, za kuchochea vurugu, za ukali, lugha zilizo kinyume na maadili mema ya mtanzania ambazo watoto na vijana hawapaswi kuzisikia toka kwa watu wazima.
Tundu Lissu ukimuzuia kuongea lugha hizo atakuwa bubu kwani ndizo lugha pekee anazozijua.
Wananchi wanachotaka kusikia kutoka kwa mgombea urais ni vitu ambavyo mgombea atawafanyia wananchi na taifa kwa ujumla wakimuchagua kuwa rais wao ili kipata maendeleo. Na mambo haya ayaseme kwa lugha ya staha yenye kuwashawishi waamini anasema kweli na wakimuangalia macho yake waamini anasema ukweli.
Mgombea anapaswa kuyaelewa matatizo makuu ya msingi ya taifa letu yanayokwamisha maendeleo ambayo ni:
1. Neocolonism (Ubeberu). Maliasili na utajiri wetu zimeendelea kuporwa kwa wingi kwenda kiendeleza mataifa ya Ulaya, Asia na Amerika. Waporaji hawa (mabeberu) tumekuwa tukiwaita wawekezaji wamekuwa wakitupoza kwa tu misaada midogo midogo.
2. Rushwa
3. Utegemezi
4. Kutojiamini kuwa tunaweza
Huyu jamaa kwa kuwa hakuwapo nchini kwa miaka mitatu hajui hata mambo ambayo tayari yameshafanyika. Hususani jana kwenye sikukuu ya wakulima alizungumzia usumbufu wa kodi na mambo mengine mbali mbali waliyokuwa wakiyapata wakulima njiani wakisafirisha mazao yao. Hajui kwamba kodi hizo na usumbufu huo wa njiani JPM alisha ukomesha zamani. Itamchukua si chini ya miezi 6 kuyajua yote yaliyotendeka katika kipindi hicho cha miaka 3 alichokuwa hayupo maana mengi sana.
Jamaa huyu anapinga ujenzi wa bwawa kubwa kuliko yote Afrika la kuzalisha umeme la Nyerere (Stiegler's) kwa kuwa tayari tunayo mabwawa ya Mtera na Nyumba ya Mungu. Hivyo anaungana na hao mabeberu waliokuwa wakipinga kwa nguvu zote ujenzi wa bwawa hilo. Ikatulazimu tulijenge kwa pesa zetu wenyewe.
Jamaa anafikiri kuwa nchi kuwa na deni la mikopo kubwa kwake ni tatizo. Hajui kuwa hayo ndiyo maendeleo. Nchi jajiri ndizo zinazoongoza kwa ukubwa wa madeni ya mikopo. Hata watu majiri wana madeni makubwa ya mikopo. Masikini huwezi kuwa na madeni makubwa, kwanza hakuna atakayekukopesha kwani anajua hutaweza kurudisha mkopo. Masikini hakopesheki. Tajiri ndiye anakopesheka. Dunia imetutambua sisi ni matajiri wa kiwango cha middle income country. Hivyo madeni ya mikopo lazima yakuwe.