Zitto: Msitegemee nitakosoa kama kipindi cha Magufuli

Zitto: Msitegemee nitakosoa kama kipindi cha Magufuli

Wanasiasa wote ni wachumia matumbo tu , hakuna wa kukutetea ,
Chamsingi ni kufanya kazi kwa bidii na kwa kutumia maarifa aliyokupa Mungu ili uweze kujikwamua kimaisha wewe na familia yako
Hapa ndipo unakosea. Nadhani ni watanzania wengi wenye mawazo kama yako. Huku ni kutoona ''nje ya boksi'' na ndicho kilichafanya nchi yetu kufika hapa ilipo. Ukijifanya ''kutoona'' viongozi wanafanya nini ni lazima utakwama. Kazi zako zote unazofanya zinategea uongozi unafanya nini. Hivyo ni sahihi ungesema wananchi tusiwe mashabiki wa viongozi bali tuwe mashabiki wa uwajibikaji. Yaani tuwe mbele kudai viongozi wawajibike bila kujali ni wa vyama kama au wametoka wapi. Hivi utakubaliana na mimi nikisema kuwa hata CCM iliyo madarakani leo hii wananchi wetu tukiamua kuamka na kuwakaba koo kila wanapofanya uzembe nchi itabalika na kupiga hatua kubwa? Narudia tena maisha yako na familia yako na kesho ya watoto wako inategea viongozi wanafanya nini hivyo ni muhimu kuhakikisha tunawawajibisha.
 
Huyu mutu ya Kigoma leo imesema tusimtegemee akikikosoa Kama alivyokuwa anafanya awamu ya JPM. Nadhani anachosau zito Ni kwamba hakuna mwananchi anayetaka ukosoaji, wananchi wanachotaka ni kuona kiongozi anamsimamo na anaweza kuwatetea iwe kipindi Cha njaa au Cha neema.

Zitto anachodhania yeye ni kwamba maisha yasiasa nikukosoa nakusahau kwamba endapo utakosoa bila hoja au bila msimamo unaoonekana hakuna atakayeangaika na wewe. Akina Polepole wamejaribu kukosoa na Wana hoja ila wananchi wamewapuuza kwa sababu wanajua wanatafuta riziki ya matumbo yao na familia zao.

Gwajima alijitutumua akapuuzwa kwa sababu alielekeza hoja zake kwa manufaa yake na taasisi yake. Membe kaibuka juzi watu wamempuuza kwa sababu alipaswa kusema JpM akiwepo ila kusubiri hayupo nikujitaftia umaarufu usio na tija. Akina Mdee hakuna anayewasikiliza maana watu wmeona wazi wamethamini familia zao kuliko Taifa.

Hivyo Zitto hata ukae kimya na usifie kila kitu poa tu, wamekujua wewe unatafuta Nini kwenye siasa. Watakaodumu ni wale watakaobaki na misimamo ya asili.
Umenena na wewe usibezwe umeandika kwa ufupi lakini umesheheni mambo.
 
Huyu mtu anashangaza mno,

kwa akili zake anawaza labda sisi tunategemea siasa zake ili mambo yetu yaende.
Zitto ndivyo alivyo. Lakini anatumia weakness tulionayo watanzania ya kutegemea watu watufanyie mambo yetu. Hivyo ameshajiweka kwenye kundi la watu wenye akili na muhimu sana kwa siasa za Tanzania. Kiukweli Zitto ni ''mjanja mjanja'' fulani anayeitumia siasa kwa maslahi binafsi.
 
Wanasiasa wote ni wachumia matumbo tu , hakuna wa kukutetea,

Chamsingi ni kufanya kazi kwa bidii na kwa kutumia maarifa aliyokupa Mungu ili uweze kujikwamua kimaisha wewe na familia yako
Sawa kabisa tatizo maamuzi ya wanasiasa ya uhusino pia na kazi unazofanya. Mfano mbolea kwa wakulima, kodi kwa wafanya biashara, ajira kwa wahitimu, ni mengi. Siasa na maisha ya watu haviwezi kutenganishw

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Huwa nashangaa mno nikiwa naona Watanzania wakimkubali sana wakati binafsi ndiye Mwanasiasa mbovu, mnafiki na msaliti kuwahi kutokea Tanzania.

Mimi ni mmojawapo kati ya wanaomkubali sana Zitto Kabwe.

Actually nimekuwa nikimtakia siku zijazo aje kuwa rais wa JMT.

Lakini naona kama nimeanza kutokumuelewa uaminifu wake maana maswali yameanza kuwa mengi kuliko majibu.
 
Huyu mutu ya Kigoma leo imesema tusimtegemee akikikosoa Kama alivyokuwa anafanya awamu ya JPM. Nadhani anachosau zito Ni kwamba hakuna mwananchi anayetaka ukosoaji, wananchi wanachotaka ni kuona kiongozi anamsimamo na anaweza kuwatetea iwe kipindi Cha njaa au Cha neema.

Zitto anachodhania yeye ni kwamba maisha yasiasa nikukosoa nakusahau kwamba endapo utakosoa bila hoja au bila msimamo unaoonekana hakuna atakayeangaika na wewe. Akina Polepole wamejaribu kukosoa na Wana hoja ila wananchi wamewapuuza kwa sababu wanajua wanatafuta riziki ya matumbo yao na familia zao.

Gwajima alijitutumua akapuuzwa kwa sababu alielekeza hoja zake kwa manufaa yake na taasisi yake. Membe kaibuka juzi watu wamempuuza kwa sababu alipaswa kusema JpM akiwepo ila kusubiri hayupo nikujitaftia umaarufu usio na tija. Akina Mdee hakuna anayewasikiliza maana watu wmeona wazi wamethamini familia zao kuliko Taifa.

Hivyo Zitto hata ukae kimya na usifie kila kitu poa tu, wamekujua wewe unatafuta Nini kwenye siasa. Watakaodumu ni wale watakaobaki na misimamo ya asili.
Zitto Kabwe yuko sahihi. Hata humu JF wakosoaji wengi wa Magufuli wamebadilika including mimi mwenyewe. Wakati ule tulikosoa uvunjwaji wa haki za raia, ukosefu wa utawala bora, uwapo wa kikundi cha WASIOJULIKANA, matumizi ya taslimali za Taifa wilayani Chato.

Sasa hatuwezi kuishi kwa kukariri kukosoa Serikali hata kwa mambo mema yenye tija ambayo Rais SSH anafanya.
 
Wakati ule tulikuwa tukimsikia akitia neno zitapotolewa takwimu za serikali na taarifa mbali mbali zikiwemo za makusanyo ya mapato ya serikali, bot , takwimu, n.k

Siku hizi hatumsikii akitia neno kabisa au ndio kusema siku hizi mambo yameimarika taarifa zimekuwa za kuaminika tofauti na wakati ule?
Siku hizi hakuna kupika taarifa kama alibyokuwa anapika Magufuli
 
Atakuwa keshakabidhiwa kwa samia ale, kwa magu alikabidhiwa ili ale ngoma ikadunda. Akaamua kuwa mpinzani wa kila kitu.
images%20(5).jpg
 
Akosoe vipi wakati mkigoma yuko palee kama CO?

Tena watakuwa wanamloga sana mama samia ili mpango awe rais

Wanakigoma mnawajua vizuri?
 
Wanasiasa wote ni wachumia matumbo tu , hakuna wa kukutetea,

Chamsingi ni kufanya kazi kwa bidii na kwa kutumia maarifa aliyokupa Mungu ili uweze kujikwamua kimaisha wewe na familia yako
Kwamba hata Lissu na Mbowe pia wanaingia kwenye hiyo list ya wanasiasa wachumia tumbo?
 
Kuna mchangiaji mmoja jana kwenye Uzi flani alisema inabidi kiibuke chama kingine ambacho kiongozi wake ni mwanajeshi,hapa nishaanza kumuelewa alikua na maana gani.
 
Back
Top Bottom