Serikali hii sio rafiki na wafanyabiashara.
Mfano, Serikali imekuwa wafanyabiashara wao wenyewe kwa kuanza kufuta mashirika binafsi ya Mawakala wa meli (shipping agent) na kufanya wao kazi za uwakala wa meli.
Nasema imeamua kuyafuta indirect, serikali inapotunga sheria kuwa kazi zote za shipping agent, atafanya yeye kasoro Meli za Container, maana yake yale makampuni yaliokuwa yanafanya kazi ambazo sio meli za container hawatakuwa na kazi na automatically watafunga biashara zao.
Ni kodi zao kiasi gani itapotea?
Wafanyakazi wangapi wanarudi mtaani?
Katika dunia ya sasa ambayo bandari jirani wanaweka ushindani zaidi, sisi tunaondoa ushindani kwa kuwanyima wenye meli kuwa na uamuzi wa kumtumia wakala wanayemtaka, huku tozo za kodi zikiwa juu, tutegemee mzigo unaoshushwa Dar kupungua kwa kiasi kikubwa, hasa transit cargo na kuhamia Mombasa na beira.
Kupanga ni kuchagua, huwezi ukawa adui wa wafanyabiashara, vilio ni vingi sana, wakati mwingine Mungu hawezi akaruhusu serikali kufanikiwa, anaposikia vilio vya watu wanaoumizwa kutoka kila kona.
TASAC (wakala wa meli wa serikali)
1) Yeye ni regulator kwa makampuni yote ya shipping agent (sijui anaji regulate vipi yeye mwenyewe maana na yeye pia ni wakala na ni regulator)
2) Yeye ni Wakala wa Meli (shipping agent) kwa sheria inayompa kufanya kazi almost zote kasoro container
3) Yeye ameweka sheria kuwa ni lazima afanye Tallying, mzigo wowote unaoshuka yeye anatoa huduma ya Tallying KWA LAZIMA, na ameweka rate kubwa mno, mwenye mzigo hana uchaguzi kuwa afanye tally au laa kama mwanzo. Mfano, mzigo wa ngano ton elfu 40, saivi wanalipa dola 18,000 ambayo kabla walikuwa hawalipi. Halafu wanaulizwa how do they tally ngano, hawana majibu. Huu ni wizi na kupandisha bei ya bidhaa bila sababu ya msingi.
4) Yeye ameweka sheria lazima afanye clearing and forwarding ya aina ya mizigo almost more than 50% inayoshuka, hizi kampuni za clearing zitafanya kazi gani?
5) Tasac huyohuyo anakusanya 1.3% ya mapato yote ya kampuni binafsi za shipping agent kabla ya matumizi yao.
6) Tasac huyohuyo anakusanya kodi ya mzigo kutokana na mahali ulipakiwa.
Yaani kila kitu sasa bandarini ni Tasac, Tasac, Tasac., mzigo.mmoja, Tasac anatozo lukuki
Tunasubiri anguko la uchumi kwa maamuzi haya mabaya waliofanya ktk sekta ya bandari, na watakapotaka kurudi, itakuwa too late
Sent using
Jamii Forums mobile app