Zitto: Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema...

Status
Not open for further replies.
Na mshahara wa dhambi ni mauti.
 
Wewe Zitto Kabwe ni mpumbavu na mzandiki mkubwa! Jana ulikuwa unaufurahia huu uvumi. Baada ya kuugundua ukweli unajifanya mtetezi. Tulikuonya na tunakuonya, acha siasa za kipumbavu!
 
Tena JK alitupia hadi picha akiwa kwenye makorido ya hospitali na tababsamu juu.

Binadamu kuugua ni jambo la kawaida,sasa sijui wengine wanajiona miungu watu hawapaswi kuugua!
 
Hii ndo post ya zitto walipoanza kutoa na kueneza uvumi wao. Yaani kubwa zima halina akili.

Kuna watu wanaudhi sana. Afu unataka serikali itoe uvumi. Wakati wewe ndo ulileta huo uvumi. Wewe ndo unatakiwa kutoa hofu ulizoleta mpuuzi mkubwa.
 
Sasa ndio umeshajishtukia, Magufuli hafi ataishi,nguvu za giza zimeshindwa kwa jina la Yesu
 
Ukiona hivyo amesha kufa kabisaa! mtakumbuka maneno yangu
 
Hakuna mwenye mamlaka juu ya afya na uhai wake. Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayetupa vyote hivyo. Hivyo hatupaswi kujivunia juu ya afya zetu au uhai wetu, wala hatupaswi kufurahia wenzetu afya zao zinapopata matatizo hata kama tutakuwa na tofauti kimitazamo/kifikra!

Nimesikitika kwa baadhi ya watu wanaoshabikia kuhusu tetesi juu ya afya ya rais wetu!
Achilia mbali upendo tunaohubiriwa kwenye dini zetu, kuna ile hali ya ubinadamu ambayo ni natural hiyo nayo wanaikosa?

Wengine wanadhani kupata matatizo ya kiafya ni adhabu kwa sababu wanazozijua wao. Je wewe au kwenye familia yako au ukoo wenu hakuna mwenye tatizo la kiafya? Kama wapo unadhani ni kwa sababu wamefanya machukizo kama unavyofikiria kwa mwenzio kwa hiyo wanaadhibiwa? Kuna wengine kiafya hatuko wazima na wengine tumepoteza wapendwa wetu. Je na sisi tunaadhibiwa au wapendwa wetu waliotutangulia ni kwa sababu walikuwa wakosaji sana?

Nimesikitika sana kwa response ya baadhi yetu baada kuwepo kwa taarifa za uvumi juu ya tetesi za afya ya rais wetu!

Kibusara kabisa hata kama mtu mna tofauti naye kwenye suala kama hili ni vema ukawa kimya kama utashindwa kutoa pole au kufanya dua yako kwa kumoumbea nafuu! Hakuna anayeijua kesho yake hasa kiafya na uzima, Mungu pekee ajua! Wala afya zetu zisitufanye tukajivuna sana dhidi ya wale wanaopitia changamoto za kiafya!

Mungu ni wetu sote! Tuishini kwa upendo na wala ubaya haushindwi kwa ubaya bali kwa wema!

Mungu amtie nguvu rais wetu na ampe wepesi kwa matatizo yanayomkabili juu ya afya yake na uongozi wa nchi yetu!

Mungu ibariki Tanzania
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…