Wanabodi
Pili nimetumia neno la kuudhi,waache ujinga,wapeleke majina ya chama chao kuunda SUK kule Zanzibar!. Ujinga hapa ni kufanya jambo lile lile katika mazingira yale yale na kutegemea matokeo tofauti!
View: https://youtu.be/4AWaU_8FYhQ?si=TCb3xSJiXdcuuaZ8
ACT ya sasa kule Zanzibar, tangu wakiwa Cuf, wamekuwa wakishiriki chaguzi za Zanzibar na matokeo ni yale yale, wanafanyiwa kitu kile kile, hivyo hata walipokubali kushiriki wa uchaguzi huu, walijua nini kitatokea, sasa wanasusa nini?
Natoa wito kwa Uongozi wa ACT Wazalendo, hakuna chochote msichokijua kuhusu siasa za Zanzibar, wekeni silaha chini, teuweni wawakilishi wenu kwenye GNU, pelekeni majina, rejeeni kwenye SUK, uchaguzi mwingine ni 2030.
Mungu Ibariki Zanzibar
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali