Zitto: Msaidizi wa Maalim Seif alinipigia simu mara 4 kutaka kunijulisha msiba sikupokea ndipo akanipigia Rais Mwinyi nikapokea kwa mujibu wa sheria

Zitto: Msaidizi wa Maalim Seif alinipigia simu mara 4 kutaka kunijulisha msiba sikupokea ndipo akanipigia Rais Mwinyi nikapokea kwa mujibu wa sheria

Nani kasema Zitto Kabwe ndio alitakiwa kutangaza kifo?

Hiyo itifaki kila mtu anaijua ndio maana Zitto Kabwe amesema aliipokea hiyo simu kwa mujibu wa sheria maana yake ni kwamba vinginevyo asingepokea angeendelea kuogopa!
Zitto ni kiongozi mkuu wa chama, unafkiri Zitto atakapopata taarifa ya msiba anatakiwa afanye nini kwenye chama kama si kusimama kwenye jukwaa akawatangazia wenzake? Ndio mana alisubiri simu ya rais ili akipata taarifa huko kuwe na kauli ya pamoja kiprotocal.,

Mkuu em niambie wewe huogopi kifo?
 
Nadhani alijua mapema alipoenda kumuona kuwa hatoboi tena, zile 📞 mfululizo alijua tu atakuwa kakiki ze baketi
 
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360 KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema siku maalim Seif alipofariki yeye alikwenda hospitali asubuhi na kuelezwa maendeleo ya mgonjwa.

Anasema ilipofika saa 5 na ushee akiwa katika shughuli za chama alipigiwa simu na msaidizi wa maalim Seif aliyekuwa anashinda pale hospitali na hakuipokea.

Akapiga tena mara tatu zaidi lakini Zitto hakupokea kwa sababu alijawa na uwoga na hakuwa tayari kupokea habari mbaya kwa wakati huo, anaeleza Zitto.

Baadae kidogo nikapigiwa na mh Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi ndipo kwa mujibu wa sheria ikanibidi nipokee na akanijulisha habari za msiba na tukakubaliana alitangazie taifa kisha nasi kama chama tukatangaza baada ya tangazo la serikali, amemalizia Zitto Kabwe.

Chanzo: Clouds TV

My take: Kiongozi anayeogopa taarifa ya msiba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu kweli? Maana 2025 Zitto anatajwa kugombea urais.

Maendeleo hayana vyama!
Wachawi na wenye asili za kichawi ndio huwa hawana woga na taarifa za misiba ya wapendwa wao...
 
Pole yake sana kwa kushindwa kupokea simu sababu ya kuhofia kupokea taarifa mbaya...
 
Nimependa approach ya raisi Mwinyi ya kumtaarifu kwanza kiongozi mwenza wa Maalim then wakakubaliana wote kwa pamoja taifa litangaziwe... Then ndo chama kikatangaza...

Nadhani huku bara Zitto angepata taarifa kupitia tangazo la serikali🤣🤣
 
Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360 KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema siku maalim Seif alipofariki yeye alikwenda hospitali asubuhi na kuelezwa maendeleo ya mgonjwa.

Anasema ilipofika saa 5 na ushee akiwa katika shughuli za chama alipigiwa simu na msaidizi wa maalim Seif aliyekuwa anashinda pale hospitali na hakuipokea.

Akapiga tena mara tatu zaidi lakini Zitto hakupokea kwa sababu alijawa na uwoga na hakuwa tayari kupokea habari mbaya kwa wakati huo, anaeleza Zitto.

Baadae kidogo nikapigiwa na mh Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi ndipo kwa mujibu wa sheria ikanibidi nipokee na akanijulisha habari za msiba na tukakubaliana alitangazie taifa kisha nasi kama chama tukatangaza baada ya tangazo la serikali, amemalizia Zitto Kabwe.

Chanzo: Clouds TV

My take: Kiongozi anayeogopa taarifa ya msiba anaweza kuwa amiri jeshi mkuu kweli? Maana 2025 Zitto anatajwa kugombea urais.

Maendeleo hayana vyama!
Kwani Zitto Kabwe siyo Binadamu. Hakuna Binadamu ambaye anauwezo wa kuvumilia kufiwa na mtu wake wa karibu.
Ila Sifa za kuwa Rais kuwa anazo au hana umezingatia nini?
Kiujumla Zitto Kabwe nimemgundua ameanza kuelewa maana halisi ya kufuata sheria
 
Hujui hata kiswahili,kuna ushupavu ktk kifo,ulisikia wapi hiyo.Habari mbaya inahitaji Ujasiri siyo ushupavu.

Mtu kuwa Rais ni maamuzi ya wananchi, kwasababu urais ni zaidi ya Ujasiri war kupokea taarifa za msiba. Ila km Ni kipimo kwa mujibu wa mtoa mada basi mtu yeyote anaweza kuwa rais ilimradi ni jasiri tu.
Umepanick eee😃😃😃😃
 
Hivi wabongo mnaelewa kweli au ni uzuzu tu yeye kasems hakutaka kupokea habari mbaya kwa wakati huo
 
Back
Top Bottom