Zitto: Msitegemee nitakosoa kama kipindi cha Magufuli

Sawa kabisa; kwa kuwa vinyonga ni wengi dunia hii. Hata kwenye msafara wa mamba na kenge hawakosi.
 
Wanasiasa wote ni wachumia matumbo tu , hakuna wa kukutetea,

Chamsingi ni kufanya kazi kwa bidii na kwa kutumia maarifa aliyokupa Mungu ili uweze kujikwamua kimaisha wewe na familia yako
Umenena vema.
Agiza supu kisha niletee bill
 
Wewe ndo mdini haswa kwasababu unaangalia kila kitu kwa mizani ya dini ya mtu, tatizo watu wa CHADEMA mmejimilikisha kila kitu. Upinzani ni wenu, akili nyingi ni zenu, viongozi bora ni wenu. Yoyote alietofautiana nanyi ni adui i really wish Prof Safari na Baregu wangekuwa bado wapo CHADEMA maana hili kundi la radicals kama nyie mnaua chama kwa kujiona wajuaji na wapinga kila kitu nguvu ya kuondoa serikali hamna mnabaki kupiga kelele tu kwenye mitandao wakati hamna chochote mnachoweza kufanya. Mwenyekiti wenu mpaka leo yupo ndani karibu mwezi wa nne huu mmebaki kujidai Mungu atatulipia wakati mlikuwa mna mjaza upepo. Mwanasiasa bora ni yule anaejua nguvu zake halisi na uwezo wa kusoma muktadha kung'ang'ania nguvu wakati huna ni upuuzi maana utaendelea kuteseka tu natamani CHADEMA ingekuwa na kina Mnyika wengi kuliko radicals kama nyie msiopima muktadha bali kuendekeza vita msizoziweza.

Zitto umaarufu kapa kipindi cha JK, JK alikuwa mkristo? Zitto kipindi cha Magufuli 2015 mwishoni mpaka 2017 september alikuwa hakosoi sana kama sasa ila alibadilika kwa tukioa la Lissu kupigwa risasi je Magufuli alikuwa Muislam ?

Tuache siasa za majitaka.
 
Hivi unadhani ukosoaji kwa Mkapa utakuwa sawa na ukosoaji kwa JK, Magufuli na Samia? kila mtu ana mtindo wake wa uongozi vivyo hivyo watakosolewa tofauti, mtu katili atakosolewa kwa ukatili wake. Kama tumerudi kwenye siasa za hoja na ushindani Zitto atakosoa kulingana na muktadha huo. Nafikiri ni mtu asie mwelevu pekee ndo atatamani Zitto amkosoe Samia na serikali yake kama alivyokuwa anamkosoa Magufuli.
 
Huyo cag kastaafu kabla ya muda,watu wakitafuta mlango wa kumtupa nje,sisi siyo wajinga
 
Well said Mkuu
 
Unafanya kazi kwa bidii halafu watawala wanachukua ulichofanyia kwa bidii kwa tozo halafu Hela zinalipa mapolis kubambikia watu kesi
Ukifanya kazi kwa bidii na ukiwa na mpunga wa kutosha sizani kama tozo zitakuumiza kichwa ,
Sifukirii kama bakhresa na Mo kama tozo zinawaumiza kichwa
 
una uhakika Gwajima alipuuzwa, haya ni maoni yako nadhani siyo fact
 
Hakuna anayetegemea chochote cha maana kutoka kwake.
 
Huyo ni mwanasiasa anayetegemea siasa aendeshe maisha yake kwa hiyo ni jambo la kawaida yy kuwa CCM B kwa hiyo lazima asifu na kuabud ili mkono uende kinywan
 
Huyo cag kastaafu kabla ya muda,watu wakitafuta mlango wa kumtupa nje,sisi siyo wajinga
Wewe ni mjinga hujui shera inayohusu uteuzi wa CAG.

Sheria inasema kuwa CAG huteuliwa na rais kwa muhula wa miaka mitano, baada ya kipindi hicho cha miaka mitano rais anaweza kumteua tena kwa kipindi kingine cha miaka mitano; hawezi kutumika kwa zaidi vya vipindi viwili.

Assad unayelilia alimaliza kipindi chake cha miaka mitano; rais hakumteua kutumika kipindi kingine cha pili.
 
ZZK amekuwa cheap sana siku hizi. Kweli muda ni mwamuzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…