Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Mkuu hebu nisaidie alisemaje hawa wanaomshutumu naona wanamkandia tu ili tupime mizani
Nenda Twitter utakuta alichoongea.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hebu nisaidie alisemaje hawa wanaomshutumu naona wanamkandia tu ili tupime mizani
Ingia ikulu mawasiliano you tube anaapisha viongoz leo Mira huu
Zitto ni mchawi kama wachawi wengineIla kuna watu wanafiki sana na zito ni mmoja wao... hivi JPM akipatwa na mabaya wewe utafaidikaje?
Na mshahara wa dhambi ni mauti.Nikikumbuka jinsi Tundu Lissu;
●Alivyopigwa risasi Bungeni
●Alivyonyimwa matibabu na Govt
●Alivyonyimwa mshahara
●Alivyoporwa ubunge
Kwa kweli sasa nimeamini malipo ya ubaya ni hapa hapa duniani.
Ukimtendea ubaya mwenzio nawe utalipwa kwa ubaya.
Wewe Zitto Kabwe ni mpumbavu na mzandiki mkubwa! Jana ulikuwa unaufurahia huu uvumi. Baada ya kuugundua ukweli unajifanya mtetezi. Tulikuonya na tunakuonya, acha siasa za kipumbavu!Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:
Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.
Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.
Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.
Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.
Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.
Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
Tena JK alitupia hadi picha akiwa kwenye makorido ya hospitali na tababsamu juu.Msemaji wa Serikali anapaswa aseme jambo kuhusu hili.
Mbona JK aliumwa ngiri (Waliita tezi dume), akatangaza!
Kama kuna ukweli basi tumuombee.
Tunafahamu kuwa kuna mengi ya haki na yasiyo ya haki aliyoyafanya yaliwaumiza wananchi.Wala tusiombeane mabaya..tuombe yote mawili uzima wa afya na kubadilika kwa kiongozi wetu.
Hakika Mwenyezi ndie mwenyezi kujua
You tube ukuluMmmh, huyu aliyesema yuko live anamaanisha nini?
You tube ukulu
Sasa ndio umeshajishtukia, Magufuli hafi ataishi,nguvu za giza zimeshindwa kwa jina la YesuNimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:
Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.
Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.
Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.
Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.
Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.
Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
Umewahi kujiuliza kwa waliofanyiwa mabaya na jiwe?Ila kuna watu wanafiki sana na zito ni mmoja wao... hivi JPM akipatwa na mabaya wewe utafaidikaje?