Zitto Mshauri OMO kuwa Pragmatist,Acheni Ujinga Pelekeni Majina ya SUK, Kususa Hakusaidii KITU

Mwalimu P.
kumbe ulisha washauri mapema sana dah 🤣

Othman Masoud ana kiburi kisicho na faida kisiasa, wamejichelewesha wenyewe,
in fact na kama kuna hasara za kisiasa wamepata wenyewe ACT
 
Kwmaba zito yey kama yeye hawezi teuliwa kuwa naibu rais hapo Zanzibar
 
Mwalimu P.
kumbe ulisha washauri mapema sana dah 🤣

Othman Masoud ana kiburi kisicho na faida kisiasa, wamejichelewesha wenyewe,
in fact na kama kuna hasara za kisiasa wamepata wenyewe ACT
Naunga mkono hoja, OMO ni kibri jeuri haswa anapokutana na dhulma ama akihisi kutotendewa haki. Kwangu mimi, huyu ni mtu hatari sana!, enzi za Dr Shein, nilimshauri Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii

Na Dr. Husein Mwinyi pia nilimshauri Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu

Wagombanao, ndio wapatanao, maadam sasa wamepatana, hili ni jambo la kheri, tuwapongeze, yaliyopita si ndwele, tugange yajayo, 2030 OMO atapata na atapewa!.

P
 
nakubali mwalimu P 🤝
 
Hakuna ushauri wako uliozingatiwa hapa zaidi ya Mwinyi kukubali yaishe!
 
Kufanya jambo lile na kutarajia matokeo tofauti ni kujidanganya tu.

Mazungumzo yote tangu 90s mpaka sasa hivi CCM hawajawahi kuwa na nia ya kutenda haki.
 

Pascal unakonga vibaya. Au umeanza kunywa gongo upoteze mawazo kwa shida Za maisha. Hivi wapi OMO aikubali matokeo ? Mbona unampakazia uongo?
 
Hakuna ushauri wako uliozingatiwa hapa zaidi ya Mwinyi kukubali yaishe!
Hakuna ushauri wangu uliozingatiwa kivipi, wakati kilichofanyika leo kila kitu ni wamepita mle mle!.
Linganisha bandiko hili nimeshauri nini na nini kinatokea!.

P
 
hongera Zitto kumshauri OMO kuacha ujinga,
Hivi OMO alikuwa anafanya ujinga? Unajua ni nini kilitokea hadi kifikia maridhiano? Mkuu Wacha ujinga. Kuwa mjinga si tatizo, ila kuwa mjinga usijue kuwa wewe ni mjinga, huo ndio ujinga. Jipime wewe uko wapi? OMO atabaki kuwa OMO siku zote, kwani huyo ndiye OMO.

Nakumbuka sana bandiko lako baada ya OMO kuikataa katiba mbovu pendekezwa, lakini huyo ndiye OMO.

Zawadini
 
Hatimaye
Safi kabisa
Huu ni utekelezaji wa ushauri huu View attachment 3672925 https://www.jamiiforums.com/threads...majina-ya-suk-kususa-hakusaidii-kitu.2413666/

P
 
ACT wazalendo uchwara hawana uwezo wa kujataa SUK maana ipo kikatiba yale yalikuwa ni maigizo ya nitoke vipi. Lakini huuu mgindo wao unalea kidonda ambacho siku moja kitafumka, haiwezekani watu wamekufa zaidi ya 518 lakini wao hawaoni umuhinu wa kutafuta haki wala kuwasemea hao watu ati wanajiunga na wauaji wa oktoba 29, 2025
 
We Jamaa huwa ni mtu wa kupenda maslahi sana na unajua kupaka rangi hayo maslahi yako ya kijanjajanja huwa unaanzia mbali sana.

Ni hivi mtu kama wewe inabidi mtu uwe makini sana la sivyo kumpoteza mtu ni rahisi sanq halafu ukamgeuka na ukamsababishia matatizo makubwa.

Staili za Zito,Simbachawene,Kabudi hizi
 
Wacha kujimwambafai wataingia baada ya maridhiano ya kutaka kuinasua Zanzibar kutokana na jinamizi la uvamizi wa Tanganyika. Tatizo ni huu uvamizi .
Leo Ijumaa, uteuzi wa VP1 unafanyika leo, anaapishwa kesho, on Monday wanateuliwa mawaziri 4 wa ACT, na na kuikamilisha SUK kuhitimisha huo ujinga!
P
 
Leo Ijumaa, uteuzi wa VP1 unafanyika leo, anaapishwa kesho, on Monday wanateuliwa mawaziri 4 wa ACT, na na kuikamilisha SUK kuhitimisha huo ujinga!
P
Wanafanya hivyo kwa mujibu wa makubaliano ya maridhiano ili kubadilisha sheria, katiba na tume ya uchaguzi . C C M wakizingua wanajitoa
 
OMO ni miongoni mwa wanasiasa wasiojifunza kwa waTangulizi wake.

Maalim Seiph Sharif Hamad alisusia hadi uchaguzi mkuu, hakuambulia chochote na matokeo yake maisha magumu yakamrejesha SUK.

Sijui yeye OMO alikua anafikiria nini hata ushawishi hana,
sijui alidhani atabembelezwa na kupata nafasi kubwa zaidi ya makamu wa Rais wa kwanza wa SMZ?🐒
 
SUK ni utapeli. Sijui nani kawaroga wapinzani wakadhani CCM iko tayari kwa demokrasia ya kweli.

2030 kilio kitakuwa ni kile kile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…