Uchaguzi 2020 Zitto: Ni muhimu na ni lazima vyama makini vya upinzani kuweka Mgombea mmoja katika ngazi zote Bara na visiwani

Zito anahaha sasa zile £ laki tatu na nusu alizoahidiwa na Kuku zimeyeyuka maana kibarua chake kiliota mbawa. Sasa anahaha anapiga hesabu kwenye mabua.
 
DJ atakubali? Atataka hao wagombea wote wawe wa chama chake. Waulizwe UKAWA walichofanywa na CDM hawatakaa wasahau.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
Chadema ina wanachama wengi na wenye ushawishi mkubwa majimboni kuliko ACT unataka CHADEMA iachie nafasi ya urais kwa ACT ?

Hizi zitakuwa bangi bila shaka.
 
Kwa vyovyote vile itakuwa, kwa mazingira yeyote yale yatakuwa, ni muhimu na lazima Vyama makini vya Upinzani kuweka Mgombea mmoja wa Urais wa Muungano, Urais wa Zanzibar, Kila Jimbo la Uchaguzi la Ubunge na Uwakilishi na kila Kata ya Udiwani. Nimezunguka Vijijini, CCM INANG’OKEKA-Zitto Kabwe on twitter.
Zito kama anataka umoja yeye ndiyo anatakiwa kuwaunga mkono CHADEMA wenye mtaji mkubwa wa wanachama na wapiga kura kuliko hiyo ACT yake ambaye hata wanachama 10k haina
 
Bara inafaa iwe CHADEMA.
Hapa nchi ni moja tuu,
Uchaguzi uliopita chadema waliweka Mgombea,
Zamu hii ni zamu ya wahanga wa CUF walioko ACT.
Kuhusu zenji ,tazameni wenyewe ,ukweli unajieleza Chadema haina mtaji wa watu huku, iliyokuwa CUF ndiyo ilikuwa namtaji ambao umefilisika na kuhamia ACT
Hoja hapa ni kuingoa CCM kwanza sio kupigana vijembe.
Tunaweza kupeana conesicion fulani za kimkakati ili kubakisha uhai wa vyama vyetu
 
Washirikiane ACT na Chadema, ACT Zanzibar, Kigoma na Pwani, mikoa mingine waachiwe Chadema na Hashimu Rungwe, NCCR, TLP, UDP, Chausita na takataka zingine zishirikiane na CCM.
 
Zito kama anataka umoja yeye ndiyo anatakiwa kuwaunga mkono CHADEMA wenye mtaji mkubwa wa wanachama na wapiga kura kuliko hiyo ACT yake ambaye hata wanachama 10k haina
Hapana upande wa Zanzibar ACT wapo vzr kuliko chadema
 
Hapa nchi ni moja tuu,
Uchaguzi uliopita chadema waliweka Mgombea,
Zamu hii ni zamu ya wahanga wa CUF walioko ACT.
Kuhusu zenji ,tazameni wenyewe ,ukweli unajieleza Chadema haina mtaji wa watu huku, iliyokuwa CUF ndiyo ilikuwa namtaji ambao umefilisika na kuhamia ACT
Hoja hapa ni kuingoa CCM kwanza sio kupigana vijembe.
Tunaweza kupeana conesicion fulani za kimkakati ili kubakisha uhai wa vyama vyetu
Upo sahihi kabisa mkuu
 
Kwa vyovyote vile itakuwa, kwa mazingira yeyote yale yatakuwa, ni muhimu na lazima Vyama makini vya Upinzani kuweka Mgombea mmoja wa Urais wa Muungano, Urais wa Zanzibar, Kila Jimbo la Uchaguzi la Ubunge na Uwakilishi na kila Kata ya Udiwani. Nimezunguka Vijijini, CCM INANG’OKEKA-Zitto Kabwe on twitter.
Yamkini ni mimi na akili zangu ndizo zinazonifikirisha kufikiri kuwa vyama vya upinzani Tanzania vimepoteza DIRA na MUELEKEO kiasi kwamba wanachowaza ni kuitoa CCM madarakani Basi.

Ijapokua ndio msingi wa upinzani lakini sio monotony kiasi hicho. Ndio kwani siwasikii wakiimba nyimbo za neema juu ya nchi na wananchi imma wake fursa kwa vijana na uboreshaji wa mfumo wetu wa elimu ambao asilimia kubwa imekua ikiwafeva wenye KUMBUKUMBU na UWEZO WA KUKARIRI na kuwatupa nje ya mfumo wenye AKILI na VIPAJI ambao hawana uwezo wa kukariri na kumbukumbu zao ni ndogo.

Mfumo ambao lugha imewafelisha wengi kwakuwa swali ni lile like ila lugha ikichezewa kidogo basi naye ni rahisi kwenda alijojo, mfumo ambao hautufunzi kutatua matatizo ya jamii yetu na kutukaririsha utatuzi wa matatizo ya wenzetu na mifumo ambayo kwao imefanikiwa ila kwa kuzingati mazingira na tamaruni za kwao ambayo ukileta katika jamii zetu huku zinadunda.

Mfumo ambao umejikita katika kutengeneza watu wa zao la Hesabu, Maarifa ya Jamii na Lugha na kuwatupilia mbali watu wa mikondo mingine kama Waigizaji, Wachekeshaji, Wanamuziki, Wachezaji (mpira, gofu, kriketi, tenesi, mpira wa Pete, basketi nk.), Wale wa mikondo ya michezo ya mapigano kama Karate, Ndondi, Nk.

KELELE INAYOSIKIKA NI ADUI YETU NI CCM TU, NA LAZIMA TUMTOE. KWANINI MSIJIKITE KWENYE KUWAPA MAARIFA WANANCHI YA KUMUDU MKATE WAO WA KILA SIKU KWANZA.
 
Kwa vyovyote vile itakuwa, kwa mazingira yeyote yale yatakuwa, ni muhimu na lazima Vyama makini vya Upinzani kuweka Mgombea mmoja wa Urais wa Muungano, Urais wa Zanzibar, Kila Jimbo la Uchaguzi la Ubunge na Uwakilishi na kila Kata ya Udiwani. Nimezunguka Vijijini, CCM INANG’OKEKA-Zitto Kabwe on twitter.
Kwa tume hii ya uchaguzi, na kanuni hizi za maadili ya uchaguzi zilizotolewa na msajiri wa vyama, wapinzani hata wafanyeje na wapendweje na wananchi, CCM ni kidedea.
 
Zito Yuko sahihi adui wa taifa ni CCM hivyo lazima upinzani wawe kitu kimoja .
Ninyi watu wenye mapenzi mema piganieni kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi. La sivyo kuungana kwa upinzani hakutafua dafu. Kete mhimu ni kupambana kuweka uwanja wa ushindani "level" kwanza. Bado kuna mda wa kuhakikisha hili linafanyika. Mengine yatafuata.
 
Twende mbele turudi nyuma, Zitto ni genius wa siasa za Africa. Kama hamtaki njoo mninyonge niko hapa nafurahia ushindi wa Dr. Hussein Mwinyi na anguko la Jecha
 
Kwa vyovyote vile itakuwa, kwa mazingira yeyote yale yatakuwa, ni muhimu na lazima Vyama makini vya Upinzani kuweka Mgombea mmoja wa Urais wa Muungano, Urais wa Zanzibar, Kila Jimbo la Uchaguzi la Ubunge na Uwakilishi na kila Kata ya Udiwani. Nimezunguka Vijijini, CCM INANG’OKEKA-Zitto Kabwe on twitter.
Maji yamezidi unga. Pole Sana.
 
Ninyi watu wenye mapenzi mema piganieni kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi. La sivyo kuungana kwa upinzani hakutafua dafu. Kete mhimu ni kupambana kuweka uwanja wa ushindani "level" kwanza. Bado kuna mda wa kuhakikisha hili linafanyika. Mengine yatafuata.
Wewe unayewaambia wenzako wapiganie sio Mtanzania ?
 
Back
Top Bottom